Skip to main content

NYEZUMA: ‘MRADI WA ‘PAMOJA’ NI WA AINA YAKE KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI’

 


NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

MTAALAMU wa Masuala la Jinsia, kupitia Mradi wa ‘Pamoja’ wa kukuza usawa wa kijinsia Zanzibar, Nyezuma Simai Issa, amesema Mradi huo, ni wa aina yake, na utapunguza wimbi la ukatili na udhalilishaji, pindi utakapomalizika.

Mtaalamu huyo, aliyasema hayo leo Juni 11, 2026 ukumbi wa Samail Gombani Chakechake Pemba, wakati akielezea muhutasiri ya utekelezaji wa mradi huo, kwa Kamati teule ya wilaya ya Chakechake, ya utekelezaji wa mradi huo.

Alisema, jambo jipya ambalo limo ndani ya mradi huo, ni ujenzi wa vituo vinane, vya makuzi na malezi ya awali ya mtoto, ambapo kila wilaya kitajengwa kimoja.



Alisema, lengo la kituo hicho ni kuwapa nafasi wazazi na walezi, kujiendeleza kiuchumi, wakiwa na uhakika wa malezi kwa watoto wao.

‘’Kupitia mradi huu wa miaka mitano, jambo kubwa ambalo limo pamoja na mingine mazuri, tutajenga vituo vinane, kwa wilaya zote nane, zilizopotiwa na mradi huu,’’alifafanua.



Aidha Mtaalamu huyo, alisema jambo jingine ambalo litafanyika, ni kuona kila wilaya mradi unalikarabati jengo moja, chakavu na kwa ajili ya matumizi kama, hayo ya awali.

‘’Mradi huu, pamoja na kuanza kwa ujenzi wa vituo hivyo vinane, lakini pia unapanga kukarabati majengo mingine machakavu kwa wilaya zote, ili nayo yatowe huduma za makuzi na malezi ya awali ya watoto,’’alifafanua.

Hata hivyo alifafanua kuwa, ijapokuwa Mkoa wa Mjini Magharibi, haumo kwenye mradi, lakini mradi utajenga kituo cha kitaifa cha kutoa msaada wa kisaikolojia.



Akizungumza kwenye mkutano huo, Mtaalamu wa masuala ya kijamii, kupitia Mradi huo, Ali Wadi Makame, alisema ndani ya mradi, utawapa mikopo wanawake, waliojikusanya kwenye vikundi vya ushirika.

Alieleza kuwa, hayo yatakuja baada ya kuwapa mafunzo maalum, ya jinsi ya kujikwamua na umaskini na matumizi ya fedha hizo.

‘’Mradi huu, utawapa mikopo ya fedha moja kwa moja wanawakwe walioanzisha vikundi vya ushirika na ambavy0 vimesajiliwa, ili sasa iwe sababu ya kukuza pato lao,’’alifafanua.

Hata hivyo aliwataka wananchi wa Zanzibar, na hasa ambao mradi huo unatekelezwa, kujenga ushirikiano na maafisa watakaopita vijijini, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo.



Kuhusu kanuni za maadili, alisema mradi unataka wajumbe hao kuheshimiana na kujengeana nidhamu wakati wote, wanapokua kwenye shughuli zao.

‘’Ni jambo la kawaida kwa sisi watumishi, sasa kupitia mradi huu zitakuwepo na kisha zitasainiwa na wajumbe wa kamati zote, ili kulinda heshima wakati wote,’’alifafanua.

Katika hatua nyingine, alisema kwa sasa mradi huo kwa kuanzia, unatekelezwa kwa majaribio katika wilaya za Kati kwa Unguja na Chakechake kwa Pemba, na kisha wilaya nyingine za Kusini, Kaskazini ‘A’ na ‘B’ Mkoani, Wete na Micheweni zitafuata.



Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, walisema mradi huo ni nzuri na umekuwa na mwelekeo wa aina ya pekee, katika kupunguza wimbi la ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

Mmoja kati ya washiriki hao ambae pia ni Katibu wa Kamati ya kupambana na udhalilishaji wilaya ya Chakechake Rashid Said Nassor, alisema bado vitendo vya udhalilishaji vinaendelea kutokea.



Nae Salma Khamis Haji, alisema kilichobakia ni kwa jamii, ni kutoa ushirikiano na watendaji walioteuliwa kupitia mradi huo.

Kwa sasa takwimu zilizokusanywa na Ofisi ya Mtakwimu mkuu wa serikali Zanzibar, iliripoti matukio 1,809 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia, kwa mwaka 2024, ambapo waathirika walikuwa 1,809 na wengi walikuwa watoto, sawa na asilimia 84.3.

 



Wilaya ya Chake chake, ilishika nafasi ya nne, kwa kuripoti matukio 113, kati ya wilaya 11 za Unguja na Pemba, huku wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja, ikiwa ya mwanzo kwa matukio 431.

 

Kwa mwaka jana, matukio hayo kwa Unguja na Pemba, yalipungua 581, maana yalikua 1,228, kinyume na yale 1,809 ya mwaka 2024, jambo ambalo hata baadhi ya wilaya, ikiwemo ya Chake chake, yaliripotiwa kushuka.






 


Wilaya iliyoongoza kwa mwaka jana ni Magharibi ‘A’ kwa matukio 247, na wilaya ya Chake chake safari hii, ilipanda nafsi moja, ingawa iliripoti matukio kiduchu 93, tofauti na matukio 113 ya mwaka 2024.

 

Waathirika wakubwa kwa mwaka 2025, ni watoto, waliokuwa 1,050 sawa na asilimia 85.4 kwa Unguja na Pemba, wakifuatiwa na wanawake 162 asilimia 13.2 na wanaume 18, sawa na asilimia 1.5.  

                         Mwisho

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...