Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka
wananchi kuzingatia umuhimu wa Afya ya akili ili kuzuia maafa ambayo yanayoweza
kutokea na kupelekea athari kubwa kwa katika mwili wa binadamu.
Akizungumza katika bonanza
la kuadhimisha kuelekea siku ya afya ya akili
na maafa duniani lilofanyika katika jengo la Chuo cha
Afya Zanzibar Wilaya ya Magharib “B” Unguja, amesema kila mwananchi anapaswa
kutambua umuhimu wa afya ya akili kama ilivyo afya ya mwili ili kujikinga na maafaa
ambayo yanawezakujitokeza.
Amesema
afya ya akili ni muhimu kwa kila mtu kwani inamuwezesha kuishi maisha yenye
furaha, tija na kujisikia vizuri ulimwenguni. Lakini mara nyingi suala hili
halipewi kipaumbele kinachostahili. Hivyo
Waziri huyo amehimiza suala la afya ya
akili kupewa kipaumbele na kila mtu, kutambua kwamba ni sehemu muhimu ya afya kwa ujumla.
“Afya
ya Akili ni muhimu kwa kila mmoja wetu, kwani maafa hayachagui mtu wa kumuathiri, yanaweza kumuathiri mtu
yeyote, mahali popote, wakati wowote” Alisema Waziri Pembe.
Alifahamisha kwamba kila ifikapo
tarehe 13 Oktoba, huadhimishwa Siku ya Afya ya akili na maafa Duniani, siku hii inawakumbusha watu/jamii juu ya
umuhimu wa kuwa tayari katika kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea. Pia alisema
siku hiyo huongeza uelewa wa afya ya
akili na kuleta mabadiliko chanya kwa afya ya akili ya kila mtu.
Aidha Waziri Pembe alisema mwaka huu
2023, katika kuadhimisha Kimataifa siku ya Afya ya akili itachunguza uhusiano
wa pande mbili kati ya maafa na usawa wa kijinsia, hivyo amewaomba wananchi
kupenda kukuhimizana kushiriki katika
kila tukio la kuendeleza umoja, au kujiunga na mazungumzo juu ya kupambana na
usawa wa kijinsia kwa ajili ya maendeleo
ya nchi yetu.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji Chuo cha
Afya Zanzibar (ZSH) Aziza Hemed ametoa wito kwa wananchi kuwa mabalozi wazuri
kuhamisha jamii kupata ushauri nasihi na kisaikolojia pale ambapo wanapopata
matatizo za kimaisha kwani hatua hiyo inaweza kupunguza athari za maafa ambazo
zinatokana na binadamu.
Kupitia bonanza hilo shughuli mbali
mbali zimeandaliwa ikiwemo debeti,michezo,utowaji wa zawadi pamoja na zoezi la
kuhitimisha program ya mafunzo ya msingi “Crash Program”.
MWISHO
Comments
Post a Comment