NA HAJI NASSOR, PEMBA:::
FAMILIA tatu zenye watu wa makundi tofauti wakiwemo wenye ulemavu, na
wananchi 82 wamejiunga na elimu ya watu wazima miezi mitano iliyopita, baada ya
taasisi za ZAFELA, PEGAO na TAMWA kuibua changamoto hizo.
Tasisi hizo kwa sasa, zinaendelea
na utekelezaji wa mradi wa miaka minne, wa Kuwawezesha Wanawake Kudai haki zao za uongozi, demokrasia na
siasa ‘SWIL’ chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofis za PEGAO leo Juni 2, 2022, Mkurugenzi wa Jumuiya
hiyo, Hafidh Abdi Said, alisema jengine ambalo limeibuliwa na kufanyiwa kazi,
ni kujitokeza wanawake 40 wanaotarajia kuingia kwenye uchaguzi mkuu.
Alieleza
kuwa, wanawake hao wamedhamiria kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2025, na
PEGAO wamejiandaa kuwapa mafunzo, ya kuwajengea uwezo.
Hafidhi,
alieleza kuwa jengine kwa sasa wameshawafikia wananchi 3,222 kuwapa elimu ya
umuhimu wa uongozi kwa wanawake.
Kati
ya wananchi hao, wanawake waliofikiwa ni 1,971 na wanaume 1,251 ambapo mradi
huo unatarajiwa kutia nanga mwaka 2024, na ukidhamiria kuwafikia wanawake 6,000.
Mkurugenzi
huyo alisema, kazi iliyofanywa na wahamasishaji jamii 40, ambapo 10 kutoka kila
wilaya, ilisaidia mno maendeleo ya mradi huo.
Kwa
upande wake Mratibu wa mradi huo Dina Juma Makota kutoka PEGAO, alisema
wamewaibua wananchi 11, ambao walishakata tamaa kupata vitambulisho vya
mzanzibari mkaazi, na sasa tayari wanavimiliki.
‘’Wapo
wengine wanne, wanaendelea na utaratibu wa kufuatilia na kulipa kwa ajili ya
kupata vitambulisho hivyo, ambapo hilo ni eneo moja la changamoto
walizoziibua,’’alieleza.
Aidha
Mratibu huyo alisema, jambo jengine, ambalo liliibuliwa kila wanapokutana na
jamii, na ubovu wa miundo mbinu kama ya barabara na ukosefu wa huduma kama za maji
safi na salama.
‘’Kuhusu changamoto ya kwanini wanawake hawaonekani kugombea nafasi za uongozi, walitueleza wanazungukwa na rushwa na ngono na fedha,’’alieleza.
Mapema
muhamasishaji jamii kutoka ‘PEGAO’ wilaya ya Wete Raya Said Ali, alisema bado
kuna muitikio mdogo kwa wananchi kuhudhuria kwenye mikutano.
‘’Inatubidi
wakati mwengine tuwapitie wananchi kwenye makaazi yao, kuwataka washiriki
kwenye mikutano yetu, na wanaokuja hupata manufaa,’’alisema.
Mwisho wa utekelezaji wa mradi wa Kuwawezesha Wanawake Kudai
haki zao za uongozi, demokrasia na siasa ‘SWIL’ unatarajiwa wanawake
wasiopungua 6,000 iwe wamesha wezeshwa kudai haki zao.
Mradi huo uliozinduliwa Novemba, 2020, na ukitarajiwa kutia
nanga mwaka 2024, watu 100 wakiwemo wanawake na wanaume, iwe tayari wameshajengewa
uwezo, ili nao sasa kuwafikia wanawake 400, ambao nao wenyewe wanatarajiwa
kuwafikia wanawake hao 6,000.
Idadi hiyo wanawake 6,000 watakaofikiwa, ni sawa na PEGAO, TAMWA
na ZAFELA kuwafikia wanawake 1,200 kwa kila mkoa mmoja, kati ya mitano ya
Unguja na Pemba.
Ambapo hapo ni sawa na wanawake 546 kutoka kila wilaya moja,
kati ya wilaya 11, ambapo Pemba zipo nne na Unguja saba.
Zanzibar yenye majimbo 50 ya uchaguzi, hivyo utaona kuwa, mradi
huu wa ‘SWIL’ sasa utawafikia wastani wa wanawake 120, kutoka kila jimbo moja
la uchaguzi, sawa na kufikiwa wanawake 55 kwa kila wadi moja, kati wadi 110 za
Unguja na Pemba.
Mwisho
Comments
Post a Comment