NA HAJI NASSOR,
PEMBA::
MKE wa Makamu wa
Kwanza wa rais Zanzibar, Zainab Kombo Shaib, amewakumbusha wazazi na walezi
wenye watoto wao skuli ya maandalizi na msingi ya ‘Better Change Academy’ ya
Gombani Chake chake Pemba, kulipa ada zao kwa wakati, ili kufanikisha azma ya
waalimu kuwapatia elimu bora watoto wao.
Alisema kama wapo waliookeza kwenye elimu kwa kuanzisha kituo
cha elimu ya maandalizi na msingi, ni wajibu kwa watakaopeleka watoto wao hapo,
kulipa kipaumbele suala la ada.
Mke huyo Makamu wa Makamu wa Kwanza, ameeleza hayo ukumbi wa Samail
Gombani Chake chake Pemba, kwenye mahafali ya pili ya skuli hiyo, yalioambatana
na siku ya wazazi.
Alisema, mazuri yalioonekana kwenye sherehe hizo, msingi wake
mkuu ni wazazi na walezi, kukubali kulipa ada zao kwa wakati.
Alieleza kuwa, elimu ni jambo pekee la thamani na ndio urithi pekee kwa mtoto, hivyo ni wajibu kwa mzazi ama mlezi huiska, kulitia maanani, jambo hilo.
"Niwakumbushe wazazi na walezi wenzangu, tuhakikishe
tunajipanga vyema, ili kuona kuwa uhai wa skuli hii ambayo ni ada, zinalipwa
kwa wakati,"alieleza.
Katika hatuna nyingine, Mke huyo wa Makamu wa Kwanza wa rais
Zanzibar, Zainab Kombo Shaib amewataka wazazi wa kike kuacha utamaduni wa
kuwapa watoto wao simu, kama sehemu ya ulezi.
Alieleza kuwa, siku hizi watoto wamekuwa wakilelewa na picha za
katuni, milio ya simu ili mzazi ama mlezi apate wasaa wa kufanyashughuli zake
nyingine, akijua mtoto wake yuko salama.
"Sasa simu ndio mlezi wetu nambari moja, sisi baada ya
kuzaa mlezi wa watoto wetu ni milio ya simu na katuni na bila ya kujua kuwa,
hicho ni moja ya chanzo cha ubakaji,"alifafanua.
Alisema kuwa sasa wale wanawake waliokuwa walezi ndio wanaoishia
kwenye kumbi za starehe, harusi na huo wakati mdogo unaopatikana, watoto baada
kunyonyeshwa wanapolia, huachiawa simu kama mlezi wao.
Akizungumza kuhusu skuli hiyo, Mke huyo wa Makamu wa Kwanza wa
rais Zanzibar, mama Zainab Kombo Shaib, aliupongeza uongozi wa skuli hiyo, kwa
juhudi zao kubwa.
"Skuli ndio kwanza ina miaka miwili, lakini matunda yake
kama vile inamiaka 10, kwa kweli waalimu wanapiga kazi,"alifafanua.
Hata hivyo ameiomba wizara ya elimu na mafunzo ya amali, kuwa
karibu mno na skuli hiyo ili kufanikisha azma yao, ya kutoa elimu yenye kiwango.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya wazazi skulini hapo,
Khalfan Amour Mohamed alisema, licha ya changamoto wanazokabiiana nazo, lakini
juhudi za walimu zinaonekana kwa vitendo.
Alieleza kuwa, skuli hiyo ambayo bado ni changa kwenye ramani ya
mji wa Chake chake, lakini wamekusudia kuleta mabadiliko makubwa ya kielimu kwa
haraka.
"Changamoto ya uhaba wa vyumba vya kuosomea na idadi ya
waalimu saba ni ndogo, ingawa tunaendelea kujipanga, kufikia ndoto,"alieleza.
Akizungumzia umuhimu wa elimu, sheikh Said Abdalla Nassor
alisema, hilo ndio jambo pekee ambalo mzazi anatakiwa kuhakikisha, anampa mtoto
wake.
Akisoma risala Maaidizi Mwalim mkuu wa skuli hiyo, Issa Kingawaya,
alisema moja ya changamoto wanazokabiliana nazo, ni ukosefu wa huduma ya maji
safi na salama skulini hapo.
Aidha alieleza, kuwa jambo jengine ambalo ni kero kwao ni
uchakavu wa barabara, iliyoingia skulini kwao kutoka barabara kuu ya Chake
chake.
Katika mahafali hayo, yalioambatana na siku ya wazazi michezo
kadhaa iliyopamba jukwaa, ilikuwepo ikiwa ni pamoja na utenzi, igizo, wimbo na
masuala ya ibada kama dua sira hadithi kur-an tafsiri.
MWISHO
Comments
Post a Comment