Skip to main content

FANI YA UTANGAAZAJI NA FURSA MPYA KWA WANAWAKE PEMBA


NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

‘’MTANGAAZAJI aliyekuwa akinivutia ni Fatma Said Ali, Sauti ya Tanzania Zanzibar ‘STZ,’’anasema mtangaazaji Khadija Kombo Khamis wa ‘ZBC’ Pemba.

 

Alikuwa akimpenda mtangaazaji huyo kuanzia sauti yake, mawimbi ya utangaazaji, mpangilio wa maneno yake na anavyomalizia.

 

Khadija Kombo Khamis ambae kwa sasa ni mtangaazaji wa Shirika la Utangaazaji Zanzibar ‘ZBC’, kumbe alianza kuipenda fani hiyo tokea akiwa skuli.

 

Hakuacha wakati mwingine hata akiwa na wadogo zake, kujifanya mtangaazaji, huku akimfuatilia Fatma Said wa ‘STZ’ wakati huo na sasa ‘ZBC’.

 

Baada ya kumaliza masomo, sasa mwendo ikawa ni kufika wizara ya Habari Pemba, na kuanza harakati na ilipofika mwaka 1991 hadi mwaka 1992, aliajiriwa eneo la ndoto yake.

 

Hapo ikawa sio Khadija Kombo pekee, walionufaika na ajira ya ‘STZ’ tena sehemu ya uandishi wa habari, bali na mapacha wenzake Jitihada Abdalla Salum na Mchanga Haroub Shehe.

 

Baada ya ajira, safari ya kwenda kupata mafunzo ya watatu hao, ikawadia hadi Unguja, wakawa mikononi mwa nguli wa utangaazaji Hassan Vuai na Nassra Mohamed Juma.

 

Mchanga anasema, walipofika huko walitawaliwa na woga, wasiwasi, kupasukwa na moyo na walifikiria kuwa, wala hawatoweza kutangaaza.

 

‘’Unajua Hassan Vuai, wakati wa kazi utani huweka pembeni na hata Nassra Mohamed Juma, alikuwa sawa na bossi wetu,’’anasimulia.

 

Mchanga Haroub anasema hapo walidumu kwa miezi tisa, ndio wakaondoka pikioni na kurudi Pemba, kwa kazi ya ya utangaazaji.

 

Pacha wa wanawake hao, ambao ni kundi la pili kwa utangaazaji kisiwani Pemba, Jitihada Abdalla Salum, anasema walitua kisiwani humo, kwa hamu kubwa.

 

Kazi ya wanawake hao watatu, ukiachia mtangaazaji wa mwanzo kisiwani Pemba Najma Khalifan, aliyedumu kwa miaka 15, sasa wao ikiwa ndio wanaokibeba kisiwa cha Pemba, kiutangaazaji.

 

‘’Unajua kazi ya utangaazaji, ilionekana ngumu na hata ukiiambia familia unataka kuingia eneo hilo, kama hawakufahamu,’’ anasema Khadija Kombo.

 

Jitihada anasema, baada ya kuwasili Pemba, sasa wakawa ndio wanawake pekee, wanaoyapeperusha matangaazo na vipindi vyote, kutoka Pemba.

 

‘’Unakumbuka miaka hiyo, redio pekee iliyokuwa ikinguruma ni sauti ya Tanzania Zanzibar ‘STZ’ hivyo, ilikuwa rahisi kuenea kwa jamii, majina yetu,’’wanasema.

 

Ingawa wanasema kwa wakati huo, walilazimika vipindi vyao, kuvisafirisha aidha kwa meli au ndege, kwenda kuhaririwa na Hassan Vuai na kurudishwa tena Pemba, ili visikike redioni.

 

Khadija anasema, baada ya vipindi hivyo kuvitengeneza, na kisha kurudi Unguja, ndio vimeshapata ruhusa ya kusikika hewani.

 

Wanasema, kazi hiyo ilidumu kwa miaka zaidi ya 10, hadi kuanzia mwaka 2013 sasa walipopewa dakika 30 za mubashara ‘live’.

 

‘’Mimi nilikuwa na kipindi cha ‘ukumbi wa wanawake’, ambapo nilikuwa nahoji wanawake, juu ya shughuli zao mbalimbali za maisha,’’anasema Khadija.

 

Ambapo Mchanga Haroub kwa wakati huo, alikuwa akiongoza kipindi cha ‘matukio ya wiki’, na Jit-hada kipindi cha ‘watoto’.

 

Baada ya kuonekena wanawake hao, wameshaimudu redio kwa upande wa Pemba, waliongezewa muda hadi saa moja, kwa siku zote za kazi.

 

YEPI WANAONA NI MAFANIKIO

Khadija anasema, kwanza kuvunja mwiko wa jamii, ambapo walidhani wanawake hawawezi kutangaaza.

 

Ndio maana anasema, kuanzia hapo, waliwapokea akina Shikha Rashid Seif, Zuwena Shaaban Maalim wote wakihudumu redio ya serikali.

