Skip to main content

DKT. MWINYI ATEKELEZA AHADI YAKE YA KUONGEZA MSHAHARA WATUMISHI WA UMMA

 



NA MOZA SHAABAN, PEMBA @@@@

SERIKALI ya awamu ya nane inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi imetekeleza ahadi yake ya kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma kuanzia mwenzi wa Oktoba mwaka kutoka shilling laki tatu kwa kima cha chini cha mshahara hadi shillingi laki tano.

Ongezeko hilo ni utekelezaji wa ahadi yake alioitoa katika hutuba yake kwa wafanyakazi wa sekta za umma alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, yaliofanyika Kizimbani Mkoa wa Mji Magharibi Unguja.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuthibitisha utekelezaji wa ahadi hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Dkt Haroun Ali Suleiman alisema, ongezeko la mishahara limezingatia zaidi watumishi wote na pamoja na wanaofanya kazi katika mazingira magumu.

"Tupo hapa kuthibitisha kua ahadi ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuongeza maslahi ya mishahara kwa watumishi wa umma kuanzia mwenzi huu itathibitika kwa vitendo kama alivyoahidi katika hutuba yake ya siku ya wafanyakazi Mei 1 mwaka huu, kwamba kima cha chini cha mishahara kitakua shilling laki tano, hili linaenda kutimia kwa vitendo ", alieleza.

Alieleza, sekta ya elimu imeangaliwa zaidi kwa kutolewa posho kwa waalimu wanaosomesha katika mazingira magumu hususan waliopo katika maeneo tengefu ya visiwani, waalimu wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, pamoja na maofisa elimu.

Dkt. Haroun alifahamisha kuwa katika sekta ya afya, pia Serikali imeiangalia kwa kuongeza posho kwa wauguzi pamoja na maasifa afya wa wilaya (DMOs).

Alieleza kuwa, mbali na sekta ya afya na elimu watumishi wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na viongozi wakuu wa nchi wamezingatiwa katika suala hilo.

Alisema, marekebisho hayo ya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wa umma ni ya tatu sasa kufanyika, huku lengo likiwa ni kuongeza hamasa kwa wafanyakazi ya kujituma zaidi katika kuihudumia jamii.

Aidha, aliwasisitiza watumishi kuendelea kufanyakazi kwa bidii na kujituma ili kuzithamini juhudi zinazofanywa na Serikali siku hadi siku.

"Kila mtumishi atafaidika na maboresho haya ya viwango vya mishahara, na maboresho hayo yamezingatia elimu, uzoefu na namna mtumishi anavyofanya kazi," alifahamisha.



Waziri Haroun alitoa wito kwa wafanyabiashara kutotumia fursa hiyo kama ni sababu ya kuongeza bei za bidhaa na badala yake wafanye biashara kwaimani na kuzingatia taratibu za bei za bidhaa husika.

Katika hatua nyengine Waziri Haroun alikabidhi usafiri wa bajaji kwa jumuiya nne za wasaidizi wa sheria kutoka wilaya nne za Pemba, ili kusaidia kurahisisha safari zao katika utekelezaji kazi zao, kutokana na jumuiya hizo kuonekana  kufanya kazi kwa ufanisi katika kuisaidia jamii.

Aidha, aliwasihi wasaidizi wa Sheria kuvitunza vyombo hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu kwa maslahi ya jamii zinazo wazunguka.

Katika makabidhiano hayo alitoa wito kwa wananchi kuzitumia jumuiya za wasaidizi wa Sheria katika kutatua changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakwaza, hali itakayosaidia upatikanaji wa haki katika jamii.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa bajaji hizo kwa niaba ya jumuiya hizo Msaidizi wa Sheria Mohamed Hassan aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP na Serikali ya Island kwa kuwapatia usafiri huo utakaorahisisha utendaji kazi wao katika utoaji wa huduma za kisheria kwa kufanikisha malengo ya Serikali ya kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

Jumla ya bajaji nne zinazotumia umeme zimetolewa kwa jumuiya nne za wasaidizi wa Sheria kisiwani Pemba, ikiwemo ya Chake chake, Mkoani, Micheweni na Wete Pemba.

                         MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...