Skip to main content

MABODI: ‘IPIGENI 119 KUTOA TAARIFA ZA DAWA ZA KULEVYA’

 



NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

WANANCHI kisiwani Pemba, waetakiwa kuipiga nambari 119, ambayo ni bure, wanapoona kuna viashiria au mtumiaji, muuzaji, msambaazaji na muingizaji wa dawa za kulevya nchini.

Ushauri huo umetolewa leo Juni 13, 2026 na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maryam Juma Abdalla ‘MABODI’, wakati akizungumza na wananchi hao, uwanja wa Gombani Chakechake, kwenye uzinduzi wa siku ya kimataifa ya kupinga dawa za kulevya.

Alisema, kwa upande wake serikali imeshaweka mikakati kadhaa, ikiwemo kuanzisha nambari hiyo bure kwa ajili ya kupokea taarifa, za dawa za kulevya.

Alieleza kuwa, nambari hiyo iko wazi saa 24, na wananchi watakaoipiga watapokelewa na kupewa ushirikiano, ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

‘’Tukiwa ndani ya uzinduzi wa kampeni ya kupinga matumizi, usambaazaji, uingizaji, uuzaji wa dawa za kulevya, leo itumie nambari hiyo bure, ili kuwaokoa vijana wetu,’’alisisitiza.

Aidha Katibu Mkuu huyo, alisema kwa sasa hali inatisha kwa Zanzibar, ambapo mwaka 2015, kulikuwa na vijana watano (5) tu, walioanzishwa dawa maalum za ‘methadone’, ingawa kuanzia mwaka 2016, waliongezeka na kufikia 1,838.

‘’Tiba hii ipo na inapatikana na kutolewa na wizara ya Afya, ili kuhakikisha vijana wanapona, waliotumia dawa za kulevya na kuamua kuacha matumizi hayo,’’alifafanua.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo, alisema ni dhahiri kuwa, vijana wanaendelea kutumia dawa za kulevya, bila ya kujua kuwa wanahitajika kulijenga taifa lao.

Mapema Kaimu Waziri, Ofisi hiyo, Hamza Hassan Juma, alisema serikali inaelewa kuwa waingizaji, wasambaazaji na hata wanaozitengeneza dawa za kulevya ni watu wakubwa, na wenye fedha zao.







Alieleza kuwa, hata hivyo serikali haijalala imeanzisha mipango na mikakati endelevu, ili kupambana na wanaojiita wakubwa wa dawa za kulevya.

Alifahamisha, hakuna hata mtu mmoja, ambae ameitia serikali mfukoni mwake, na watahakikisha wanaoingiza wanahama Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hatua nyingine, Kaimu huyo Waziri ofisi ya Makamu wa Kwanza, alimtaka Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti, na Kupambana na dawa za Kulevya Zanzibar, asimuonea yeyote aibu, pindi wakimkuta na dawa za kulevya.

‘’Hata nikiwa mimi Waziri, au Katibu mkuu, Mwakilishi, sheha na mwingine yeyote, mkamateni na sheria ichukua nafasi yake,’’alifafanua.

Hata hivyo alisema, wale wanaokimbilia kwa viongozi wa juu na kupiga simu ili kupata msamaha wasahau, kwani kila kiongozi kwa sasa, hayuko tayari na hilo.







Aliwakumbusha masheha na kamati zao, kuendelea kufuatilia wanaouza, kutumia, kuingiza, kusambaaza dawa za kulevya, kwenye maeneo yao.

Akizungumzia mbinu za wafanyabiashara hao haramu za dawa za kulevya, aliwatahadharisha wananchi, kuwa sasa dawa hizo, huchanganywa na vyakula kama biskuti.

‘’Tumeshabaini kuwa, sasa dawa za kulevya huchanganywa kwenye ubuyu, peremendi na biskuti, hivyo wananchi wawe makini na hili,’’alifafanua.



Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti dawa za kulevya Zanzibar, Kanali: Bur-han Zubier Nassor, alisema serikali inayodhamira ya dhati, ili kuondoa kabisa dawa za kulevya.



Alieleza kuwa, moja ya athari za dawa hizo, ni kudhoofisha afya ya mtumiaji, vifo, kuongezeka kwa uhalifu na kudumaza uchumi wa taifa.

Mapema Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Rashid Hadid Rashid, aliwakumbusha vijana kuwa wanahitajiwa na taifa lao, kulijenga na hivyo wa kutumia dawa za kulevya, itakuwa vigumu.



Baadhi ya wananchi waliohudhuria, walisema bado adhabu sio kali, kwa wanaokatwa na kutiwa hatiani kwa dawa za kulevya.

Mohamed Issa Haji wa Gombani, alisema kama wanaokamatwa na dawa hizo, wanapewa adhabu ya kunyongwa kama ilivyo mataifa mingine, jambo hilo lingekoma.

Mayasa Hassan Kassim wa Wawi, alisema bado hajaona kupungua kwa watumiaji wa dawa za kulevya, ndani ya jamii.



Kwenye hutuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza mwaka 2023/2024, kuliripotiwa kesi 312 na kufanyiwa kazi, zikiwemo 25 zilizopo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, 31 kwa Mkemia Mkuu, 215 zilifunguliwa mahakamani na kesi 41 ziliendelea na upelelezi.

Kesi hizo zinajumuisha watuhumiwa 316, wakiwemo 306 wanaume na 10 wanawake kwa Unguja na Pemba, kwa kipindi hicho pekee.

Kuhusu utoaji wa huduma za upataji nafuu, zimeendelea kuimarishwa katika kituo cha tiba na marekebisho ya tabia, cha Kidimni Unguja, na waraibu 186 walipokelewa, kati yao 40 waliruhusiwa baada ya kukamilisha tiba, 35 waliondolewa, 60 wametoroka na 51 wanaendelea kupata huduma.

 Hata hivyo, ikaelezwa kuwa, kwa muda wa miaka minne, kutoka 2020/2024, Ofisi imefanikiwa kuwamata watuhumiwa 1,220, wakiwemo wanaume 1,169 na wanawake 51, wakihusishwa na dawa za kulevya zikiwemo bangi kesi 757, heroin kesi 463.

Ambapo kati ya hizo, 1,198 zilifunguliwa, 755 zimefikishwa mahakamani, na wakifanikiwa kuteketeza vielelezo vya dawa za kulevya, vyenye uzito wa kilogramu 1,619.86 kwa kipindi hicho.

Kubwa zaidi, wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha tiba na marekebisho ya tabia kwa waraibu wa dawa za kulevya, kilichopo Kidimni Unguja.

Ambapo kauli mbiu ya mwaka huu, inaeleza kuwa, ‘ushahidi uko wazi, ekeza katika kinga

               Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...