NA
SAIDA ALI, PEMBA@@@@
VYAMA
vya siasa vitambue kuwa kuna watu wenye ulemavu wa uziwi na wana haki ya kusikiliza
kampezni zao.
Kuna baadhi ya vyama
havijazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu, hasa wale wenye uziwi, katika
mikutano.
Jambo ambalo linalowanyima
haki yao ya msingi ya kufatilia sera za vyama, ili siku ya kupiga kura wafanye
uamuzi sahihi.
Vipo vyama 17 vilivyosimamisha
wagombea na 11 vimefanikiwa kusimamia wagombea urais, ingawa ni chama cha
mapinduzi CCM pekee ndio kinachotekeleza ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu
wa uziwi.
Imefahamika vyama vyengine
vimekuwa vikiendesha kampeni zao bila ya kuwashirikisha watu wenye ulemavu wa
uziwi, kwa kukosekana kwa wakalimani wa lugha za alama.
Tena zipo asasi za kiraia
kadhaa ikiwemo ile ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya
Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO), Jumuiya ya Wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-Zanzibar, zimekuwa zikipigia kelele
na kutetea haki za watu wenye ulemavu.
Hapa Kaimu Mratibu wa
TAMWA-Ofisi ya Pemba Amina Ahmed, anasema hasa kundi la viziwi wamekuwa
wakikosa sera za vyama, kwa kukosekana wakalimani.
‘’Ni kweli tumekuwa
tukipiga kelele kila uchao, ili kuona wakati huu vyama vikinadi sera, zinakuwa
sera jumuishi kwa wenzetu hawa,’’anasema.
Anasema wamekuwa wakitoa
mafunzo kwa waandishi wa habari ili kuteteta haki za watu wenye ulemavu.
Kwa mujibu wa Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) watu wenye ulemavu wapatao 8,021 wanatarajiwa
kushiriki katika uchaguzi mkuu mwaka huu Zanzibar.
Mkurugenzi wa uchaguzi
Idarous Faina anafafanua kua, kati ya hao wapo viziwi 1,667 wenye ulemavu wa
ngozi wakifikia 102 na wasioona 678.
Mkataba wa kimataifa wa haki
za watu wenye ulemavu wa mwaka 2006 (CRPD), ibara ya 29 (a), inazitaka nchi
wanachama, kuhakikisha kuwa, watu wenye ulemavu wanashiriki kikamilifu katika
medani ya siasa.
Ukataba ukafafanua kuwa,
tena iwe kwa misingi iliyo sawa na wingine, ikiwa ni pamoja na fursa ya kuchangua
na kuchaguliwa.
‘’Watu wenye ulemavu,
wanatakiwa kuwekewa mazingira sahihi ikiwemo kupata taarifa, ili kushiriki
kikamilifu katika masuala ya umma bila ya ubaguzi wowte,’’umefafanua mkataba
huo.
Sheria ya watu wenye
ulemavu Zanzibar nambari 8 ya mwaka 2022, kifungu chake cha 29 kinaeleza
umuhimu wa watu wenye ulemavu kuweza kufikia miundo mbinu mbali mbali pamoja,
taarifa mawasiliano na haki zote za kibinaadamu za msingi.
Ikifafanua kuwa, suala la
kuwepo kwa wakalimani kumbe kwa mujibu wa kifungu hicho na kile cha 28 (1)(d),
kinachofafanua suala la kupata taarifa, ni jambo la lazima kwao.
Ndani ya Katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 11 na 12, kikabainisha kuwa, usawa kwa
binaadamu wote mbele ya sheria, binaadamu wote huzaliwa kupata uhuru, anastashiki
heshima ya kutambuliwa kuthaminiwa utu wake wanayo haki bila ya ubaguzi wowote.
Hata kile cha 18,
kinasisitiza haki ya kupokea, kutoa na maoni ni haki ya kikatiba, ingawa
haikuwataja watu wenye ulemavu, ikijumuisha raia wote.
Taarifa ya fedha ya mwaka
2022/2023 ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, ilishirikiana na Madrasa Early
Childhood Program, kuendesha mafunzo kwa viongozi kadhaa wakiwemo Makatibu
wakuu, Maafisa Wadhamini, ili kuwajengea uwezo, wajibu wa kuwajali watu wenye
ulemavu.
VIZIWI
WENYE WANASEMAJE
Adinani Khamis Juma ni
mlemavu wa uziwi akizungumza chini ya mkalimani wake, anasema vyama vya siasa,
bado havijawashirikisha kusikiliza sera zao, wakati huu wa kampeni.
Anasema kwa kupewa
ukalimani tu, anaona gari za matangaazao ya kampeni, ingawa baadae hajui nini
kinaendelea.
‘’Kwa kweli mimi kupitia rangi za chama tu,
ndio huwa najua kuwa kile ni ACT, CCM, AAFP, ADA TADEA au Chaumma, lakini
sisikii sera na ahadai zao,’’analalamika.
Yumma Mohamed Mbarouk,
anasema hata wakati mwingine hajui mikutano hiyo ya kampeni inafanyika wapi,
hushuhudia foleni na gari na pikipiki tu.
Anasema, vyama vimewasahau
kuwa nao, wanahitaji kusikia sera na ahadi, ili ikifika Oktoba 29, mwaka huu
wafanye uamuzi sahihi.
Mohamed Khamis wa Wawi,
anasema sikio lake ni kuwepo mkalimani wa lugha ya alamam, ili awafafanulie,
ingawa hilo halipo.
Zaina Mohamed Ali, anasema
vyama vya siasa vimekuwa viwaacha nyuma, na kuzisahau sheria, mikataba na
katiba kwamba wanahaki sawa ya kupata taarifa kwa aina ya ulemavu wao.
