Skip to main content

Posts

WAKILI WA UTETEZI KESI YA UDHALILISHAJI PEMBA AOMBA KUFUTIWA SHTAKA MTEJA WAKE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:::   WAKILI wa utetezi, Massoud Mohamd Said, katika shauri la kuingilia kinyume na maumbile, ameiomba mahakama maalum ya kupambana na makosa ya udhalilisjaji ya mkoa wa kusini Pemba, kuliondosha shtaka hilo, kutokana na upande wa mashataka, kushindwa kuwasilisha mashahidi.   Alidai kuwa, mahakama inamakali mithili ya kiwembe na ina nguvu hata kusukuma jabali, sasa ni vyema wakazitumia, ili shataka hilo, kuliondosha na lisimuumize mteja wake.   Aidha wakili Massoud, alida kuwa mteja wake Haroub Bakar Hamad miaka 22, bado ni kijana mdogo anahitaji kuweko uraiani, ili aendelee na shughuli zake, na sio kuendelea kuumia akiwa rumande.   Wakili huyo, aliyadai hayo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, mara baada ya upande wa mashataka kudai kuwa, shauri hilo lipo kwa ajili ya kusikilizwa, ingawa hawakupokea mashahidi.   Ndipo Hakimu alipompa nafasi wakili huyo wa utetezi, na kudai kuwa, sasa imekuwa wimbo wa ...

MAMA ZAINAB AKUMBUSHIA ADA SKULI 'BETTER CHANGE ACADEMY' KWA WAZAZI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::  MKE wa Makamu wa Kwanza wa rais Zanzibar, Zainab Kombo Shaib, amewakumbusha wazazi na walezi wenye watoto wao skuli ya maandalizi na msingi ya ‘Better Change Academy’ ya Gombani Chake chake Pemba, kulipa ada zao kwa wakati, ili kufanikisha azma ya waalimu kuwapatia elimu bora watoto wao.   Alisema kama wapo waliookeza kwenye elimu kwa kuanzisha kituo cha elimu ya maandalizi na msingi, ni wajibu kwa watakaopeleka watoto wao hapo, kulipa kipaumbele suala la ada.   Mke huyo Makamu wa Makamu wa Kwanza, ameeleza hayo ukumbi wa Samail Gombani Chake chake Pemba, kwenye mahafali ya pili ya skuli hiyo, yalioambatana na siku ya wazazi.   Alisema, mazuri yalioonekana kwenye sherehe hizo, msingi wake mkuu ni wazazi na walezi, kukubali kulipa ada zao kwa wakati.   Alieleza kuwa, elimu ni jambo pekee la thamani na ndio urithi pekee kwa mtoto, hivyo ni wajibu kwa mzazi ama mlezi huiska, kulitia maanani, jambo hilo.   "...

AFUNGWA MIAKA 7 PEMBA KWA KUMBAKA MTOTO WAKE WA KUMLEA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:: MSHTAKIWA Said Abdalla Issa (40) wa Chanjamjawiri na Kengeja, ameanza maisha mapya chuo cha mafunzo, kwa muda wa miaka saba (7), baada ya mahakama maalum ya kupambana na makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, kukumuta na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kulea mwenye miaka 14. Pamoja na kutumikia adhabu hiyo, aidha hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, alimtaka mshitakiwa huyo kumlipa fidia ya shilingi milioni 1 muathirika huyo, haraka iwezekanavyo.   Mshitakiwa huyo ambae alimbaka mtoto wake huyo kumlea mwanzoni mwa mwaka 2019, kisha kesi hiyo kwa mara ya kwanza, ilifunguliwa mahakamani hapo, Mei 23, mwaka huo huo na upande wa mashataka, ukaanza kuwasikiliza mashahidi.   Akisoma hukumu ya kesi hiyo, hakimu Muumini alisema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ambao haukucha chembe ya shaka, ulitosha kumtia hatiani mshatakiwa huyo.   Alisema, mtu pekee anaeweza kuthibitisha kuwa ameingiliwa ni muathirika, na upande w...