 

Wanawake hao nguli ya utangaazaji, wanasema hata uanzishwaji wa vituo vya redio jamii Micheweni miaka 16 iliyopita na redio jamii Mkoani miaka 11 sasa, mchango wao uko.



 

Haya nathibitishwa na mtangaazaji wa mwanzo wa kike kwa redio Jamii Micheweni Time Khamis Mwinyi, akisema anajivunia watangaazaji hao, kama sehemu ya waalimu wake.

 

‘’Walikuja akina Mchanga na Khadija kwa nyakati tofauti, kutufundisha mbinu za utangaazaji bora, sasa tumeshajiweza,’’ anasema.

 

Amina Massoud Jabir wa Redio Jamii Mkoani, ambae amaeshanyakua tuzo zaidi nne za utengenezaji vipindi bora, anasema mchango wa watangaazaji hao, anaukumbuka.

 

‘’Mimi ni tunda la akina Mchanga Haroub, Khadija Kombo na Jit-hada Abdalla kwa njia moja ama nyingine, sasa nimeshaitawala studio,’’anasema.

 

Kwa ufunguzi huo wa milango, sasa Pemba, inaowatangaazaji wa kike 25, kutoka mmoja ambae ni marehemu Najma Khalfan, kwa miaka zaidi ya 35 iliyopita.

 

Na Shirika la Utangaazaji Zanzibar ‘ZBC’ pekee kwa Pemba, ambalo linao watangaazaji, waandishi na wapiga picha wanawake wanane, ikifuatiwa na redio jamii Micheweni iliyoongeza wanne, kutoka mmoja wakati inaanzishwa 2010.

 



Huku redio jamii ya Mkoani, nayo ikivamiwa na watangaazaji watano, lakini cha kufurahisha, wakioongozwa na wanawake mahiri watatu, akiwemo Khadija Ali Yussuf.

 

Kituo cha Azam tv, nacho kikiwakilishwa na mwanammke mmoja, huku nafasi ya mitandao ya kijamii nayo ipo inayoongozwa na wanawake, kama vile pemba ya leo blog.

 

CHANGAMOTO ZA WATANGAAZAJI KWA SASA

Time Khamis Mwinyi wa redio jamii Micheweni, anasema ni kukosa mafunzo ya kina ya kidigitali.

 

‘’Miaka hii sio kama ile walioanza waalimu wetu akina Khadija na Mchanga, ya kukata waya au kuingiza kanda, sasa ni ‘digitali’, ndio inayoongoza,’’anasema.

 

Khadija Kombo, anasema anaona, fani kama imevamiwa kupindukia, na baadhi yao wakishindwa kuheshimu, maadili na sheria za utangaazaji.

 

‘’Nahisi kama porojo jingi watangaazaji wa sasa, na wakati mwingine hata kupoteza ladha ya kipindi husika, maana zamani tukiingia na mpango ulioandikwa ‘script,’’ anaeleza.

 

Mchanga Haroub Shehe anasema, sasa watangaazaji wa karne hii, wamekuwa na maneno mingi, wanapokuwa studio, mapaka wanarejerejea.


 


‘’Enzi zetu akina Suleiman Juma Kimea hao, Makame Abdalla, Hassan Vuai na Nassra Mohamed Juma, wanakusikiliza na karatasi mkononi, wanaorodhesha makosa yako, ukimaliza wanakutafuta,’’anafafanua.

 

Fatma Hamad Faki, aliyewahi kuhudumu na redio Adhana na Swahib Fm, kwa nyakati tofauti, anasema utangaazaji sasa umekuwa rahisi kuufanya, kwa kuwepo kwa mapinduzi ya teknologia.

 

MAMENEJA WA REDIO/WAKURUGENZI

Meneja mstaafu wa Redio Jamii Micheweni Hamad Shapandu Mwinyi, anakiri kuwa, wakati wanaanzisha redio hiyo mwaka 2010, walioibeba ni watangaazaji wanawake.

 

Meneja wa Radio Jamii Mkoani Said Omar Said, anasema anaowatangaazaji watano, ingawa wanawake watatu, ndio wanaoongoza kwa kupata tuzo.

 

‘’Karibu asilimia 90 ya vipindi na matukio ya moja kwa moja ‘live’ yanaendeshwa na watangaazaji wakike hapa kituoni,’’anakiri.

 

Mkuu wa vipindi Shirika la Utangaazaji Zanzibar ‘ZCB’ Pemba Juma Mussa Juma, anasema hakuna matangazo au kipindi kinchoruka, kikakosa mwanamke.

 

‘’Sasa ndani ya ‘ZBC’ watangaazaji na waandishi wanawake, wamekuwa tegemeo, na hata kwenye ufundi wa kisasa wamejanjaruka,’’anakiri.

 

WASIKILIZAJI

Aisha Muhdin Jabu wa Micheweni, anasema hupata ladha nzuri, wakati wa kuendesha vipindi, kama kitaongozwa na mtangaazaji Time Khamis Mwinyi.

