NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@
MATAIFA kadhaa ulimwengini,
Tanzania ikiwemo zimeridhia mikataba na matamko ya usawa wa kijinsia na
uwezeshaji wanawake kwenye uongozi.
Hii ni kama ilielezwa katika tamko maarufu la la
Haki za Binadamu la mwaka 1948.
Zanzibar imesaini mikataba ya kikanda na
kimataifa, lakini safari ya utekelezaji ni ndefu kwa sababu hadhi sawa
kwa wanawake na wanaunme katika uongoz.
Mara nyingi unapofanyika uteuzi nafasi wanazopewa
wanawake huwa hazina hadhi sawa na zile wanazokabidhiwa wanaume.
Vyama vya siasa navyo vinawaacha nyuma wanawake
katika kuwapa nafasi za kugombea kama, inavofanyika kwa wanaume na jina la
mwanamke likipita huwa kama bahati mbaya.
Taarifa
ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, inafafanua kuwa, kwa uchaguzi wa 2020,
wanaume walioteuliwa na vyama kugombea kuingia katika Baraza la Wawakilishi walikua
190 na walioshinda ni 42 wakati wanawake walikuwa 61 na walioshinda ni
wanane (8).
Taarifa za Shirika la Wanawake la Umoja wa
Mataifa (UN Women) na Umoja wa Mabunge (IPU) za 2017 zimeonesha kuwepo ongezeko
dogo la viongozi wanawake katika serikali na mabunge.
Maana katika majimbo 50 ua uchaguzi ya
Zanzibar, wanawake katika baraza la kutunga sheria, wanane hii ni saw ana asilimia16,
wabunge ni wannne kwa asilimia 8, mawaziri ni sita sawa na asilimia 33 na
Makatibu Wakuu ni saba sawa na asilimia 39.
Kati ya wakuu wa mikoa watano Zanzibar, wanawake
ni wawili, huku wakuu wa wilaya 11, wanawake wakiwa watatu pekee, ambapo na masheha
wanawake ni 81 kati ya 388.
KATIBA/SERA/MATAMKO
Katiba ya Zanzibar ya 1984, kwenye
kifungu cha 11 na cha 14, vimeweka wazi kuwa kila mzanzibari anayo haki na
uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo
yanayomuhusu.
Aidha
Dira ya Zanzibar ya 2050 imeelezea jinsi gani masuala ya usawa wa jinsia juu ya
kuondoa unyanyasaji na kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wanawake.
Sera ya jinsia inaeleza ushiriki wa wanawake
katika vyombo vya utoaji maamuzi, katika ngazi zote ni mdogo na kwa hivyo
serikali, kwa kushirikiana na wadau wengine, itafanya juhudi kuona makundi yote
na yaliyopembezoni.
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika SADC) ambayo mkataba wake ulitiwa saini mwaka 2008 inaeleza,
kutaka kuondoa utafauti na kuwatenga wanawake katika nyanja mbalimbali za
maendeleo na kusaidia kuwepo usawa wa kijinsia katika nchi wanachama na kufikia
asilimia 50/50 kwenye maamuzi.
Makubaliano yanayojulikana kama ‘Itifaki ya
Maputo’ ambayo yalifanyika Msumbiji mwaka 2003, inacho kipengele kinachoonyesha
haki ya wanawake, kushiriki katika siasa na mchakato wa vyombo vya kutoa maamuzi.
Mkataba wa kimataifa wa kutokomeza aina zote
za ubaguzi, (CEDAW) wa mwaka 1979 ambao unapinga aina zote za udhalilishaji na
kusisitiza, ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi.
Ibara 12, inasisitiza ushiriki sawa wanawake na wanaume
kufikia asilimia 50/50 kwenye nyanja za maamuzi, serikalini na taasisi binafsi.
Aidha jukwaa la Mpango wa Utekelezaji wa
Beijing mwaka 1995, ibara ya 7 kinataka ushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa
kuzingatia uwiano wa kijinsia kwenye ngazi zote za uongozi.
VYAMA VYA SIASA
Anaewania nafasi ya uwakilishi wa Jimbo
la Chambani Pemba, Bahati Khamis Kombo, ansema hali sio mbaya kwa viongozi wa
chama chake cha CCM na serikali katika kuteua wanawake kuwa viongozi.
