Skip to main content

HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU ZAZIDI KUPIGIWA CHAPUO

                                   



NA ZUHURA JUMA, PEMBA


USHIRIKIANO unahitajika zaidi katika kuhakikisha kunakuwa na ukondoishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu, ili wapate haki zao za msingi.

Akiwasilisha mada katika mkutano wa Mtandao wa Wilaya wa Mpango Jumuishi wa Maendeleo katika Jamii (CBID), Mshauri kutoka Shirika la watu wenye ulemavu la Norwey (NAD) Christine Cornick alisema, wamekuwa wakifanya kazi na mtandao huo, ili kuisaidia kuleta mabadiliko katika jamii.

Alisema kuwa, ushirikiano wa pamoja ndio utakaoleta nguvu ya kufanya kazi na kuleta mabadiliko ya haraka katika ukondoishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika nchi mbali mbali.

"Katika mtandao huu tumeshirikisha watu mbali mbali, wanakuwa na sehemu ama mahala ambapo wanakutana na kubadilishana uzoefu katika ngazi mbali mbali na kutoa maamuzi ya kujenga jamii iliyobora", alisema Mshauri huyo.

Alifahamisha kuwa, watu wenye ulemavu wamekuwa wakikosa huduma zao za msingi, jambo ambalo linasababisha kudharaulika na kudhalilika, hivyo mtandao huo wanaamini utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto zilizopo.

Mapema Mkurugenzi wa Baraza la watu wenye ulemavu Zanzibar Ussi Khamis Debe alisema kuwa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ipo pamoja na watu wenye ulemavu kutumia mtandao huo katika kuhakikisha wanafikisha changamoto zinazowakabili sehemu husika, ili ziweze kupatiwa ufumbuzi unaofaa.

"Tunaamini kwamba lengo la taasisi ya malezi na makuzi Bora ya watoto (MECP-Z) ina lengo la kutusaidia na kupata haki zetu sawa na watu wengine, hivyo tushirikiane kwa pamoja ili kufanikisha", alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi huo Saida Amour alieleza kuwa, watu wenye ulemavu wanakosa usaidizi katika sehemu za kutoa huduma, wanalipishwa nauli mara tatu wakati wanapokwenda safari na pia kuna ushirikishwaji mdogo katika masuala ya michezo.

"Hizi ni changamoto kubwa zinazowakabili watu wenye ulemavu ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi na kuondoshwa kabisa ili wajisikie huru ndani ya jamii", alieleza Mratibu huyo.



Nae muwasilishaji kutoka SHIJUWAZA Ali Khamis Machano alisema kuwa, watu wenye ulemavu wamekosa elimu ya watu wazima pamoja na ya utunzaji wa fedha, jambo ambalo linasababisha kutoendeleza biashara zao wanazonzisha kwa lengo la kujikwamua kimaisha .

"Watu wenye ulemavu unakuta mara nyingi miradi yao inakwama na hawaendelei mbele, jambo hili linawakwaza sana, hivyo kuna haja ya kupewa elimu ya utunzaji wa fedha", alifafanua.

Washiriki wa Mkutano huo walisema kuwa, mtandao huo ni mzuri sana, kwani unaunganisha wadau mbali mbali, jambo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa katika kipendekeza na kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.

Mkutano huo umeandaliwa na MECP-Z kupitia mradi wa Mpango Jumuishi wa Maendeleo katika Jamii (CBID) kwa ufadhili NAD ambao umefanyika katika Ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake.


                      MWISHO.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...