 



Khatib Khamis Khatib wa Machomane, anasema, wanapofuatilia mikutano ya moja kwa moja, ‘live’ huvutiwa na pozi na madaha ya mtangaazji Khadija Kombo.

 

Mayasa Haji Mcha wa Mkanyageni, anasema aliwahi kuhojiwa miaka saba iliyopita, na mtangaazaji Khadija Ali Yussuf wa Mkoani FM, na hadi sasa kumbukumbu ya sauti nyororo ameitunza.

 

Fatma Haji Said (55) wa Wawi anasema anazikumbuka vyema sauti muruwa za  watangaazji Mchanga Haroub, Jiti-hada Abdallaah na Khadija Kombo, wakati huo.

 

‘’Utasikia tu…mmpenziii msikilizaji, kama bado uko nasi muda huu, hii ni STZ na kipindi hewani…ni ukumbi wa wanawake AU ukumbi wa watoto na sikukuu,’’anakumbuka.

 

‘TUZ’ INAFANYA NINI KWA WATANGAAZAJI

Adam Ramadhan Kombo, ni Mratibu wa Tume ya Utangaazaji ofisi wa Pemba, anasema wamekuwa wakiwawezesha kwa mafunzo watangaazaji wote.

 

Anasema, hata wanapotaka kuandaa kanuni au mabadiliko ya sheria, huwashirikisha kikamilifu, kwani wao ndio wadau wakuu.

 

Anasema sasa fani hiyo, imekuwa kimbilio la watangaazaji wanawake, baada ya kuimarisha miundombinu, ikiwemo sheria zinazowalinda.

 

‘Katika eneo ambalo sasa wanawake kisiwani Pemba, wanaliingia, ili kuekeza ni utangaazaji, maana zamani alikuwepo mmoja tu, lakini idadi imeongezeka,’’anasema.

 

WATANGAAZAJI WANALINDWA VIPI NA SHERIA YA TUME?

Kuanzia mwaka 1997, serikali kwa kuwajali watangaazaji wa Zanzibar, ilianzisha Sheria ya mwaka huo, nambari 7.

 

Ambapo pamoja na mambao mingine, ilitaka kuondoka fani ya utangaaji kuvamiwa, kuchafuliwa na kuingiliwa na hata kuwalinda watangaazaji.

 

Maana sheria hiyo, ambayo imeshawahi kufanyiwa marekebisho, sehemu yake ya pili na hasa kifungu cha 5, kimekuja kuhalalisha uanzishwaji wa Tume.

 

Ambapo kifungu cha 6, kikafafanua muundo wa Tume hiyo, ambapo kifungu cha 6 (1) (a) kikatangaza kuwepo kwa Mwenyekiti atakayeteuliwa na Rais.

 

Kifungu (b), pia Rais huyo atamteua Katib Mtendaji, ambae atakuwa ni Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo, ambapo yote ni kwa maslahi ya watangaazaji.

 

Kifungu kizuri ndani ya sheria hiyo, ni cha 11 kinachopiga ‘marufuku kwa yeyote kurusha au kupokea kurusha au kwa namna yoyote kuendesha, huduma za utangaazaji, kufanyabiashara na vifaa vya utangaazaji, au kurusha jambo lolote linahitaji lieseni chini ya sheria hii, isipokuwa awe na leseni inayotambulika’’ kinafafanua.

 

 Sheria hiyo kwenye kifungu chake cha 13 (1), kwa maslahi ya shughuli ya utangaazaji Zanzibar, kinafafanua kuwa, ‘endapo Tume imeridhika kwamba muombaji leseni husika anakidhi matakwa ya sheria, ikiwa mmiliki wa leseni, itatoa leseni kwa mujibu wa utaratibu na kuzingatia malipo ya ada’.

 

Ingawa kufungu chingine kitamu kwa watangaazaji ni kile cha 17 (6), ambapo kinamlazimisha mpewa leseni, baada ya kupewa taarifa ya kukanusha, kuiarifu Tume, juu ya ukweli na ataweka na kuhifadhi kipindi  kinacholalamikiwa….kinaendelea kifungu hicho.

 

USHAURI WA WAATANGAAZAJI WANAWAKE KWA TUZ.

Wanaiomba Tume ya Utangaazaji, kuendelea kukutana nao, ili kuhakikish fani ya utangaazji haivamiwi na inalindwa.

 

Khadija Kombo Khamis wa ‘ZBC’ Pemba, anasema Tume, imekuwa ikikutana nao kila shida inapotekezea, ingawa ni vyema wajibu huo, ukaongezewa.

 

Amina Massoud Jabir wa redio jamii Mkoani, anasema, wakati umefika sasa kwa Tume ya Utangaazaji, kuanzisha tuzo maalum, kwa watangaazaji wanawake.

 

Fatma Hamad Faki, ambae anamiliki blog, anasema ada ya mwaka ya shilingi 500,000 ni kubwa, ni vyema ikawekwa shilingi 100,000 kama ilivyo, kwa Baraza la Habari Tanzania MCT.

              Mwisho  

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...