NA MARYAM NASSOR, ZANZIBAR@@@@
MKUU wa mkoa wa mjini Magharibi
Unguja, Idrissa Kitwana Mustafa , amekitaka chuo kikuu cha taifa Zanzibar ( SUZA) kuendelea kuandaa mashindano ya waandishi chipukizi, ili kuwapima uwezo wao katika kada hiyo.
Ameyasema
hayo, katika hafla ya kuwatunuku vyeti na zawadi washindi wa shindano la
waandishi chipukizi, katika chuo cha SUZA
kampasi ya Kilimani.
Alisema ,
fani ya uwandishi wa habari ni kada nyeti sana, hivyo ni vyema wanafunzi
wakasoma na kufanya kazi kwa bidii, kwani kumeibuka wimbi kubwa la watu
wanaojiita waandishi bila ya kuwa na sifa ya uaandishi au bila ya kusomea.
“ Siku hizi
kumeibuka wimbi la waandishi makanjanja na wao wanajiita waandishi wa habari,
wakati hawajasomea hata cheti katika habari na kuichafua kada hii kwa kwenda
kinyume na maadili ya uwandishi,”alisema.
Aidha
alisema kuwa, kwa kupitia mashindano kama hayo, watapatikana wandishi wazuri na
wajuzi wa lugha, kwani ili uwe mwandishi mzuri basi , uwe na uwelewa wa lugha
nyingi ikiwemo kichina ambacho kinafundishwa katika chuo hicho.
Nae Mwenyekiti
wa kamati ya majaji, Saleh Yussuf
Mnemo alisema kuwa, kazi
zilizowasilishwa zilikuwa ni 40 na zote zilikuwa nzuri na zenye sifa, hivyo
walipata wakati mguu kumtafuta mshindi.
Alisema
kuwa, katika vipengele vilivyoshindaniwa vilikuwa ni vitatu, ambavyo ni uwandaaji
wa makala za televisheni na radio, makala za mtandaoni na utangazaji .
Akisoma risala ya chuo hicho, Dk. Khamis Juma
Abdallah ambae ni mkuu wa habari na mawasiliano chuo cha SUZA, alisema kuwa
lengo la kuandaa mashindano hayo, ni kujali mchango wa vijana hao na ililenga wale kuanzia miaka 18 hadi 35.
Nae, balozi
mdogo wa China , anaeishii Zanzibar Zheng Min alisema kuwa kuna ofa kubwa ya
masomo kwa wanafunzi wa Zanzibar, hivyo ni vyema wakasoma kwa bidii na
kujifunza lugha ya kachina, ili
wanufaike na fursa hiyo.
Mashindano hayo, yaliyodhaminiwa na baraza la
habari Tanzania kwa upande wa Zanzibar (MCT ZNZ), Klabu ya waandishi wa habari
(ZPC) na SUZA washindi katika mashindano hayo, walidhawadiwa vyeti na fedha
taslimu .
MWISHOO
Comments
Post a Comment