‘’Wakati mwingine nakwenda
kwenye mikutano mtupu na narudi sikuvuna jambo, kubwa nashuhudia wasanii
tu,’’analalamika.
‘’Tunaathirika hatupati
sera za vyama isapasavyo, labda kwa chama nnachokipenda ndio naweza kubagua kwa
rangi tu,’’ anasema.
Mwalimu wa mkalimani wa
lungha za alama Asha Issa Mohamed, anasema Chama cha Mapinduzi pekee, ndio
kinachozingatia na kuwashirikisha watu wenye ulemavu wa uziwi.
‘’Wamekuwa wakituarifu na
kutaka taratibu za kupatikana kwa mkalimani, na wale wenzetu ambao ni viziwi na
ni CCM, hupata taarifa na sera za chama chao,’’anasema.
WANAJAMI
Fatma Ali Hamad, jamii
anaeshiriki kwenye kampeni za vyama vya siasa, anasema watu wenye ulemavu wa
uziwi, bado hawajazingatiwa mahitaji yao, katika kufikiwa na sera za vyama.
Issa Haji Mohamed, asema
inawezekana vyama havihitaji kura za viziwi ndio maana, vimekuwa vizito
kuwawekea mkalimani kwenye mikutano.
Mwanaisha Hassan Khamis,
anasema sheria na mikataba hazijawasahau watu wa kundi hilo, ingawa baadhi ya
vyama bado ni changamoto.
VYAMA
VYA SIASA VINAJIBU NINI
Katibu wa CCM mkoa wa kusini
Pemba Kajore Vyohoroko, anasema wamekuwa wakiwatumia wakalamani hasa wanapokuwa
na wagombea ngazi ya urais, kusudi viziwi wapate sera.
Maana Katiba ya chama hicho,
ya mwaka 1977 toleo la 2007, linaeleza kua CCM, kinaamini kwamba watu wote ni
sawa.
Mwenyekiti wa chama cha
ACT –Wazalendo Mkoa wa kusini Pemba Mohamed Abdallah anasema, hutumia watu wa
karibu na viziwi, katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa.
Anasema kuwa, bado chama
kinaupungufu wa wataalamu wa lugha ya alama, hivyo inawawia vigumu kupata
wataalamu wa kutosha wa kuwatumia katika mikutano yao.
‘’Tutafanya jitihada zetu
ipasavyo kuhakikisha kundi hilo muhimu linapata ujumbe unaokusudiwa,’’ anasema.
Makamu Mwenyekiti wa Chama
cha Alliance Afrika Farmers Party (AAFP) Omar Juma Said, anasema bado wako
nyuma hawajapata muamko na elimu ya kuwafikia watu wenye ulemavu wa uziwi.
Anasema anajua kuwa, watu
wenye ulemavu wana haki za msingi ya kuchagua, kusikiliza pamoja na kupata
taarifa, ingawa kwa sasa suala la kuwapatia taarifa halijafanyika.
‘’Ni kweli watu wenye
ulemavu wa uziwi hatujawashirikisha katika kusikiliza ilani ya chama chetu,
mikutano yote tuloifanya hapakuwa na mkalimani wa lugha za alama,’’ anakiri.
Chausiku Khatib Mohammed
ni Mgombea mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani kwa tiketi ya
NLD, anakiri kuwa, hawajawashirikisha na wamesahau kama kuna watu wenye ulemavu
wa uziwi.
‘’Kwa sisi tumesahau kabisa, kama kuna watu
wenye ulemavu wa uziwi, mpaka sasa hatujawashirikisha juu ya kusikiliza ilani
ya sera za chama chetu, na kura zao
tunazihitaji,’’anafafanua.
Asha Said Suleiman ni Mgombea
Uwakilishi wa Jimbo la Mtambile Chama cha ADA-TADEA anasema,
hawajawashirikisha watu wenye ulemavu katika kunadi sera zao.
Anasema hata kama wamepewa
mafunzo na TAMWA juu ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu, ingawa, hushindwa
kwa gharama ya mkalimani.
‘’Mkakati wetu ni kupita
nyumba kwa nyumba, kutangaza sera ya ilani ya chama chetu, kwa kila mwenye
ulemavu wa uziwi, ili wasaidizi wao waweze kuwasaidia,’’anasema.
TUME
YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA
Suleiman Salim Ahmad ni
Afisa Mfawidh Tume ya haki za binaadamu na utawala bora Pemba, anasema ni kweli
tume imegundua pengo lipo hasa katika mikutano ya hadhara.
Anasema wamekuwa wakitoa
mafunzo kwa vyombo vya habari, ili kupeleka ujumbe juu ya haki za binadamu kwa
kufanya makala vipindi na hata habari.
BARAZA
LA WATU WENYE ULEMAVU
Mratibu wa barazala la Taifa la watu wenye ulemavu Pemba
Mashavu Juma Mabrouk anasema wamekuwa wakinasihisha vyama vya siasa kwenye
vyombo vya habari ili kuandaliwa mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu.
‘’Tumekuwa tukitetea haki
za watu wenye ulemavu kupitia vyombo vya habari juu ya mchakato wa kampeni unaondelea kuwekwa wakalimani wa lugha za alama,’’
anasema.
JUMUIYA
ZA WATU WENYE ULEMAVU
Maryam Mohamed Salum ni
Afisa watu wenye ulemavu Pemba, anasema wamekuwa wakihamasisha sana serikali, tasisi
na mashirika kuwa kila kitu washirikishwe watu wenye ulemavu.
Anasema ni CCM pekee, tena
kwa mikutano ya ngazi ya urais, watu wao wenye uziwi, hunufanika na
kinachozungumzwa.
MWISHO.



Comments
Post a Comment