MZEE 'SODA' MIAKA 76, ATUNDIKWA MIAKA 10 CHUO CHA MAFUNZO KWA UBAKAJI PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: HATIMAE mahakama maalum ya kupambana na makosa ya udhalilishaji Mkoa wa kusini Pemba, imemswekwa chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 10, mshitakiwa Khamis Juma Chumu ‘ soda ’ (76) mkaazi wa Mtoni Chake Chake, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 13.   Hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, alisema kati ya adhabu hiyo, mshtakiwa atatumikia chuo cha mafunzo miaka 10 kwa kosa la ubakaji wa mtoto huyo.   Akisoma hukumu hiyo, alisema upande wa mashtaka ulifanikiwa kuwasilisha mashahidi watano kwenye kesi hiyo, akiwemo mtoto mwenyewe, ambae alitosha kwa kiwango kikubwa, ushahidi wake kuishawishi mahakama.   Alisema, mtoto ndio shahidi mkuu anayepaswa kuihakikishia mahakama kuwa, alibakwa na kutorosha ama laa, na sio mtu mwengine yeyote.   Hakimu huyo akiendelea kusoma hukumu hiyo alisema, wakati mtoto huyo wa miaka 13 anatoa ushahidi wake mahakamani hapo, akiongozwa na wakili wa serikali Ali Amour Makame, a...

KONGAMANO SIKU 16: ZLSC CHASIKITISHWA BABA, WAJOMBA KUWABAKA WATOTO WAO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ kimesikitishwa na kitendo cha baadhi ya baba wazazi, walezi na waalimu wa madrassa, kuwafanyia vitendo vya ukatili na udhalilishaji watoto walio na mamlaka nao. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Kituo hicho Harusi Miraji Mpatani, kwenye maelezo yake yaliotolewa na Mratibu wa kituo hicho Pemba Safia Salehe Sultan, kwenye kongamano la kuelekea siku 16 za kupinga ukatili, lililofanyika Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake chake. Mkurugenzi huyo alisema, katika utafiti wa miezi tisa, uliofanywa na Chama cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar, watu 182 walifanyia usaili ili kupata taarifa hizo. Alisema, kati ya watu hao wanawake 115 na wanaume walifikiwa 67 kutoka kisiwa cha Unguja na Pemba, ambapo moja ya malengo ya utafiti huo ni k ufichua kesi zilizo jificha kutokana na muhali na mkwamo katika ngazi za chini mpaka kufikia muafaka wa kesi husika.   Alieleza kuwa, ameshtushwa na kubainika kwa...

KONGAMANO SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI PEMBA LAWAONYESHEA VIDOLE WATOTO KUANZIA MIAKA 14

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:: MAHAKAMA maalum ya kupamba na makosa ya ukatili na udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, imesema kesi za udhalilishaji zinazowahusu watoto wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 17, ndio pekee zinazowatesa wao na ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka, kwa kule kukataa kutoa ushahidi. Kauli hiyo, imetolewa na Hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, wakati akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuali yalioulizwa na wananchi, kwenye kongamano la kuelekea siku 16 za kupinga ukatili, lililofanyika Kiwanda cha Makonyo Wawi. Alisema, mara matukio hayo yanapotekezea kwenye jamii, wazazi wao huwa na ari, kasi na hamu ya kuyafikisha mbele ya vyombo vya sheria, ingawa baada ya muda, hawaonekani mahakamani. Alisema, na hasa kesi za aina hiyo zinazowaweka njia panda ni zile zinazowakabili watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi 17, ambao kimatendo ni watu wazima. ‘’Hao wanaobahatika kufika mahakamani, basi wakati wa kutoa ushahidi hueleza kuwa, wale watuhumiwa waliodai kuwab...