NA
HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAGOMBEA
Ubunge na Uwakilishi wa Jimbo la Mtambile kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF,
wamesema kama wakipewa ridhaa, makundi ya vijana, watu wenye ulemavu, wanawake
na wajasiriamali, watanufaika kwa mikopo isiyo na riba, kama njia ya kuwakwamua
na umaskini.
Walisema,
wameshaona wapi wanaotoa mikopo wanakosea, na kuendelea kuyaacha makundi hayo,
wakichukua mikopo ingawa, kisha hurudi tena kwenye hali ngumu ya maisha.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti kwenye kampeni za nyumba kwa nyumba jimboni humo, wamesema njia
pekee ya kuwapa maisha bora makundi hayo, ni kuwachagua wagombea wa CUF na kisha,
kulitekeleza hilo.
Mgombea Ubunge jimboni
humo Rashid Soud Khamis, alisema, ameshaiona njia ya makundi hayo kuondokana na
umaskini wa kipato, ikiwemo ile ya kuwapatia mikopo isiyo na riba.
Alieleza kuwa
vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na wajasiriamali wa Jimbo la Mtambile,
hawaamini kuwa, mikopo yenye riba ni njia ya kufikia ndoto zao, bali wanahitaji
mikipo iliyo salama.
‘’Wananchi wa
Jimbo la Mtambile, ikiwa mnataka kuukimbia umaskini kupitia njia za kujiajiri,
nikopesheni kura niwalipe maendeleo ya kiuchumi,’’alifafanua.
Nae Mgombea Uwakilishi
wa Jimbo hilo Asha Siasa, alisema suala la mikopo yenye heshima na
thamani kubwa, ndio azma yake, pindi akipewa ridhaa.
‘’Kila mmoja anaelewa
kuwa, chama cha CUF kinapenda kutenda haki sawa kwa wote, na ndio pekee, kilicho
na nia thabiti ya kuhakikisha unyonge kwa nchi hii, unaondoka,’’alifafanua.
‘’Kama ngazi ya
urais wa Zanzibar, tulishauokosa kwa sababu za kisheria, sasa kura zenu zihamishieni
kwangu, niwe Mwakilishi wenu, tusaidiane kufikia ndoto zetu.
Aidha Mgombea
huyo wa Ubunge, alisema kama akipata ridhaa hiyo, atakuwa mtetezi mzuri wa maslahi
ya Zanzibar, ili kuhakikisha Muungano unakuwa na manufaa mapana kwa pande zote.
‘’Nikiwa Mbunge wenu,
sitokwenda bungeni kulala na kutia saini pekee, nitayatetea masalahi ya wazanzibari,
maana huo, ndio msimamo wa CUF tokea mwaka 1992,’’alifafanua.
Aidha, aliahidi
kuimarisha huduma ya maji safi na salama, na yawe na manufaa mapana, kwa
wajasiriamali wa mboga mboga, wenye viwanda vya matofali na kilimo chingine.
Katika hatua
nyingine Mgombea Uwakilishi wa Jimbo hilo la Mtambile Asha Siasa, aliwataka
wananchi wa jimbo hilo, kuwatilia kura za ndio, wagombea wote wa chama hicho.
‘’Mwenzangu ni mgombea
Ubunge, mimi Mwakilishi na madiwani wetu, hawa ndio wakombozi wenu kihistoria,
Oktoba 29, mnatakiwa masanduku mkayajaze,’’alifafanua.
Baadhi ya wananchi
waliokuwa wakifuatilia kampeni za wagombea hao wa vijiji vya Kidutani, Majenzi,
Mtuhaliwa, Mtambile, Muwanda na Mizingani, wameahidi kuwapigia kura.
Uchaguzi mkuu wa
mwaka huu, unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, nchini kote, ambapo kwa Zanzibar
ukitanguliwa na kura ya mapema ya Oktoba 28, kwa watu maalum wakiwemo watendaji
wa Tume ya Uchaguzi.
Zanzibar yapo majimbo
50 ya uchaguzi ambapo kwa Pemba, yapo 18,
likiwemo la Mtambile, Mkoani, Kiwani, Chambani, Chonga, Ziwani, Wawi, Ole,
Pandani, Micheweni, Wete, Mtambwe, Konde, Gando, Kojani, Wingwi na mingine.
Mwisho
Comments
Post a Comment