NA
HAJI NASSOR, PEMBA::
MSHTAKIWA
Said Abdalla Issa (40) wa Chanjamjawiri na Kengeja, ameanza maisha mapya chuo
cha mafunzo, kwa muda wa miaka saba (7), baada ya mahakama maalum ya kupambana
na makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, kukumuta na hatia ya kumbaka
mtoto wake wa kulea mwenye miaka 14.
Pamoja
na kutumikia adhabu hiyo, aidha hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma,
alimtaka mshitakiwa huyo kumlipa fidia ya shilingi milioni 1 muathirika huyo,
haraka iwezekanavyo.
Mshitakiwa huyo ambae alimbaka
mtoto wake huyo kumlea mwanzoni mwa mwaka 2019, kisha kesi hiyo kwa mara ya
kwanza, ilifunguliwa mahakamani hapo, Mei 23, mwaka huo huo na upande wa
mashataka, ukaanza kuwasikiliza mashahidi.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo,
hakimu Muumini alisema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ambao haukucha
chembe ya shaka, ulitosha kumtia hatiani mshatakiwa huyo.
Alisema, mtu pekee anaeweza
kuthibitisha kuwa ameingiliwa ni muathirika, na upande wa mashataka uliweza
kumuongoza vyema mtoto huyo, na kukiri kuingiliwa kwake.
‘’Mtoto kwanza alimfahamu
mshitakiwa (baba yake wa kufikia), na kisha aliieleza vyema mahakama, namna
alivyobakwa kutoka hatua moja hadi nyingine,’’alisema.
Aidha hakimu alisema, mtoto
huyo (aliyebakwa), alimtambua bila ya shaka yoyote mshitakiwa huyo, alipokuwa
mahakamani, na hatua zilizochukuliwa na mama yake wa kulea, baada ya kubakwa.
‘’Lakini hata maelezo ya
askari mpelelezi, nayo yaliunga mkono vyema maelezo ya mtoto, aliyoyatoa wakati
akihojiwa kituo cha Polisi wilaya ya Chake chake, na kuzidi kuunga nguvu
ushahidi huo,’’alisema Hakimu.
Katika hatua nyingine Hakimu
huyo, alisema upande wa mashataka, ulithibitisha bila ya shaka umri wa mtoto
kuwa ni miaka 14, ambapo kisheria hana ridhaa kwenye makosa ya ukatili na
udhalilishaji.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu
hiyo, upande wa mashtaka ukioongozwa na wakili wa serikali Ali Amour Makame,
uliiomba mahakama hiyo, kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa.
‘’Vitendo vya ukatili na
udhalilishaji vimekuwa vikiwaandama watoto, na wakati mwengine wamekuwa wakifanyiwa
na watu wao karibu kama kaka au baba, sasa ni wakati wa mahakama kutoa adhabu,
ambayo itakuwa fundisho kwa wengine,’’alisema.
Hata hivyo, upande wa
utetezi ukiongozwa na wakili wake Abeid Mussa Omar, aliiomba mahakama hiyo,
kumpunguzia adhabu mteja wake.
Alisema kuwa, bado ni nguvu
kazi ya taifa, samba mba na kuwa na familia kubwa inayomtegemea, hivyo kama
akipewa adhabu kali, anaweza kusababisha athari.
‘’Mteja wangu anafamilia
kubwa inayomtegemea kwa kila kitu, sasa ni vyema kwa upande wa mahakama,
ikalizingatia hilo, ili kuweko kwake ndani, isiwaumize wengine,’’aliomba.
Baada ya maombi ya pande
zote mbuli, hakimu alisema ameyazingatia, na kuamua kumpeleka chuo cha mafunzo kwa
muda wa miaka saba (7), na kumlipa fidia muathirika ya shilingi milioni 1.
Shahidi wa mwisho katika
kesi hiyo, alikuwa ni mke wa mshtakiwa huyo, Shemsa Hakim Khamis wa
Chanjamjawiri wilaya ya Chake chake, ambae awali alidai kuwa, mume wake hakumbaka
mtoto wao wa kumlea, bali ni uongo alioutengeneza mtoto huyo.
Hata hivyo ushahidi huo, haukusaidia
kumnasua mume wake kwa kosa la ubakaji kwa mtoto huyo, na hatimae juzi Novemba
29, mwaka 2022, kuhukumiwa miaka 7 na kulipa fidia ya shilingi milioni 1,
ingawa haki ya rufaa imetolewa.
Mshtakiwa Said Abdalla Issa mkaazi
wa Kengeja na Chanjamjawiri wilaya ya Chake chake, alimbaka mtoto wake wa
kulea, tokea mwaka 2019.
Kufanya hivyo ni kinyume, na
kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6
ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment