NA ASHA ABDALLA ,PEMBA @@@@
KAIMU mkuu wakala wa uwezeshaji Wananchi kiuchumi Ali Mohamed Ali amewataka Wajasiriamali wazingatie masharti na vigezo ambavyo vinatakiwa katika ukamilishaji wa kujaza fomu ya kuombea mkopo ili wapatiwe mkopo kwa haraka na kuweza kuyafanya yale malengo yao waliojiwekea .
Aliyasema hayo Mei 25 wakati walipokua wakipewa Mafunzo ya kuomba mkopo wa 4 4 2 huko katika ukumbiwa wa baraza la Mji Wilaya ya Chakechake mkoa wa kusini Pemba .
Alisema kuwa wajasiriamali ili waweze kuupata mkopo kwa haraka bila usumbufu nilazima wafuate mashatri yote ya kukamilisha vigezo na waondokane nausumbufu ambao utaweza kujitokeza na kuweza kuchelewa kupata mkopo kwamuda wanao taka kupatiwa mkopo huo .
Kaimu huyo alisema kua mkopo wa 4 4 2 ulio chini ya Baraza la Mji umeletwa hususani ni kwa makudi makuu matatu ambao ndio wanaoweza kupata fursa hiyo yakupatiwa mikopo na kuweza kujiendeleza na biashara zao ambazo wanataka kuzifanya .
"Mkopo huo tumeuandaa kwa makundi makuu matatu wakiwemo vijana wenye umri usiozidi miaka 35, wanawake ambao wataweza kujisimamia wao wenyewe bila ya kumshurikisha mwanaume wowote na wale wenye mahitaji maalumu ,hao ndio tulokusudia kuwapatiya mkopo huo "Alieleza
Aidha aliwaomba wajasiriamali hao wanapochukuwa mikop hiyo wanatakiwa kuifanyia biashara ambayo itawapatia tija kwaharaka nakuweza kurejesha mikopo kwa wakati uliokusudiwa kurejeshwa ili na wengine watakapokuja kuja kuomba mkopo waweze kunufaika .
Hatahivyo aliwasihi wazee ambao wameshazidi umri wa miaka 36 wasiendelee kukaa bilaya kujishuhulisha na kazi yoyite waombe mikopo ya covidi19 ambayo inatolewa kwa watu tofauti ili waweze kujikwamua na maisha ya sasa na hapo mbeleni .
Kwaupande Kaimu Mratibu Mitaji na mikopo Haji Khamis Haji alisema kuwa wajasiriamali wote wanaotaka kuomba mkopo wa 4 4 2 nilazima wawe na umri usiozidi miaka 35 pekee ndio wenye sifa yakupatiwa mkopo huo,kwani hilo niagizo kutoka kwa Mh. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Hussein Ali Mwinyi .
Aidha aliwaeleza kua wajasiriamali wanatakiwa kuchukua mkopo zaidi ya mmoja ili kuepusha kuzorota kwa malipo ya mkopo huo na kusababisha Matatizo mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza na wengine kukosa kupatiwa huduma hiyo.
Nae Meneja kutoka Tanzania commercial Bank TCB Tawi la Pemba Shomary Rimosho alisema kua mkopo hiyo haina hasara wala Riba hivyo Mjasiriamali anatakiwa anapokopa mkopo ajitahidi kufanya biashara kwa haraka na kuweza kuzirejesha kwa wakati ili nawengine wapate kunufaika kwa mkopo huo.
Aidha aliwaomba wajasiriamali hao wawe na ukweli pale wanapo jaza fomu ya kuomba mkopo na wawe na ushirikiano mkubwa kati yao na Baraza la mji kwani wao ndio waliowabebea dhamana kuhusu mikopo hiyo.
Kwa upande wake Mratibu wa kamati ya 4 4 2 katika Baraza la manispaa Chake Chake Abdalla Saleh Issa alitoa wito kwa wale wote waliopewa mafunzo hayo waendelee kujitathmini wale ambao wanasifa ya kupatiwa mkopo waanze mchakato wakuomba mkopo kwani baraza lipotayari katika kuwasimamia kwanguvu zote mpka pale watakapo fanikisha suala hilo.
Nae Ali khamisi Ali ambae ni mshiriki wa mafunzo hayo alitowa wito kwa Vijana na Wananchi kwa ujumla kuwa wanapokujiwa na fursa kama hizi wazikimbilie katika kujikusanya vikundi ilikuapatiwa mkopo kwani zimeletwa na Serekali kwaleongo lakuja kuwakomboa wanachi wake.
Hatahivo aliwaomba wajasiriamali wenzake wawe karibu nawale watu ambao wanahitaji maalumu ilikuwaunga mkono nawao ili nawao waweze kunufaika katika kuitumia mikopo hii ikiwa nawao nimiongoni mwa walengwa wa hii mikopo.
Aidha aliwashauri wajasiriamali hao kwa wale wote watakao pata mkopo huo wa 4 4 2 wajitahidi kutumia kwamalengo yaliokusudiwa nasio kwenda kuzitumia kwa kujinunulia mahitaji mengine ambayo hayahusiani namkopo huo .
Mafunzo hayo yameandaliwa na wakala wa uwezeshaji wanachi kiuchumi pamoja na TCB yakiwa chini ya ufadhili wa baraza la mji Chakechake ambayo yanaendelea katika wilaya zote nne za Pemba.
MWISHO
Comments
Post a Comment