NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@
TUME ya uchaguzi Zanzibar ‘ZEC’ imesema
imeshaandaa mazingira rafiki kwa watu wa
makundi maalumu, wakiwemo wenye ulemavu,
ili kuh’akikisha ushiriki wao, katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29
mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Kamishna wa tume hiyo Pemba
Ayubu Hamad Bakar, wakati akizungumza na wadau wa uchaguzi, katika mkutano
uliofanyika ukumbi wa mikutano Wawi Chake chake Pemba.
Alisema ili kuhakikisha makundi hayo yanashiriki
ipasavyo katika uchaguzi huo ‘ZEC" imeweka vituo vya kupigia kura, katika
maeneo yanayofikiwa na kila mmoja.
Alisema jingine ZEC, imeandaa vitambulisho maalumu
kwa watu wenye ulemavu, imetoa mafunzo maalum kwa maafisa wake, yanayozingatia uhitaji
wa watu hao pamoja na kuchapisha vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu wa uoni.
"Ili kuhakikisha ushiriki wa kila mmoja katika
mchakato huu wa kidemokrasia, tumeweka mazingira rafiki kwa kila mmoja, ikiwa
ni kuwafundisha maafisa wetu, jinsi ya kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu na
kwa mwaka huu,’’alifamisha.
Alieleza kua, watu wenye ulemavu ni wadau muhimu
katika kufanikisha zoezi la upigaji kura, kwani wanaidadi ya kubwa katika
daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisisitiza kuwa, upigaji kura ni haki ya kikatiba ya kila mmoja na kipengele muhimu cha kidemokrasia na utawala bora, ambavyo ni muhimu katika maendeleo ya nchi na watu wake.
Aliongeza kuwa, ushirikishwaji wa makundi hayo ni
utekelezwaki wa sera ya jinsia ya 2025, inayolenga ujumuishi, wa kila mtu
katika jamii kwenye hatua zote za kimaendeleo
ikiwemo ya kidemokrasia.
Akizungumzia umuhimu wa ushiriki wa makundi maalumu
katika mchakato wa uchaguzi mkuu, Kurugenzi ya elimu ya wapiga kura na
mawasiliano kwa umma Juma Sanif Shehe alisema, ni kuwezesha utekelezaji wa haki za binaadamu,
pamoja na kuhakikisha ushiriki wao katika demokrasia.
Aliongeza kua, ili kuhakikisha uchaguzi jumuishi
tume imetoa mafunzo kwa watu hao, na
kuanzisha madawati katika ngazi za kiutawala, katika tume hiyo ili kuhakikisha
mamkundi yote ni jumuishi katika uchaguzi mkuu.
Nao Afisa watu wenye ulemavu wilaya ya Wete aliipongeza tume ya uchaguzi, kwa
kushirikiana na wakandi maalumu, katika hatua zake zote za maandalizi ya uchaguzi,
kitu ambacho ni chakipekee kwa mwaka huu.
"Tuipongeze ZEC kwa mwaka huu imechukua
jitihada za makusudi ili kuhakikisha ujumuishi wa makundi yote katika uchaguzi,
kuanzia hatua za awali za uandikishaji, jambo ambalo ni zuri kwetu,’’alifafanua.
MWISHO
Comments
Post a Comment