NA NIHIFADHI ABDULLA, ZANZIBAR@@@@
“SIKUJUA kinachoendela nilimuona tu baba kavimba
nikamsalimia hakutikia vizuri mimi nikaingia ndani kukoga na mambo mengine”
Amesimulia Wafaa akiwa kwenye upenu wa Nyumba na kuwacha
kumlisha mtoto kwa muda wa sekunde 5 huku akionesha huzuni usoni mwake.
Jina lake halisi Wafaa Makame Hassan miaka 26
anakumbuka yaliyomtokea na namna alivyokatishwa ndoto za kuwa mwanamichezo
miaka 12 iliyopita wakati anasoma skuli ya Muyuni iliyopo Wilaya ya Kusini Mkoa
wa Kusini Unguja.
Amesema alikuwa na ndoto za kuwa mchezaji mkubwa wa
mpira wa Nyavu (Net Ball) na tayari alishaanza mashindano ya Skuli
kwa skuli ya Elimu bila ya malipo.
Ameendelea kusema baada ya kupumzika alipata habari
kutoka kwa Shangazi yake ambae kwa sasa ameshatangulia mbele ya haki kwamba baba yake kapiga marufuku kwenda
kwenye michezo kwa madai kufanyika
uhuni.
“Kuna mtu kampigia simu baba yako kuwa mnachanganyika
na wanaume na kushikana hivyo amekasirika na lazima ukubaliane nae” alielezea
Wafaa akimnukuu shangazi yake.
Wafaa amesema siku hiyo ilikuwa nzito kwake kwani
hakutarajia kukutana na hali hiyo na
mwisho wa siku akukubaliana mzazi wake
na hivyo ndoto zake zikaishia hapo.
“Sikuwa na furaha nilikasirika sana nikaingia ndani
karibia siku nzima niliwanunia watu wote
wa nyumbani lakini mwishowe nikawa sawa nitakasirika mpaka lini anabaki kuwa
mzazi wangu tu na zile ndoto zikafikia tamati siku ile”
Juma Hassan baba mdogo na mlezi wa Wafaa amesema
ameamua kumkataza kushiriki michezo kutokana na lawama na maneno ya watu
wengine kwa kuambiwa wanafanya uhuni.
“Najua kama lile jambo halikumfurahisha mwanangu
lakini sifa ya mtoto wa kike ni kujiheshimu na kujilinda kwenye michezo yao ilo
halikuwepo na ndio maana nikapewa salamu ili nimchunge na mimi sikuona vibaya
kwani mtoto halelewi na mmoja,
“Wafaa ni mtoto wa marehemu kaka yangu aliniachia
akiwa mdogo na kusisitiza nimlee kwa misingi mizuri angeharibika huko michezoni
mm ningekuwa mgeni wa nani nikaona la maana asiende michozoni na sio yeye tu
hata wanangu wengine wakike hatoenda
kule hakuna maadili
Salama ali haji mama mzazi wa Wafaa amesema kiupande
wake haoni tatizo mtoto wa kike kushiriki michezo kwani anaona wanawake
mbalimbali ambao wameajiriwa kupitia sekta hiyo na wanaendesha Maisha yao bila
tabu.
“Mimi sikusikilizwa na wala sikufurahi lakini mtoto
akiwa ulezini mzazi huna kauli, dada ake alikuwa anashiriki michezo skuli kutwa
hakai nyumbani na siku mzuia mpaka kachoka mwenyewe kwasababu sikuona tatizo
kuna wanawake wangapi wameajiriwa kwa michezo hayo ndo maendeleo yenyewe”
alimalizia Bi Salama.
Wafaa kwa sasa ni mke na mama wa watoto wawili amesema
baada ya kusitishwa kushiriki michezo hata nguvu ya kusoma masomo mengine nayo
ikayeyuka “baada ya hapo maendeleo yangu ya kusoma yakapungua na kusababisha
kidato cha nne kufanya vibaya kwenye mtihani wangu wa Taifa na hivyo nikaolewa na sasa nalea wanangu”
alimalizia Wafaa huku akimnywesha mwanawe maji.
Taasisi ya wanawake kwenye michezo nchini marekani (womens sport
foundation inaonesha kwamba wasichana ambao wana umri wa miaka 14 huacha
kuendelea na michezo ikiwa tofauti na wavulana wenye umri huohuo
Kwa hapa Zanzibar moja ya vikwazo hivyo ni wazazi
kutowaruhusu watoto wao kwa madai ni kinyume na maadili silka na utamaduni
Kutokana na
changamoto hizo lukuki zilizopo
zinazomkwamisha mwanamkke na msichana kufikia ndoto zake za kimichezo jitihada mbalimbali
zinachukuliwa kuhakikisha linapatiwa ufumbuzi na kuona kiwango cha wanawake
kwenye sekta hiyo kinaongezeka
Afisa mradi wa
kukuza usawa wa kijinsia na ujumuishi kwenye michezo Khairat Haji
amesema Chama cha Waandishi wa habari Wanawake TAMWA Zanzibar
kimeona haja ya kushirikiana Waandishi wa habari juu ya kuandika masuala ya
michezo kwa wanawake na wasichana ili iwe rahisi kufikisha ujumbe kwa jamii
kuondoa mifume dume ambayo ni vikwazo dhidi yao.
“Kwenye mradi huu tunafanyakazi na waandishi wao
wanauwezo wa kuibua changamoto, vikwazo lakini pia kuonesha wale wanawake
waliofanikiwa kwenye michezo ambao watakuwa kielelezo kwenye jamii na mfano
bora wa kuigwa
Mradi huo
unatekelezwa na shirika la maendeleo la
ujerumani GIZ, Chama cha waandishi wa
habari wanawake TAMWA ZANZIBAR kwa
kushirikiana na Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA na kituo
cha majadiliano kwa Vijana (CYD)
lengo ikiwa ni kuipa elimu jamii ya kuwaunga mkono wanawake katika
kushiriki michezo kwa maendeleo.
Comments
Post a Comment