NA MARYAM NASSOR, ZANZIBAR@@@@
MTUHUMIWA wa kesi ya mauwaji, Khalfan Ali Abdallah( 26)
amepandishwa katika kizimba cha mahkama kuu Tunguu Zanzibar ,kwa tuhuma za kuua kwa makusudi
chanzo kikitajwa ni wivu wa mapenzi.
Akisomewa shitaka lake
hilo na Mwendesha mashtka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar, Ali
Amour Makame, mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo.
Mara baada ya
kufika mahakamani hapo, mtuhumiwa huyo akitokea rumande, Mwendesha mashtaka
kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar Ali Amour Makame
Alimueleza, Jaji wa
mahakama kuu Zanzibar kuwa, kesi iyo ipo kwa ajili ya kuanza kutajwa maelezo
ya awali, lakini bado upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kumpa muda
mtuhumiwa kutafuta wakili wa kesi yake.
“Mheshimiwa Jaji leo (jana),
kesi hii ipo kwa ajili ya kutajwa, lakini tunaomba uihairishe na kuipanga
tarehe nyengine, ili kumpa muda
mtuhumiwa kutafuta au kutafutiwa
wakili, kwa ajili ya kumsimamia kesi yake,” alidai.
Baada ya maelezo hayo,
Jaji wa mahakama kuu Zanzibar Ali Mohamed Ali, alimuuliza mtuhumiwa huyo
kuwa yuko tayari kwa ajili ya kuhairishiwa kesi yake hiyo na kujibu ndio.
Kesi hiyo yenye namba 16/2024, kwa mara ya
kwanza ilisomwa mahakamani hapo Juni 3, mwaka huu na kuhairishwa
mpaka Juni 26 mwaka huu, kwa ajili ya kuanza kutajwa tena mahakamani hapo.
Awali ilidaiwa
mahakamani hapo, kuwa mtuhumiwa huyo, anadaiwa kumuua kwa makusudi mke wake wa ndoa kwa sababu ya wivu wa mapenzi.
Mtuhumiwa huyo, alitenda
kosa hilo, Bwejuu mkoa wa kusini Unguja, majira ya saa 4:00 usiku.
Hilo
ni kosa kinyume na kifungu cha 179 na 180 chini
ya kifungu namba 6 cha mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Jaji huyo, aliutaka
upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa shauri hilo, ili kesi
hiyo ianze kusikilizwa, na kuihairisha Juni 26 mwaka huu, kwa ajili ya
kusikilizwa maelezo ya awali na mtuhumiwa kurejesha rumande.
MWISHO
Comments
Post a Comment