Skip to main content

Posts

LEO NI SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, UNANAFASI GANI HAPO ULIPO?

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:::- MAZINGIRA ni vitu vyote vinavyotunzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai.  Vitu vyenye uhai, ni pamoja na mimea na wanyama, lakini visivyo na uhai ni pamoja na hewa, maji na ardhi.  Maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho, hutegemea mahusiano mazuri kati ya watu na mazingira . KWANINI TUYAHIFADHI MAZINGIRA? Hifadhi ya mazingira  ni juhudi zinazofanywa na binadamu, ili kuhakikisha dunia anamoishi usiharibiwe na utendaji wake, bali uweze kuwafaa watu wa vizazi vijavyo. Tunatakiwa tutunze mazingira, kwani tukiyachafua tutapata magonjwa ya mlipuko kama vile kipindu pindu na mengine mengi. SABABU ZA MATOKEO YA UCHAFUZI WA MAZINGIRA Binadamu ndiye anayehusika na uchafuzi wa mazingira, na maendeleo yake ya viwanda na teknolojia na ukuaji wa idadi ya watu ni sababu zingine, zilizo wazi za kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira. Katika miaka ya hivi karibu...

PEGAO, TAMWA, ZAFELA WAUPIGA MWINGI PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: FAMILIA tatu zenye watu wa makundi tofauti wakiwemo wenye ulemavu, na wananchi 82 wamejiunga na elimu ya watu wazima miezi mitano iliyopita, baada ya taasisi za ZAFELA, PEGAO na TAMWA kuibua changamoto hizo. Tasisi hizo kwa sasa, zinaendelea na utekelezaji wa mradi wa miaka minne, wa Ku wawezesha Wanawake Kudai haki zao za uongozi, demokrasia na siasa ‘SWIL’ chini ya ufadhili wa      Ubalozi wa Norway. Akizungumza na waandishi wa habari ofis za PEGAO leo Juni 2, 2022, Mkurugenzi wa Jumuiya hiyo, Hafidh Abdi Said, alisema jengine ambalo limeibuliwa na kufanyiwa kazi, ni kujitokeza wanawake 40 wanaotarajia kuingia kwenye uchaguzi mkuu. Alieleza kuwa, wanawake hao wamedhamiria kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2025, na PEGAO wamejiandaa kuwapa mafunzo, ya kuwajengea uwezo. Hafidhi, alieleza kuwa jengine kwa sasa wameshawafikia wananchi 3,222 kuwapa elimu ya umuhimu wa uongozi kwa wanawake. Kati ya wananchi hao, wanawake wal...

MTANGAZAJI ITV AIBUKA MSHINDI WA JUMLA 'EJAT' 2021/2022

  Masekepa Natisa Asangama  wa  Kituo cha Runinga  cha  ITV ameibuka Mshindi wa Jumla wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2021. Aliwashinda wanahabari wengine watatu  – Nusra Kichongapishi  wa runinga ya mtndaoni ya TIFU , Sanula Athanas  wa  Nipashe  Herieth Makweta  wa Mwananchi. Ansangama  alishinda tuzo mbili  – Tuzo ya Wazi na Utalii na Uhifadhi  kwa runinga. Alitangazwa Mshindi wa Jumla wa EJAT na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye katika kilele cha tuzo hizo kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Mei 28,2021. Waziri  alimkabidhi  Mshindi huyo wa Jumla Tuzo, cheti  na hundi ya mfano ya kiasi cha sh. Milioni 3. Fedha hizo zimetolewa na mshiriki kiongozi wa EJAT , Baraza la Habari  Tanzania, kumwezesha  mshindi huyo kujiendeleza kwa masomo. Kushinda Tuzo ya Wazi  aliwashinda watangazaji wawili wa kituo cha runinga cha S...

NDIMARA MWANDISHI NGULI TANZANIA AIBUKA MSHINDI

  Mhariri mkongwe, mchapishaji na mkufunzi,  Ndimara Tegambwage,  ametunukiwa tuzo ya Mafanikio ya Maisha ya Uandishi wa Habari (LAJA) kwa mwaka 2022.   Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa, aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kama Mgeni Rasmi wa sherehe za Tuzo  za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania   (EJAT) 2021  zilizofanyika  katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam alimkabdihi  Ndimara Tuzo ya LAJA . Pia  alimkabidhi hundi ya mfano ya sh. milioni  10  kama zawadi ya LAJA. Jina la Ndimara kama mshindi wa  LAJA  lilitangazwa na Waziri wa  Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye  baada ya  mtangazaji veterani  Rose  Haji  kusoma  wasifu wake. Ndimara  ana uzoefu mkubwa wa zaidi ya miaka 40 katika vyombo vya habari. Miongoni mwa michango yake katika tasnia ya habari alikuwa mmojawapo wa waliochagiza kuanzishwa...

