NA HAJI
NASSOR, PEMBA@@@@
WANANCHI wa
shehia za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wameikumbusha tena
wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, kulifanyia matengenezo ya haraka, eneo
la barabara yao lililokotika kwa mvua tokea mwaka 2017.
Walisema,
eneo hilo tayari kwa mvua za mwaka huu, limeshakatika tena na kuifinya
barabara kuu ya Mizingani-Wambaa, jambo ambalo linaweza kusababisha ajali zisizokuwa
za lazima.
Wakizungumza na
mwandishi wa habari hizi leo Mei 29, 2024, kufuatia muendesha baiskeli mmoja kutumbukia eneo hilo,
walisema ni muda sasa wamekuwa wakiahidiwa bila ya kutekelezewa ahadi hiyo.
Walisema kuwa,
eneo hilo sasa limekuuwa tishio zaidi, hasa baada ya kuongezeka kukatika, na huku
kukiwa na ongezeko la vyombo vinavyopita eneo hilo.
Mmoja kati ya
wananchi hao Fatma Abuu Fakih, alisema eneo hilo lilipo kwenye mpindo karibu na
kijiji cha Kidutani, sasa limekuwa tishio mara mbili, kwa barabara kuliwa
zaidi.
Alieleza kuwa,
eneo hilo hutumiwa na waendesha vyombo vya maringi mawili, gari kubwa na ndogo,
watembea kwa miguu na wanyama, hivyo huwepo hatari zaidi.
‘’Serikali
ije haraka itufanyie matengenezo japo ya dharura, kabla hapajatokezea athari za
maafa, maana panatisha kwa kuwepo kwa shimo nusu na robo ya barabara,’’alieleza.
Nae Maryam Iddi
Haji, alisema eneo hilo kwa sasa limekuwa hatari kwa wanafunzi wanapokwenda na
kurudi masomoni, kwani huwa vigumu kupisha na vyombo vya usafiri hasa vyenye
mwendo kasi.
‘’Unajua
waendesha boda boda wanatabia ya kwenda mwendo kasi, na hakuna anaepunguza
akifika ‘korosini’ penye eneo barabara ilipokatika katika kwa mvua,’’alieleza.
Kwa upande
muendesha boda boda Juma Haji Khamis, alisema eneo hilo juzi nusura atumbukie,
baada ya kumkwepa mtoto mweye ulemavu wa akili.
Afisa
Mdhamini wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Pemba Ibrahim Saleh Juma,
alisema eneo kama hilo, yapo mingi kisiwani humo na tayari wizara inaandaa mpango
maalum.
Alieleza kuwa,
wizara unaompango kabambe wa kuyarekebisha maeneo kama hayo, ili wananchi
wanaotembea kwa miguu na wale wenye vyombo vya usafiri, wapite bila ya usumbufu.
Mkuu
wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alisema anaelewa vyema kuwa zipo
barabara kadhaa ikiwemo ya Mizingani –Wambaa, Mtambile- Mwambe, Mtambile-
Kangani na Kenya –Chambani kuwa zimeshachakaa.
Alisema,
mpango wa serikali kuu ni kuzijenga upya kwa kiwango cha lami, kama ambayo
imekuwa ikiahidiwa na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi.
Barabara
hizo sita za Mzingani- Wambaa, Mtambile- Mwambe, Mtambile- Kangani, Kenya
–Chambani, Chanjamjawiri- Tundanua na Chanjaani – Pujini zilifunguliwa mwaka
2012 na aliyekuwa rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Mradi huo wa ujenzi wa barabara hizo, zilijengwa kwa msaada
wa Serikali ya Norway, kupitia Shirika lake la Norad, kwa ushirikiano na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Barabara hizo zilijengwa kwa aina yake, ambapo
zilitumia mfumo wa kuwashirikisha wananchi, kwa njia ya nguvu kazi na kutumia
teknolojia ya lami baridi, na kugharimu dola za Marekani milini 11.4
zilizotolewa na Norway na serikali ilichangia dola milioni moja.
Itakumbukwa
kuwa, mvua kubwa zilizonyesha mwaka 2017/2018 pamoja na athari kadhaa zilizojitokeza,
lakini kwa upande wa barabara ya Mizingani-Wambaa eneo la Chumbageni korosini, lilikatika
na kuiacha barabara kutumika nusu hadi leo.
Mwisho
Comments
Post a Comment