Skip to main content

MCHEZO WA NG’OMBE PEMBA, UTAMADUNI UNAOBEBA WASHABIKI WINGI

 

               

           

 
NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@ 

KELELE za watazamaji, mlio ya zumari, ukichombozwa na ngoma za asili, ndizo zinazoteka nyonyo za wapenzi wingi wa mchezo wa Ng’ombe, baada ya mpira wa miguu.

 

Mchezo huu ambao umejengeka katika historia ya  maisha ya jamii ya Pemba, si burudani pekee, bali ni sehemu ya urithi wa kitamaduni unaounganisha vizazi vya zamani sasa.

 

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kuhusu historia ya mchezo huo, asili yake Pemba imehusishwa na mwingiliano wa kihistoria, kati ya jamii za Pemba na Wareno.

 

 Baadhi ya vyanzo vinaeleza kuwa, mchezo huo uliingia katika visiwa hivyo kupitia Wareno, ingawa simulizi za wenyeji pia, zimekuwa zikihifadhi historia yake, kutoka kizazi hadi kizazi.

 

Akizungumza, katika mchezo wa Ng’ombe uliofanyika uwanja cha Pujini wilaya ya Mkoani, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Riziki Pembe Juma, anasema mchezo huo, ni miongoni mwa mchezo wa kiutamaduni wa mzanzibari.

 

Ndio maana, aliwataka wananchi wa Pujini Dodo kuhakikisha wanauendeleza kwa hali na mali, ili uwe urithi kizazi hadi kizazi, kwani wizara itakuwa nao bega kwa bega, katika kuenzi mchezo huo.

 

Nae Seif Salim Mussa ambae ni Mratibu Baraza la Sanaa Pemba, anaeleza kuwa mchezo wa Ng’ombe  ni maarufu kisiwani Pemba, na hasa katika kijiji cha Pujini, ambao hadi sasa unaendelezwa na wazawa.

 

Hivyo aliwataka wachezaji na wazawa wa kijiji hicho, kuendeleza mchezo huo kwa kufanya mazoezi mara kwa mara, ili uweze kuwapatia maendeleo makubwa zaidi, ikiwemo kuwarithisha watoto wao

 

Mchezo wa Ng’ombe umekuwa ukihusishwa zaidi na maeneo mbalimbali ya Pemba, yakiwemo Pujini na Mchangamdogo, katika nyakati za zamani, ulihusishwa kwa kiasi kikubwa, na kipindi cha baada ya mavuno.

 

Ambapo kwa wakati huo, wananchi walipata nafasi ya kusherehekea na kupumzika baada ya shughuli za kilimo, au msimu kumalizika.

 

Miongo mingi iliopita mchezo huo, ulikuwa na unachezwa na wazee wa rika la kati, ambapo ulikuwa na vishawishi vingi vinavyomfanya mchezaji kuingia katika uwanja na kumcheza Ng’ombe.

 

Inaelezwa kuwa, wachezaji wa asili wa mchezo huo, hamu yao ilikuwa ni kumchezo Ng’ombe siku inapofika, na suala la hofu ya kuumia kwao, haikuwa ikiwapitikia.

 
Katika karne ya 21, ambapo kila kizazi kinataka kujifunza ama kujionesha, mchezo huo unachezwa na kuendelezwa na vijana katika kisiwa cha Pemba, na huwa ni kivutio kikubwa pale unapofanyika.

 

Maeneo ya Pujini kwa wilaya ya Mkoani na Chwale  Madenjani kwa wilaya ya Wete, hayo ni miongoni mwa maeneo yaliojikita, kuendeleza kwa kucheza mchezo huo.

 

Ingawaje huwa wanacheza kwa vipindi maalum hususan wakati wa sherehe maalum za kiserikali, au matamasha n ahata kilele cha Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Katika  uwanja wa mchezo wa Ng’ombe hauwi tu kuwa sehemu ya mashindano pekee, bali huwa ni  mahali pa kukutana, kubadilishana habari, kusherehekea na kuendeleza mshikamano wa kijamii.

 

MAZINGIRA YA UWANJA WA MICHEZO WENYEWE

Mchezo wa Ng’ombe, hufanyika katika uwanja mkubwa unaotayarishwa kwa ajili ya wachezaji na watazamaji, ambapo hawaingiliani ama kukerana.

 

Kwenye uwanja wa mchezo wa Ng’omb, hujengwa majukwaa kwa miti minene, yanayojulikana kama madungu, ambako watazamaji hukaa, tena huwa pembezoni mwa uwanja.

 

Ingawa kwenye eneo hilo, huwepo kibanda kinachojuilikana kwa jina la ‘bigili’ eneo ambalo linalohusishwa na wapiga zumari, wanaoambatana na mchezo huo.

 

Ndani ya ‘bigili’ huwekwa Ng’ombe ambae anakuwa kwenye matayarisho ya kuchezwa, na huwa ametiwa kamba ndefu, kwenye shingoni inayojuilikana kwa jina la ‘Ngoweyo’ ambayo hutumika kwa ajili ya kuchezesha Ng’ombe wenyewe.