SABABU YA KUFUNGWA JELA MAISHA HII HAPA

  Mahakama ya Wilaya Nkasi Mkoani Rukwa imemhukumu kifungo cha maisha jela Peter Malema (21) Mkazi wa Kijiji cha Nkundi Kata ya Kipande Wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka Mtoto wa miaka 4. Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Benedict Nkomola amesema Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani kwa kosa hilo. Upande wa mashitaka ukiongozwa na Waendesha mashitaka Denis Chagike na Sedrick Mashauri wameieleza Mahakama hiyo kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo March 23, 2021 katika Kijiji cha Nkundi ambapo alimbaka Mtoto huyo wa miaka 4 na kumsababishia maumivu makali. "Mtuhumiwa hili ni kosa lake la pili la ubakaji na katika kosa la kwanza aliwai kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na aliondolewa baada ya kushinda rufaa" (chanzo Milard Ayoo)

HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU ZAZIDI KUPIGIWA CHAPUO

                                    NA ZUHURA JUMA, PEMBA USHIRIKIANO unahitajika zaidi katika kuhakikisha kunakuwa na ukondoishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu, ili wapate haki zao za msingi. Akiwasilisha mada katika mkutano wa Mtandao wa Wilaya wa Mpango Jumuishi wa Maendeleo katika Jamii (CBID), Mshauri kutoka Shirika la watu wenye ulemavu la Norwey (NAD) Christine Cornick alisema, wamekuwa wakifanya kazi na mtandao huo, ili kuisaidia kuleta mabadiliko katika jamii. Alisema kuwa, ushirikiano wa pamoja ndio utakaoleta nguvu ya kufanya kazi na kuleta mabadiliko ya haraka katika ukondoishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika nchi mbali mbali. "Katika mtandao huu tumeshirikisha watu mbali mbali, wanakuwa na sehemu ama mahala ambapo wanakutana na kubadilishana uzoefu katika ngazi mbali mbali na kutoa maamuzi ya kujenga jamii iliyobora", alisema Mshauri huyo. Alifahamisha kuwa, watu wenye u...

SUCCESSFUL COMBINED SURGERY AT ABDALLA MZEE PEMBA HOSPITALI

  BY HAJI NASSOR, PEMBA::::::: OCTOBER 25, 2021 was a memorable day for Dr. Wang Juan, an obstetrician and gynecologist at the First Affiliated Hospital of Soochow University and a member of the Chinese Medical Team in Zanzibar. She had barely worked at Abdulla Mzee Hospital on the Pemba Island for one month when she encountered acomplicated case. Although she had an experience on the case before her arrival on the islands, she was still shocked by the complexity of the illness of her patient, a 21-year-old mother from Matele Chake Chake. The patient had been leaking urine for nearly seven months with a foul smell which made her so embarrassed that she always remained in her house. According to the Assistant Director of Abdulla Mzee Hospital and Head of Obstetrics and Gynecology, Dr. Aboud, the patient had delivered a healthy child by cesarean section five years ago. Seven months ago she expected her second child with a great joy but the baby died during childbirth due to...

KESI YA TUHMA DAKTARI KUMBAKA MTOTO MARA TATU PEMBA KUNGURUMA TENA LEO MAHAKAMANI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::::: MAHAKAMA ya Mkoa Wete, leo itaendelea tena na shauri la ubakaji linalomkabili, daktari Is-haka Rashid Hadid, wa Kituo cha Afya Gombani, baada ya wiki iliyopita kupelekwa rumande. Leo, Mahakama hiyo maalum ya makossa ya udhalilishaji, chini ya Hakimu Ali Abdur-haman Ali,inatarajia kuwasikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka, ambapo awali ilidaiwa upelelezi umeshakamilika. Mtuhumiwa huyo ambae ana makosa manne, matatu ni kudaiwa kumbaka mtoto mwenye 16 na la pili ni kumtorosha kutoka kwenye himaya ya wazazi wake. Awali akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Juma Mussa , alidai kuwa, mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto huyo, ambae yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake. Alidai kuwa, baina ya Aprili 21, mwaka huu mtuhumiwa huyo alimtorosha mtoto huyo, kutoka nyumbani kwao Gombani wilaya ya Chake chake mkoa wa kusini na kumpeleka nyumbani kwake Kangagani wilaya ya Wete. Ambapo baada baada ya kumtorosha, us...

WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA WATUNUKIWA VYETI, KISHA WAPEWA NENO

  NA MWANDISHI WETU, PEMBA::____------ JANA Mei 26, 2022, wasaidizi wa sheria kutoka majimbo 18 ya uchaguzi kisiwani Pemba, wamemaliza na kisha kutunukiwa vyeti vyao, baada ya kumaliza mafunzo ya siku 15 ya wasaidizi wa sheria. Aliyekabidhi vyeti hivyo, kwenye hafla iliyofanyika Gombani Chake chake, alikuwa Afisa Mdhamini Afiri ya Rais, Katiba, Sheria, Utamishi na Utawala Bora Pemba, Hali Ali Khamis. Kwenye hutuba yake, aliwataka wasaidizi hao wa sheria, kwenda kuisadiai jamii, ili kupunguza majanga kama ya udhalilishaji, dawa za kulevya, migogoro ya ardhi na ndoa. Hata hivyo aliwataka wasibweteke na elimu ya awali ya sheria walioipata, na badala yake, wabuni mbinu za kujiendeleza ili kupanua wigo, wa utoaji msaada wa kisheria. Aidha aliipongeza Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, kwa kuendelea kuijengea uwezo wa kisheria jamii ya Zanzibar. Mkurugenzi wa Idara hiyo Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema pamoja na kumalizika kwa mafunzo hayo y...