NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ UKATILI na udhalilishaji dhidi ya wanawake na wasichana unasalia kuwa kitendo cha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote. Ambapo kila mwaka makadirio ya wanawake milioni 316 sawa na asilimia 11 ya wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 45, hukutana na vitendo hivyo duniani kote, kwa mujibu wa mitandao ya kijamii. Udhalilishaji huo unaweza kua wa kimwili, kingono au kihisia. Takwimu za mwaka 2024 za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha mwanamke mmoja, kati ya watatu amewahi kufanyiwa ukatili huo katika kipindi cha maisha yake. Kwa mujibu wa takwimu za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar, zilizotolewa na ofisi ya Mtakwimu mkuu wa serikali, mwaka 2024 kulikuwa na 1,809 ya ukatili na udhalilishaji wameripotiwa. Takwimu hizi zinaonyesha waathirika wengi walikua watoto ambao ni asilimia 84.3 ikifuatiwa na wanawake ambao ni asilimia 11.7. Aidha utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali, linaloendeleza us...