Masekepa Natisa Asangama wa Kituo cha Runinga cha ITV ameibuka Mshindi wa Jumla wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2021.
Aliwashinda wanahabari wengine watatu – Nusra Kichongapishi wa runinga ya mtndaoni ya TIFU , Sanula Athanas wa Nipashe Herieth Makweta wa Mwananchi.
Ansangama alishinda tuzo mbili – Tuzo ya Wazi na Utalii na Uhifadhi kwa runinga.
Alitangazwa Mshindi wa Jumla wa EJAT na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye katika kilele cha tuzo hizo kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Mei 28,2021.
Waziri alimkabidhi Mshindi huyo wa Jumla Tuzo, cheti na hundi ya mfano ya kiasi cha sh. Milioni 3.
Fedha hizo zimetolewa na mshiriki kiongozi wa EJAT , Baraza la Habari Tanzania, kumwezesha mshindi huyo kujiendeleza kwa masomo.
Kushinda Tuzo ya Wazi aliwashinda watangazaji wawili wa kituo cha runinga cha Star – Naishook Alais Makaseni na Sudi Shaaban Ally na kwa Tuzo ya Uhifadhi na Uhifadhi alikuwa mteule pekee.
Nusra alikuwa mteule pekee na kushinda Tuzo ya kilimo na Biashara ya Kilimo kwa vyombo vya habari vya mtandaoni na piaalishinda Tuzo ya Elimu, ambapo Athanas alishinda Tuzo ya Sayansi na Tuzo ya Haki za Bindamu na Utawala Bora na Herieth alishindaTuzo za Hedhi Salama na Afya.
Kushinda Tuzo ya Sayansi na Teknolojia , Athanas alimshinda To win Elizabeth Edward Kusekwa wa Mwananchi wakati Herieth Makweta alikua mteule pekee kwa Tuzo ya Hedhi Salama na alimshinda Khamisuu Abdallah Ali wa Zanzibar Leo na Christina Mwangakale wa The Guardian.
Ephrahim Edward Bahemu wa Mwananchi alishinda Tuzo ya Uchumi, Biashara na Fedha akimshinda Francis Dhamira Kajubi wa The Guardian na Mariam Shaban Mbwana wa Mwananchi.
Michezo na Utawala Tuzo yake ilitwaliwa na Maryam Salum Habib wa Zanzibar Leo akimshindwa mwandishi mwingine wa gazeti hilo Hanifa Salim Mohamed.
Kwa Radio Tuzo hiyo imeenda kwa Said Seleman Lufune wa City FM aakimshinda Adam Gabriel Hhando wa CG FM wakati Paschal Michael Buyaga wa TBC1 tuzo hiyo kwa runinga akimbwaga Amour Khamis Ali wa Zanzibar Cable TV.
Aurea Simtowe wa Mwananchi alishinda Tuzo ya Elimu kwa magazeti akimshinda mwandishi mwenzake wa Mwananchi Tumaini Msowoya na Abdi Juma Seleman wa Zanzibar Leo.
Naishhoki Alais Makasemi wa kituo cha runinga cha Star alishinda Tuzo ya Elimu .
Beatrice Philemon Mkocho aloshinda Tuzo ya Utalii na Uhifadhi kwa magazeti wakati Najjat Hajj Omar wa The Chanzo – online alitwaa Tuzo hiyo kwa vyomvo vya habari vya mtandaoni.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi ilitwaliwa na Salum Vuai Issa wa Zanzibar Leo.
Uandishi wa Habari wa Data Tuzo yake ilitwaliwa na Francis Dhamira Kajubi wa The Guardian akimshinda Ephrahim Edward Bahemu wa Mwananchi.
Isakwisa Njole Mbyale wa Highlands FM Radio alitwaa Tuzo hiyo kwa Redio ambapo Khalifa Said Rashid wa The Chanzo alishinda tuzo kwa vyomvo vya habari za mtandaoni akimshinda Daniel Samson wa Nukta Habari Blog.
Joe Beda Rupia wa Jamhuri alishinda Tuzo ya Utawala Bora na Uwajiobikaji kwa magazeti ambapo kwa runinga TRuzo hiy ilitwaliwa na Sudi Shabaan Ally wa Star TV na Lukelo Francis Haule wa The Chanzo alishinda tuzo hiyo pia.
Halfan Chusi wa Nipashe na mwandishi mwingine wa Gazeti hilo Sanula Athanas waliwashunda wateule wengine wawili – mfa yakazi mwenzao Marco Zephania Maduhu na mwandishi mwingine Hadija Rajabu kushinda tuzo ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Tuzo ya Mpiga Picha Bora kwa Magazeti ilitwaliwa na Sabato Mwafiri Kasika wa Nipashe wakati Munira Abdillah Hussein wa BBC Swahili alishinda Tuzo ya Mpiga Picha Bora Runinga akiwashinda Festo Charles Lumwe wa Dar 24 na Peter Simon Rodgers wa ITV.
Muhidini Ally Msamba wa The Guardian alishinda Tuzo ya Mchora Katuni Bora kwa Magazeti.
Amina Ahmed Mohamed wa Zanzibar Leo aliwashinda wanahabari wawili wa Nipashe – Mary Geofrey Mashina na Augusta Mathias Njoji kutwaa Tuzo ya Jinsia na Watoto.
Kwa Redio Tuzo hiyo iliendwa kwa Gladness Joseph Msetti wa U FM Radio ya Azam Media akimshinda Adam Hhando wa CG FM.
Kwa vyombo vya mtandaoni mshindi wa Tuzo ya Jinsia na Watoto ni Harith Jaha Ally .
Tuzo ya kuripoti Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini imetwaliwa na Joyce David Joliga wa The Citizen akimshinda Elizaberth Cornery Zaya wa Nipashe. Kwa vyombo vya habari vya mtandaoni Tuzo imeenda kwa Mariam Ngollo John wa Nukta Habari Blog.
Irene Nicholaus Mwasomola wa Uhuru alishinda Tuzo ya Kuripoti Watu Wenye Ulemavu akiwashinda wateule wengine wawili- Habiba Zarali Rukuni na Haji Nassor Mohamed wa Zanzibar Leo.
Tuzo ya Afya kwa Redio imetwaliwa na Adam Gabriel Hhando wa CG FM akimshinda Isakwisa Njole Mbyale Highland FM Radio.
Jackline Inyas Silemu wa ITV alishinda Tuzo ya Afya na mtandaoni Tuzo hiyo imeenda kwa Zuhura Hassan Makuka wa Dar 24.
Tuzo ya Hedhi Salama kwa Redio imeenda kwa Peter Lugendo John wa TBC FM akiwashinda wateule wengine wawili Jecha Simai Jecha wa ZBC FM na Lugendo Ibrahim Madege wa UFM Radio.
Kwa runinga tuzo hiyo imeenda kwa Salma Msichoke Mrisho wa Star TV akimshinda mfanyakazi mwenzake Omary Hussein Omary.
Baraka Jailos Messa wa Habari Leo alishinda Tuzo ya Ushirika ambapo kwa Rdio Tuzo hiyo imetwaliwa na won the Reporting Martha Stephen Nalimi wa Shamba FM.
Elizabeth Edward Kusekwa wa Mwananchi alishinda Tuzo ya Kundi la Wazi kwa magazeti akimshinda Marco Zephania Maduhu.
Haji Nassor Mohamed wa Pemba Today alishinda Tuzo ya Kundi la Wazi kwa vyombo vya mtandaoni.
Comments
Post a Comment