Skip to main content

‘RESI’ ZA NGALAWA MANAHOZA WAMBAA, MAKOMBENI, MAKOONGWE WAZAA 'DABI'

 

 



NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

NGALAWA ni usafiri ambao wazee wa zamani, waliutumia kwa ajili ya safari zao, hasa kwa shughuli za kibiashara na uvuvi.

Usafiri huu ni urithi wa utamaduni wa mzanzibari, ulioanza kutumika katika miongo iliopita, ingawa hadi sasa hutumiwa, lakini sio sana kama ilivyokua hapo zamani.

Hili limepelekea kuchukuliwa kama moja ya urithi mkubwa wa kihistoria kwa waswahili wa Zanzibar na wale wa ukanda wa pwani.

Ndio maana, katika matamasha mbalimbali ya utamaduni wa Zanzibar, ngalawa zimekua sehemu muhimu ya matamasha hayo na kua kivutio kikubwa kwa hadhira.

Kwani hadhira kubwa ya watu ambao huenda katika matamasha hayo, hufurahia kuona jinsi watu wanavyoendeleza utamaduni huo, ambapo huko hufanyika mashindano ya resi za ngalawa.

Septemba 21, mwaka huu ilikuwa ni siku ya pili ya tamasha la 31 la utamaduni wa mzanzibari, tokea kufunguliwa kwake Septemba 19, ilikua ni siku ya kukumbuka urithi wa utamaduni wa kuendesha ngalawa.

Utamaduni ambao, unaoendana na safari za vyombo vya usafiri aina ya ngalawa, ambapo kwa mwaka huu, tukio hilo lililofanyika bandari ya Mkoani Pemba.

Ilikua ni majira ya saa 9 alaasiri, ambapo nderemo na vifijo vilisikika katika bandarini hapo, bila ya kujali miale ya jua, ilikuwa ikiwasakama kwenye pasi za uso.

Hapo hapakua na ugeni mkubwa uliokua ukisubiriwa na mafuriko ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Unguja na Pemba, kusini na kaskazini ila ni kushuhudia manahoza wenye weledi, wa kuendesha vyombo hivyo.

Furaha za wananchi hao, ilikuwa ni kuona namna gani waswahili wanaweza kuendeleza utamaduni wao wa kutumia vyombo hivyo, aina ya ngalawa.

Kwasababu uendeshaji ngalawa ni sehemu ya utamaduni wa mzanzibari, ndipo palipokua na mashindano ya Ngalawa, yaliokutanisha manahoza 15 kutoka maeneo mbali mbali ya wilaya ya Mkoani.



Resi hizo zilitoa hamasa kubwa kwa waliofika kuangalia mashindano hayo, kutokana na umahiri waliokua nao waendeshaji vyombo hivyo.

Kwenye tukio hili, viongozi mbalimbali walihudhuria, wananchi wa kawaida kike kwa kiume na wakubwa kwa wadogo, ili kuthibitisha mazungumzo ya historia ya utamaduni wa Zanzibar.

Ambapo katika juhudi za kuuenzi, wizara ya Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo iliandaa mashindano hayo yaliokua kivutio kikubwa, kwa kila aliefika.

Manahoza kadhaa walikua wakijinasibu jinsi watakavyo endesha na kushinda, huku wengine wakijibu hoja hizo kwa maneno.



Lakini kila muda ulipo sogea, na mchezo kupamba moto waswahili kutoka shehia ya Wambaa, waliibuka kua wamahiri zaidi, katika hili kwa kuchukua kwao ushindi mnono katika mashindano hayo.

Kwani kati ya washindi watano wa mwanzo wanne, kati yao walikuwa ni manahoza kutoka Wambaa, ambapo miongoni mwao ni Mohamed Haji Mohamed wa Wambaa aliechukua nafasi ya kwanza, alikuekuwa na ngalakwa ‘sila mmoja’.



Ingawaje wako wengi walioshiriki lakini nahodha huyo ndie alieibuka kidedea kwa siku hiyo, baada ya kuwaacha wenzake 14 masafa marefu.

Wakizungumza baada ya kuibuka washindi Mohammed na wenzake walisema, Ngalawa ni miongoni mwa vyombo vya usafiri vilivyo beba historia ya utamaduni wa wakaazi wa Zanzibar, na hasa kiuchumi na kijamii.

Walieleza katika kuhakikisha wanalinda utamaduni huo, wanaendelea kutumia ngalawa, katika shughuli zao za uvuvi wa kila siku, jambo lililowafanya kua mahiri zaidi.

“Katika kuhakikisha tunalinda utamaduni wetu huu,  tunaendelea kutumia ngalawa, katika shughuli zetu za uvuvi za kila siku, jambo linalochangia kua mahiri zaidi”, wanaeleza.



