NA HAJI NASSOR, PEMBA:::-
MAZINGIRA ni vitu vyote
vinavyotunzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai.
Vitu
vyenye uhai, ni pamoja na mimea na wanyama, lakini visivyo na uhai ni pamoja na
hewa, maji na ardhi.
Maisha
ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho, hutegemea mahusiano mazuri kati
ya watu na mazingira.
KWANINI TUYAHIFADHI MAZINGIRA?
Hifadhi ya mazingira ni juhudi
zinazofanywa na binadamu, ili kuhakikisha dunia anamoishi
usiharibiwe na utendaji wake, bali uweze kuwafaa watu wa vizazi
vijavyo.
Tunatakiwa
tutunze mazingira, kwani tukiyachafua tutapata magonjwa ya
mlipuko kama vile kipindu pindu na mengine mengi.
SABABU ZA MATOKEO YA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
Binadamu ndiye
anayehusika na uchafuzi wa mazingira, na maendeleo yake ya viwanda na
teknolojia na ukuaji wa idadi ya watu ni sababu zingine, zilizo wazi za
kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira.
Katika miaka ya
hivi karibuni, kwa njia hii uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira,
uzalishaji wa taka, kukata na kuchoma misitu, unyonyaji ovyo wa maliasili,
shughuli zote zinazohusiana na tasnia, madini, kilimo, biashara, unyonyaji wa
mafuta.
HISTORIA YA SIKU YA MAZINGIRA
Tangu mwaka wa 1974, siku ya mazingira duniani
huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 mwezi wa Juni, hushirikisha serikali,
mashirika ya biashara, na raia ili kushughulikia masuala nyeti kabisa ya
mazingira.
Kongamano
la Umoja wa Mataifa la mwaka wa 1972 kuhusu mazingira ya kibinadamu mjini ‘Stockholm’
Uswis, lilikuwa kongamano la kwanza kabisa la Umoja wa Mataifa.
Na
hapo neno “mazingira” kwenye anwani
yake, kuundwa kwa shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ni mojawapo
ya matokeo makuu ya kongamano hili, lilianzisha mambo mengi.
UNEP
iliundwa kwa urahisi kama kitengo cha Umoja wa Mataifa cha kushughulikia
mazingira duniani.
Shughuli
zitakazoendelezwa katika mwaka wote wa 2022 zitaangazia hatua kuu, zilizopigwa
na yatakayojiri katika miongo ijayo.
Siku
ya mazingira dunia, ni sawa na siku kuu ya Umoja wa Mataifa ya kuhamasisha na
kuchukua hatua za kushughulikia mazingira duniani.
Kwa
miaka mingi, imekuwa jukwaa kubwa zaidi la kimataifa la kuhamasisha umma kuhusu
mazingira na huadhimishwa na mamilioni ya watu kote, ulimwenguni.
MAADHIMISHO YA MWAKA 2022
Maadhimisho ya
siku ya Mazingira duniani, katika mwaka 2022, yataendeshwa chini ya kaulimbiu ‘dunia moja’ na inatoa wito wa kufanyia
marekebisho sera na maamuzi yetu, ili kuwezesha kudumisha usafi.
Kutochafua
mazingira na kuishi kwa njia endelevu na mazingira, sayari hii ndiyo makaazi
yetu tu, na ni sharti tulinde rasilimali zake zinazoweza kuisha.
‘Dunia moja’ ilikuwa kaulimbiu ya kongamano
la Stockholm la mwaka wa 1972, lililopelekea kuanzishwa kwa shirika la mazingira
la Umoja wa Mataifa (UNEP).
Miaka 50
baadaye, dunia inapoendelea kushuhudia changamoto za aina tatu duniani za
mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira, uchafuzi na taka, mambo
yanayoendelea kuhatarisha sayari yetu, kaulimbiu hii bado ina mashiko.
Lengo la 13 la
malengo ya maendeleo endeleavu ya dunia mabadiliko ya hali ya hewa, yanaongeza
kasi na matukio ya hali ya hewa kali, kama vile mawimbi ya joto, ukame,
mafuriko na vimbunga vya tropiki.
Matatizo
makubwa ya usimamizi wa maji, kupunguza uzalishaji wa mazao ya kilimo na
usalama wa chakula, kuongeza hatari za afya, kuharibu miundombinu muhimu na
kukatiza utoaji wa huduma za msingi.
