Skip to main content

MSITU WA NGEZI PEMBA NA SAFARI YA UHIFADHI, WATIMIZA MIAKA 67, ILIANZA NA WAKOLONI

 


NA ASHA SALIM- WKUMM, PEMBA@@@@

SEKTA ya kilimo Zanzibar, inaendelea kutumia nyezo muhimu na mipango thabiti, katika kunyanyua wakulima waweze kujikimu na kunufaika kupitia shuhuli za kilimo.

Katika kuhakikisha hilo, ushirikiano wa karibu kupitia washirika mbalimbali wa maendeleo na miradi inayosainiwa na serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kusaidia utekelezaji wa sekta hiyo zinaonekana.

Juhudi hizo, zinaendelea kwa ushirikiano wa karibu, kupitia idara zake, zinazotekeleza majukumu yake chini ya wizara hiyo, na sasa serikali kujivunia kufikia mafanikio makubwa ya kiuchumi.

Eeneo ambalo, serikali imekuwa na mfano mzuri wa utendaji kazi, ni kushughulikia kwa karibu msitu wa hifadhi ya Ngezi Micheweni.

KWANI MSITU WA NGEZI ULIANZIA WAPI

Taarifa zilizopo kwenye tovuti ya ‘Ngezi Vumawimbi Heritage Organization, zinaeleza kuwa, maeneo yanayozunguka msitu wa Ngezi, kumbe yamekaliwa kwa muda mrefu sana na Waarabu au Waajemi waliowahi kuishi.

Infaghamika kuwa, kupitia tovuti hiyo, mabaki ya misikiti na makaburi katika eneo hilo, yanaanzia karne ya 11 hadi ya 14.

Tena ambapo baaadhi ya miundo inaonekana kutumika kama makao makuu na Waarabu au Waajemi, ambao waliishi hapo zamani.

Kuanzia mwaka 1923, ndani ya msitu wa Ngezi, mpango wa kwanza wa usimamizi, maana mataifa ya kikoloni ya Uingereza, yaliandaa mpango wa kwanza wa hesabu (takwimu za msitu Ngezi).

Ambapo mpango na usimamizi, uliolenga matumizi  ya kibiashara ya bidhaa za misitu huo, wakijua kuwa kuna miti mipevu na madhubuti kwa matumizi.

Kuingia mwaka 1957, mfanyabiashara wa kihindi alieitwa V.R. Joshi, aliweka mashine ya kupasulia mbao, katika msitu huo.

Maana mashine hiyo wala haikukaa burea, na kuanza kupasua miti ya mbayo yenye thamani, ukiwemo mti wa Misaji.

Inaelezwa kuwa, baada ya zoezi hilo kukamilika, mfanyabishara huyo, alisafirisha mbazo hizo za Msaji na kwenda nazo nchini India, na sehemu nyingine za bara la Asia.

Ingawa inaaminika kuwa, wazo la kuufanya msitu wa hifadhi, iliashaanza na ndio maana inafahamika kuwa, mwaka 1959 uvunaji wa misitu ulifikia kikomo na Ngezi, ilipotangazwa kuwa ni msitu rasmi wa hifadhi.

Mpango wa kujaza mapengo katika sehemu mbalimbali za msitu, ambapo ulikuwa umekatwa ulifanyika, na kundi la misisi katika mwaka 1963, yaani mwaka mmoja kabla ya Zanzibar, kufanya mapinduzi.

 

Baada ya Zanzibar kufanya mapinduzi, inaarifiwa mashine maalum na za kisasa, zilitaifishwa na serikali ya Rais Karume, na hapo ilipofika mwaka 1959, uvunaji ulisimamishwa rasmi.

 

Mwaka 1996, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini jemedari Abeid Amani Karume, ilianza mpango mpya wa usimamizi, ambao ulizingatia usimamizi endelevu wa rasilimali za msitu.

 

Hadi mwaka 2004, serikali kupitia wizara husika, ilifanya juhudi kubwa za kulipanua na kujumuisha Vumawimbi, kama sehemu ya msitu wa Ngezi ulioko wilaya ya Micheweni Pemba.

 

Msitu huo umepakana na bahari ya hindi kwa kaskazini na imezungukwa na vijiji 10, vilivyomo pia shehia za Mkangale na Mkia Ng’ombe, katika upande wa mashariki, magharibi, na kusini na una ukubwa wa hekta 2,900.

 

Ingawa hifadhi hii msitu wa Ngezi, zipo taarifa nyingine zikihalalisha kuwa, inahusika na eneo la hekta 1, 440 (acre 3 600), nyingi ikijumuisha msitu wa msingi, ambayo ilianzishwa mwaka wa 1959.

 

UFUNGAJI KAMERA ZA ULINZI MSITU WA NGEZI

Kupitia Idara ya misitu, mafanikio yanaonekana katika uhifadhi wa msitu wa Ngezi Vumawimbi, kiteknologia kwa kushirikiana na mradi wa Oikos.

