ASHA ABDALLA NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAANDISHI wa habari, wasaidizi wa sheria na
watetezi wingine wa haki za binadamu kisiwani Pemba, wamesema baada ya
kumalizika kwa mafunzo ya siku nne, sasa wako tayari kuisaidia jamii, namna bora
ya kuzilinda haki za binaadamu.
Walisema kazi iliyofanywa na Mwemvuli
wa asasi za kirais Pemba ‘PACSO’ kwa kushirikiana kwa na Shirika la kimaendeleo
ulimwengini ‘UNDP’ ni jambo jema na lililobakia ni wao kuwafikia wananachi.
Wakizungumza mara baada ya kumalizika
kwa mafunzo hayo, yaliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Chake chake,
walisema wamepata elimu ya kutosha kwa ajili ya kuifikisha kwa jamii.
Watetezi hao wa haki za binaadamu
walisema, PACSO na UNDP wameshatimiza wajibu wao kwa kuwapa mafunzo hayo, sasa
kilichobakia kwao wao, ni kuhakikisha wanakutana na makundi kadhaa ndani ya
vijiji mbali mbali.
Mmoja kati ya washiriki hao Mwalimu
Mwache Juma Abdalla, alisema kazi iliyoko mbele yao ni kukutana na makundi kama
vile wanafunzi, watu wenye ulemavu, wanasiasa na vijana kuwapa elimu hiyo.
Nae mtetezi wa haki za binaadamu Saleh
Nassor Juma, alisema mafunzo hayo yamewafikia wakati mwafaka, kwani kwa sasa
kunamatendo kadhaa ya uvujifu wa haki za binaadamu.
‘’Kwa mfano watoto na wanawake
wamekuwa wakidhalilishwa kingono, kiuchumi, kisiasa, kielimu na hata kijamii,
sasa ni wajibu wetu sisi baada ya mafunzo haya kuwafikia,’’alieleza.
Nae msaidizizi wa sheria kutoka wilaya
y Micheweni Said Salum alisema watayatumia majukwaa ya wasaidizi wa sheria
wenzao, kuhakikisha elimu hiyo inasambaa wilaya nzima.
‘’Ni kweli haki za binaadamu
zinavunjwa wakati mwingine na vyombo vya serikali na kwa kiasi kikubwa jamii
yenywe, sasa tutahakikisha elimu tuliyoipata hapa inaenea,’’alifafanua.
Mwandishi wa kituo cha redio cha ZENJ
Fm Radhia Abdallah na mwenzake wa Muyaba Kombo wa Redio jamii Micheweni walisema,
wataandaa vipindi, makala fupi fupi ili kuielimisha jamii madhara ya uvunjifu
wa haki za binaadamu.
Hata hivyo mwandishi wa ITV na redio
One Pemba Suleiman Rashid amewataka waandishi wa habari wenzake, kufanya
utafiti wa kina wa habari zao za haki binaadamu, ili siwaachie wengine maumivu.
Mtaalamu wa mawasiliano ya umma kutoka
Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba
Gaspary Charles, alisema mwandishi wa habari bora ni yule anayesikiliza kero za
wananchi na kuziripoti, na sio kujiandikia habari mwenyewe.
Katika hatua nyingine mtoa mada huyo,
alisema haki za binaadamu zinauwanja mpana, hivyo waandishi wanajukumu la kuhakikisha
wanawaelimisha wananachi.
Akifunga mafunzo hayo Mwenyekiti wa Mwenvuli
wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ Mohamd Ali Khamis, aliwataka washiriki hao, kuyafanyia
kazi mafunzo hayo, ili lengo la kuomba mradi huo lifikiwe.
Alieleza kuwa, ilikuwa vigumu kwa
PACSO kuwakusanya wananchi na watetezi wote wa haki za binaadamu kisiwani
Pemba, hivyo waliopata nafasi hiyo wawe na hamu ya kuwapa elimu hiyo wenzao.
Mafunzo hayo ya siku nne mada kadhaa
zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza, haki za binaadamu, majukumu
ya waandishi wa habari na jukumu la jamii katika kulinda haki za binaadamu,.
Mwisho
Comments
Post a Comment