NA ASHA
ABDALLA, PEMBA@@@@
JAMII imekumbushwa kuwa, moja ya haki kuu ya msingi kwa kila mwanadamu ni ile ya kuishi, hivyo ni kosa kwa mtu mwengine yeyote kumuondolea mwenzake.
Hayo yalielezwa na mtoa mada mwanasheria kutoka
Shirika la Msaada na Haki za Binaadamu Siti Habib Mohamed, wakati akiendesha
mafunzo ya siku nne kwa waandishi wa habari, wadau wa habari na wasaidizi wa
sheria, yanayofanyika Chuo cha Amali Vitongoji Chake chake na kuandaliwa na
Mwemvuli wa asasi za Kirai Pemba PACSO kwa ufadhili wa UNDP.
Alisema kua zana ya haki za binadamu ilianzishwa
mnamo mwaka 1948 baada ya vita vya
kwanza vya dunia, hivyo ni wajibu wa kila mmoja hadi leo hii, kuhakikisha
anailinda na kuitetea haki ya kuishi ya mwanzake.
Alieleza kuwa, haki za binadamu kimsingi ni yale
madai au haki zote ambazo anadai binamu mara baada ya kuzaliwa, na kwa kawida
hakuna taasisi yoyote ambayo inaweza kuzuia.
‘’Ni kweli haki ya msingi kwa kila mwanadamu ni
ile ya kuishi, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anailinda yake
mwenyewe na mwenzake,’’anaelkeza.
Hata
hivyo alieleza kua kupitia Mkataba wahaki za
binadamu ambao uliasisiwa mwaka 1966 na kuanza kufanyaka kazi mwaka 1976,
umeanisha haki nyingine kadhaa za binadamu kama vile kutoa maoni.
Katika hatua nyingine mtoa mada huyo alieleza
kua zipo hatua mbali mbali, ambazo zimekuja kwa ajili ya kuzilinda haki hizo
ikiwa ni pamoja na kuanzishwa wizara maalum, kuanzishwa kwa tume ya Haki za
binadamu na utawala bora.
‘’Lakini hata kuingizwa kwenye katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na ile ya Zanzibar ya mwaka 1894 na uwepo
wa wizara husika na asasi ni sehemu ya kuzilinda,’’alifafanua.
Mapema Mkurugenzi wa PACSO Mohamed Najim Omar,
alisema waliona wakutane na waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za
binadamu na wasaidizi wa sheria, ili kuwajengea uwezo.
‘’Waandishi wananafasi kubwa ya kuhakikisha
wanakemea matendo ya uvunjifu wa haki za binadamu kupitia kazi zao,’’alieleza.
Washiriki wa mafunzo hayo walisema bado elimu
inahitajika kwa jamii, ili wafahamu athari za uvunjifu wa haki za binadamu.
Mshiriki kutoka chama cha ACT Wazalendo Saleh Nassor
Juma, waliishukuru taasisi hii ya PACSO kwa kuwapa mafunzo hayo, ambayo yamewapa
uwelewa zaidi.
Nae mtaangazaji wa Redio Istiqama Pemba Bakar
Khamis Juma, alisema kama mataifa makubwa, yatajenga utamaduni wa kuziheshimu
haki za binadamu dunia itakuwa salama.
Nao washiriki Abubakar Mohamed Ali ,Mwache Juma
Abdalla walisema, kama vyombo vya habari vitakuwa huru kufanya kazi, wanaweza
kukemea matendo ya uvunjifu wa haki za binadamu yanayojitokeza.
Mratibu wa miradi kutoka Shirika la Maendeleo
Ulimwenguni la UNDP Gamalick Sun alisema
wataendelea kuiunga mkono PACSO katika shughuli zao mbali mbali.
Alieleza kuwa, anaamini PACSO ni sehemu ya
uwakilishi wa wananchi, na ndio maana hata mafunzo hayo yamewashirikisha watu
wa kada mbali mbali.
Mafunzo hayo ya siku nne mada kadhaa
zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza, haki za binaadamu, majukumu
ya waandishi wa habari na jukumu la jamii katika kulinda haki za binaadamu,.
Mwisho
Comments
Post a Comment