 

Mmoja wa wachezaji mashuhuri wa mchezo huo Omar Abdalla Khamis, anasema hukabiliana na Ng’ombe kwa kutumia ujuzi na wepesi wa mwili, huku akiwa amedhibitiwa kwa namna inayolenga kupunguza hatari kwa washiriki na watazamaji.

 

Tofauti na mapambano ya Ng’ombe, yanayojulikana katika baadhi ya nchi, katika mchezo wa Pemba Ng’ombe si lazima auawe, baada ya mchezo, lakini huwa ni aina maalumu na aliefunzwa kwa ajili ya mchezo.

 

Anasema hakuna nguo maalumu zinazotumika kwa ajili ya kuchezea mchezo huo, ingawa ikiwa nyeupe zinatajwa kuwa sehemu ya utamaduni wa mchezo huo.

 


Hili ni kwa sababu, humsaidia mchezaji kuonekana vizuri na Ng’ombe wakati wa mchezo, na kumvutia kutaka kumpiga mwilini mwake.

 

SAUTI ZA MUZIKI NA SHANGWE

Mchezo wa Ng’ombe, hauwezi kutenganishwa na muziki, unaoambatana nae kwani mlio wa zumari na ngoma za asili, huongeza hamasa na kuifanya shughuli hiyo kunoga.

 

Kwenye mchezo huo, huwepo wa nyimbo maalumu zinazoimbwa na kwa kawaida, huwepo waimbaji na waitikiaji ambao huongozwa na mlio wa zumari.

 

Mmoja wa wachezaji wa mchezo wa Ng’ombe Omar Haji Machano, anasema watazamaji huwa ni sehemu ya mchezo, kupitia shangwe nderemo na vifijo, vilivyotanda kila kona ya eneo la mchezo huo, hali inayoongeza mvuto wake kwa jamii, na wageni waliopo.

 

“Kwa maana hii, mchezo wa Ng’ombe unaweza kutazamwa kama muunganiko wa mchezo, muziki, burudani na nyimbo za utamaduni wa mzanzibari,’’anasema.

 

  URITHI UNAOPITIA CHANGAMOTO

 Pamoja na kuendelea kuwepo mchezo huo, unakabiliwa na changamoto zinazoweza kuathiri uendelevu wake hapo baadae.

 

Baadhi ya wachezaji akiwemo Abdalla Suleiman Seif, anaeleza kuwa, mchezo umeanza kuonekana zaidi katika matamasha maalumu ya kiutamaduni wa mzanzibari, badala ya kuchezwa mara kwa mara kama ilivyokuwa zamani.

 


Anafahamisha kuwa hiyo ni changamoto zinazohusiana na zawadi, usalama na msaada kwa washiriki, wanaopata majeraha.

 

Anasema changamoto nyingine ni kuhakikisha kuwa kizazi kipya, kinaendelea kujifunza historia na taratibu za mchezo huo, hivyo bila kurithishwa kwa vijana, kuna hatari ya baadhi ya maarifa yanayohusiana na mchezo, kupotea.

 

UTAMADUNI NA UTALII KUPITIA MCHEZO WA NG’OMBE

Pemba inajulikana kwa utajiri wake wa historia, mazingira na mila, katika mazingira hayo, mchezo wa Ng’ombe unaweza kuwa sehemu ya vivutio vya kitamaduni kwa wageni.

 

Taarifa za hivi karibuni, zimeonyesha kuwa si wenyeji pekee wanaovutiwa na mchezo huo, hata wageni wamekuwa wakifika kuutazama kwa hamasa na ari.

 

Ndio maana, Kaimu Afisa Mdhamini wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Pemba Sharifa Hamad Shapandu, anasema mchezo huo usibakie tu, kuwa maonyesho kwa wageni pekee, bali uendelee kuwa sehemu hai ya jamii.

 


WITO WA KUUHIFADHI

Wadau wa mchezo huo wamekuwa wakitaka kuwepo kwa mazingira bora ya kuuendeleza, ikiwemo maeneo maalumu ya michezo, usalama wa wachezaji, mafunzo kwa vijana wanaotamani kucheza.

 

Hatua nyingine muhimu ni kuandika na kurekodi historia ya mchezo huo, kutoka kwa wazee na wachezaji waliobobea, kwani simulizi zao zinaweza kusaidia kizazi kijacho, kuelewa si tu namna kucheza, bali pia sababu zilizoufanya uwe sehemu ya maisha ya jamii.

 

Kwa maana hiyo, mchezo wa Ng’ombe ni zaidi ya tukio la burudani, na ni sehemu ya kumbukumbu, historia na utambulisho wa kitamaduni wa Pemba, katika dunia.

 

Wakasema kama historia ikiandikwa na kuhifadhiwa, maarifa yake hayawezi kupotea, kwa hiyo jukumu la kuuhifadhi Mchezo wa Ng’ombe ni la jamii, wachezaji, watafiti na taasisi za utamaduni.

 

Hata hivyo iwapo juhudi hizo zitaimarishwa, mchezo huo unaweza kuendelea kuwa sehemu muhimu ya urithi wa Pemba, na pia dirisha la dunia kuufahamu utamaduni wa waswahili wa visiwani.

 

                                           MWISHO

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...