Hata hivyo waliipongeza wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, kwa kuandaa mashindano hayo, hali inayosaidia kueneza na kukuza utamaduni huo kwa vizazi.

Mmoja wa wananchi ambae ni miongoni mwa wanaoenzi utamaduni huo Khamis Bakar Massoud anaeleza, kiufundi kabisa, ili ngalawa iweze kutembea kwa kasi ni lazima iwe na mabawa mawili kulia na kushoto.

Anaeleza kuwe na mlingoti unao simama pamoja na mambo mengine ili kuifanya iweze kutembea.



Anasema ili kuhakikisha utamaduni huo unarithiwa hutumia vyombo hivyo katika shughuli zao za uvuvi, ambapo vijana mbalimbali, hujumuika nao na kujifunza.

Anasisitiza kua ngalawa nikitega uchumi kwa mwananchi wakipato cha chini, kulingana na mwelekeo wa bahari nyingi za Zanzibar.

“Ngalawa ni sehemu ya utamaduni kwetu, lakini pia nikitega uchumi kwa mwananchi wakipato cha chini, kulingana na mwelekeo wa kiuchumi na namna bahari zetu zilivyo”, anaeleza.

Anahadithia ngalawa ni tofauti na vyombo vyengine vya usafiri, kwani nahoza (dereva) wa ngalawa hukaa, nyuma badala ya mbele.



Hili humtofautisha nahoza wa ngalawa na manahoza wa vyombo vyengine, huku mwelekeo wa upepo ukiwa na nafasi kubwa ya muongozo wa safari ya ngalawa.

Mashindano ya resi za ngalawa yaliofanyika bandari ya Mkoani, ni miongoni mwa juhudi za kulinda utamaduni wa kizanzibari, ambao ni tunu na utambulisho wa mzanzibari duniani kote.

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, ambae alikuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Mkoan Khamis Mohamed Amran, anahadithia kua uendeshaji Ngalawa ni utamaduni wenye historia kubwa, katika sekta ya usafiri na usafirishaaji Zanzjbar.

Anasema kuna umuhimu wa kufanya tukio hilo la kiutamaduni kuwa bora zaidi, kwa kushirikisha wadau kutoka nchi mbalimbali, ili kuutangaza utamaduni wa Zanzibar ulimwenguni.

“Kuna umuhimu wa kufanya tukio hili la kiutamaduni kuwa bora zaidi, katika hili ni vyema kushirikisha wadau kutoka nchi nyengine za ukanda wa pwani, ili tutangaze utamaduni wetu ulimwenguni kote”, anashauri Amran.

Aidha katika juhudi za kutia hamasa za kuendeleza utamaduni huo, anasema mashindano hayo yakifanyika tena katika bandari ya Mkoani, kutakuwa na zawadi maalumu kutoka kwake,  ikiwa ni moja ya hatua ya kuungamkono juhudi za wizara.

Amran anaipongeza wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa kuandaa mashindano hayo, hali inayosaidia kueneza utamaduni huo, huku akiishauri kupeleka mashindano hayo katika bandari ya Mkoani kila mwaka.

"Utamaduni wetu wa zanzibar ni utambulisho ulimwenguni kote, hivyo ni wasihi vijana kuulinda na kuuthamini, ili Zanzibar ibaki katika uhalisia wake, hii ni maslahi ya vizazi vya sasa na baadae", anaeleza.

Wakati wa mashindano Kaimu Ofisa Mdhamini Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Pemba Sharifa Hamad Shapandu alisema, resi za ngalawa ni mwendelezo wa matukio mbalimbali ya kiutamaduni, katika tamasha la 31, lililofunguliwa rasmi tarehe Septemba 19, mwaka huu.

Sharifa anawapongeza manahoza wote walioshiriki katika resi hizo, kwa kuonyesha umahiri wao na juhudi zao katika kutunza utamaduni wa mzanzibari.

Mkuu wa divisheni ya utamaduni Pemba Hamad Ali Haji anasema, ni jambo jema kwamba wavuvi wengi wa Mkoani, hutumia vyombo vya asili vya uvuvi kama Ngalawa, majahazi na madau, na kufanya utamaduni wa kuendesha vyombo hivyo kuendelea kubaki hadi sasa.

Mashindano ya resi za ngalawa yaliyofanyika bandari ya Mkoani Pemba, yalihusisha ngalawa 15, yakiwa ni muendelezo wa tamasha la 31 la utamaduni wa mzanzibari, lililofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais, uwanja wa michezo Gombani.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ni  nahoza Mohammed Haji Mohamed, mshindi wa pili ni Ali Haji Mohamed na mshindi wa  tatu ni Juma Haji Shaame wote kutoa shehia ya Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba.

MWISHO.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...