Anasema wanaume waliogombea wakilishi walikuwa
190 na walioshinda 42 na wanawake waliojitokeza walikuwa 61 na walioshinda ni
wanane na kwahivyo haja kwa wanawake kujiandaa vyema kwa uchaguzi zijazo.
Mwakilishi wa Wete Harusi Said Suleiman, anasema
sera ya CCM na katiba yake, zinazingatia jinsia na muda chama kinahamasisha
wanawake kugombea uongozi kwa nafasi mbali mbali.
Mwenyekiti wa mstaafu wa ACT Wazalendo, Juma
Duni Haji, anasema chama hicho kinafuata sheria na mikataba iliyoridhiwa na
kusistiza hakina mfumo dume.
Anasema kinapenda mno kuona wanawake wanashika
nafasi kubwa ndani ya chama, na mfano wa uchaguzi wa 2025, walimteua Fatma Abdull-habibu
Fereji, kuwa Mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano.
‘’Ingawa yalioyotokea mmeyasikia, baada ya
kuenguliwa lakini kama engepata kuendelea mgombea wetu Mpina na kushinda
mwanamke engekuwa Makamu wa rais,’’anasema.
Naibu Mkurugenzi kutoka ADC, Mtumwa Faiz
Sadik, anasema ili kuzipatia ufumbuzi changamoto wanazopitia wanawake, ni lazima kuwepo mipango mizuri ya kutekeleza
mikataba na maazimio ya kimataifa.
Mchakato wa kuwania uongozi kwa uchaguzi wa
mwaka 2025 kwenye majimbo wanawake walihamasika na kufikia takriban 400
kutoka katika vyama vya siasa na hasa CCM, CHADEMA, NCCR
mageuzi, na ACT Wazalendo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar, Abeda Rashid anasema, licha ya
changamoto ziliopo, wanawake wamenufaika na fursa za uongozi ndani na nje ya
vyama vya siasa.
Kwa mara ya kwanza nafasi ya Naibu Katibu Mkuu
wa wizara hiyo kuongozwa na yeye akiwa mwanamke mwenye ulemavu, kama ilivyo kwa
Mhandisi Zena Ahmed Said, kushina nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa
Baraza la Mapinduzi.
TAKWIMU ZA UCHAGUZI 2020 ULIOPITA
Inafahamika kuwa, walioteuliwa na vyama
kugombea ubunge kwa upande wa Zanzibar ni wanaume ni 257 na walioshinda 46
na wanawake walikua 81na walioshinda wanne.
Ujumbe wa baraza la Wawakilishi, walioteuliwa wanaume
190 na walioshinda 42, ambapo wanawake walikuwa 61 na walioshinda ni
wanane.
Upande wa nafasi ya udiwani, ripoti hiyo ya
ZEC inaeleza kuwa, wanaume ni 276 na walioshinda 85 ambapo wanawake walikua 74
na walioshinda ni 25.
NINI ATHARI YAKE
Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi,
anasema kwanza ni kukosa mtetezi, kwenye mausla yanayahusu wanawake, mfano huduma
za mama na mtoto.
Asha Said Suleiman, mgombea uwakilishi Jimbo
la Mtambile kwa tiketi ya ADC, anasema, kuendelea kuwekwa mkiani, kwenye utoaji
maamuzi.
Hidaya Majaka Ali, mwenye ulemavu wa viungo,
anasema kubwa ni kuendelea kuishi kwenye dimbwi la kufanyiwa kila kitu na wanaume,
hata pake pasipohotajika.
NINI KIFANYIKE.
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari
wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali, anasema moja ni waandishi
wa habari, kuendelea kupaza sauti zao.
Mwakilishi msataafu wa Jimbo la Konde anawania
tena nafasi hiyo, Zawadi Amour Nassor, anasema vyama viendelea kuwaamini
wanawake katika uongozi.
Mwanamke aliyegombea Uwakilishi wa Jimbo la
Kojani, Katija Ali Mbarouk, anasema wanaume wafundwe kuwa, majimbo hayana hatimiliki
na wao.
Hata hivyo Dk. Nkya alishauri wanawake
kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa mwaka 203o na sio kusubiri nafasi
za uteuzi au viti maalum.
mwisho

Comments
Post a Comment