Kuanzia 1880
hadi 2012, wastani wa joto duniani uliongezeka kwa 0.85 senti gredi, na kuwa
eneo la dunia kuendelea kuwa na ukame karibu muongo mzima.
Bahari
zimepata joto, kiasi cha theluji na barafu kimepungua na usawa wa bahari
umeongezeka.
Kuanzia 1901
hadi 2010, kiwango cha wastani cha bahari kiliongezeka kwa sentimita 19, kadiri
bahari zinavyoongezeka.
Kiwango cha
barafu katika bahari ya aktiki, kimepungua katika kila muongo mfululizo tangu
1979, huku uzalishaji wa hewa ukaa duniani (CO2) umeongezeka kwa karibu
asilimia 50 tangu 1990.
Uzalishaji wa
hewa ukaa haraka zaidi kati ya mwaka 2000 na mwaka 2010, kuliko katika kila miongo mitatu
iliyopita.
WADAU WA MAZINGIRA WANASEMAJE
Mohamed Khatib
Khamis wa Wamba, anaemiliki mizinga ya nyuki 50, anasema uzalishaji umepungua
kufuatia uharibifu na uchafuzi wa mazingira.
‘’Wanaoendesha
kilimo cha mihogo na kilimo cha juu cha mpunga, unaotokana na uvunji misitu,
umeathiri mfumo wa nyuki wa kupata chakula, na uzalishaji asali,’’anasema.
Mwenyekiti wa jumuiya
ya uhifadhi wa mazingira Chake chake Halima Omar Mohamed, anasema kazi ya
kuhifadhi mazingira wanayoifanya, imekuwa ikishambuliwa na jamii.
‘’Tukiwa
kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, kila ifikapo Juni 5 ya kila
mwaka, bado jamii haijaona umuhimu wa kusaidia harakati za uhifadhi
mazingira,’’anasema.
Othman Haji
Kheir wa kijiji cha Tundaua, wilaya ya Chake chake, anasema hata uoto wa asili
kama mikoko (mikandaa) imekuwa nayo ikishambuliwa na jamii, kwa matumizi
binafsi.
Sheha wa
shehia ya Ndagoni wilaya ya Chake chake Massoud Juma, anasema elimu imekuwa
ikitolewa na uhifadhi wa mazingira, changmoto ni kubadili tabia.
‘’Kasi ya
kuotesha miti kwa jamii hata iwe kwa siku za kitaifa bado iko chini, hali
inayopelekea dunia kuizidi katika uotaji miti na hatimae msitu,’’anasema.
Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services Agency)
‘TFS’ ulianzishwa kisheria kupitia tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la Julai
7, mwaka 2010 na kuzinduliwa rasmi mwaka mmoja baadae.
Kuanzishwa kwa
wakala wa Huduma za Misitu ni kwa mujibu wa Sheria ya Wakala pamoja na Sera ya
Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria za Misitu na
Nyuki Sura 323 na Sura 224 za mwaka 2002.
Lengo la 11, la
kuanzishwa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni uwepo wa usimamizi madhubuti
na wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki.
Lakini hata kuongeza
ubora na thamani ya kifedha katika kutoa huduma kwa umma, kuendelea kukuza na
kuboresha uwezo wa kutoa huduma kwa umma.
Wakala
umepanua wigo kibiashara na kuongeza maeneo ya uzalishaji miti na mazao ya
nyuki ili kukidhi mahitaji halisi, shughuli za uwekezaji, kuboresha njia
mbadala za mapato na uboreshaji wa hifadhi za misitu na nyuki kwa ujumla.
SMZ
Waziri katika
afisi ya Makamu wa Kwanza wa rais Harusi Said Suleiaman, anasema ni wajibu wa
kila mmoja kuyatunza na kuyahifadhi mazingira.
‘’Kuhifadhi
mazingira na kuacha kuyachafua halihitaji sindikizo la kisheria, iwe ni wajibu
wa kiutu kwa kila mmoja, maana faida na athari zake zinamgusa kila
mmoja,’’anasema.
Kwa mwaka huu,
Makamu wa Kwanza wa rais Zanzibar Othman Massoud Othman, ndie anayetarajiwa
kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira.
Mwisho
Comments
Post a Comment