Hii ni baada ya kufunga kamera hivi karibuni, zinazosaidia kuona wahalifu pamoja na kuona wanyama wanaohifadhiwa katika msitu huo.

Ofisa Mdhamni wa wizara hiyo, Idris Hassan Abdalla, anasema wapo wanyama, ambao hawapatikani eneo lolote ulimwengu, isipokuwa Pemba, ambao ni popo wa Pemba, na wale wingine maarufu kama Paa pamoja na Kima Punju.

Anasema ambao miaka ya nyuma hawakuwepo, sambamba na kuimarisha utoaji wa elimu ya utunzaji wa misitu, na matumizi sahihi ya msitu huo kwa jamii.

Anaeleza kuwa, hata wanafunzi katika skuli zilizopo karibu na msitu inayowazunguka kutoka idadi ya waliofikiwa na elimu ya misitu watu 1,600 mwaka 2020 hadi kufikia 2200 kwa mwaka 2025/2026.

Anafafanua kuwa, ufungaji huo wa kamera, unalenga zaidi kuhakikisha usalama wa msitu, ili kuona unazidi kunawiri na kuendelea kuwa tenuri la mapato kwa serikali kuu.

Kumbe, wahalifu wa kuwinda wanyama na ukataji wa majengo, walikuwa wakitumia nafasi ya uhaba walinzi na kupora mali za msitu huo.

Ndio maana serikali kuu, kupitia wizara husika, ilikuja na wazo ya kufunga kamera ndani ya msitu huo, ili kuulinda kisasa zaidi, na kuona unawanufaisha walio wingi zaidi.

Anasema, serikali imekuwa ikijivunia hifadhi hiyo, ambayo kwa sasa inatimiza miaka 67, tokea kuasisiwa kwakwe mwaka 1959, na wakoloni waliokuwepo.

Akawataka wananchi, kuendelea kuilinda rasimali hiyo, ambayo imekuwa ikikitangaaza kisiwa cha Pemba kiutalii, kwa kuwepo miti, ndege na wanyama adimu duniani.

 


Mkuu wa hifadhi hiyo Khamis Ali Khamis, anasema kamera zilizofungwa ni 24 na mbili ya kati ya hizo ni kwa ajili ya ulinzi wa wahalifu masitu na zilizobakia ni kwa ajili ya kufuatilia wanyama.

‘’Hizi kamera za ulinzi zintasaidia mno kubaini wahalifu wa miti, lakini hizi 22 kwa ajili wanyama, zimetusaidia kubaina aina nyingine za wanyama,’’anafafanua.

Hata Mkuu wa wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja, amekuwa akielezea kukerwa kwake, na baadhi ya wananchi, wanaouhujumu msitu huo.

‘’Wakati mwingine hata wapika pombe haramu, wavunaji mbao na majengo nao walikuwa kero, ingawa kwa sasa, baada ya kufungwa kamera hujuma sio sana,’’anasema.

Lakini akawataka wananchi, kuendelea kuisadia serikali, katika ulinzi wa rasimali za msitu huo, ambao ni urithi kutoka kwa watawala.

WANAOZUNGURUKA MSITU HUO WANASEMAJE

Nassor Kassim Rashid ni mwananchi wa karibu ya eneo la msitu, anasema hazina hiyo ni tunu, ambayo ni muhimu kwa maisha yao na wanyama na hata serikali katika kuengeza pato.

‘’Hatuna budi kuulinda huu msitu, ni hazina kwa maisha ya viumbe hai, watalii wanakuja kutoka mbali, kuona wanyama na miti adimu,’’anasema.

Issa Haji Machano, anasema wamekuwa walinzi wakubwa wa msitu huo, hata kabla ya serikali kufunga kamera, maana upepo, mbolea na mvua wanazopata anaamini ni uwepo wa hifadhi hiyo.

‘’Unajua sisi ambao tupo pembezoni mwa msitu huu, hata afya zetu zimeimarika, maana tunaishi na kijani kibichi ambacho ndio nembo ya kisiwa cha Pemba,’’anasema.

Hidaya Ali Said, anasema wamekuwa wakiwapeleka wageni wao, wanaokuja kuwatembelea, na kuondoka na mzigo wa elimu na maajabu mingine yaliomo hifadhini.

Hafsa Issa Haji, anasema hupeleka bidhaa wanapokuja wageni kuutembelea msitu huo, na kuuza kwa thamani kubwa, kama vile mikoba ya ukindu na mikeka.

‘’Kwa sasa sijawahi kushuhudia wala kusikia uwepo wa wahalifu wa msitu huo, au wawindaji haramu, maana serikali imeshafunga kamera maalum,’’anasema.

Msitu wa Ngezi ni miongoni mwa mifumo muhimu ya ikolojia, na wanadamu hupata faida nyingi kutoka katika msitu, ikiwemo ya kiuchumi, kiutalii, kiutamaduni na kimazingara.

                           Mwisho .

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...