ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@
WANAFUNZI wa skuli ya msingi ya Mtangani na
wenzao wa skuli ya sekondari ya Mauwani, wilaya ya Mkoani Pemba, wametakiwa
kushiriki kikamilifu katika kupanda miti na kuyatunza mazingira, ili
kuendeleza urithi wa kijani katika visiwa vya Zanzibar.
Hayo yameelezwa Juni 4, 2024 na Mjumbe wa Baraza kuu
Taifa la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapindizi ‘UVCCM’ anaeshughulikia mkoa wa
kusini Pemba, Amriya Seif Saleh, wakti alipokua akishiriki katika zoezi la
upandaji miti, eneo la Mtangani na Mauwani, ikiwa ni kuelekea kilele cha
maadhimisho ya siku ya mazingira duniani.
Alisema kuwa, ipohaja kwa walimu kujitahidi
katika suala la kuwaelimisha wanafunzi, juu ya umuhimu wakupanda miti,
ili kuyahifadhi na kuyatunza mazingira yao na taifa kwa ujumla.
"Niwaombe walimu, mujitahidi sana kuwapa elimu
wanafunzi hawa, ili wajue nini lengo hasa la upandaji wa miti na
kuhifadhi mazingira, waweze kunufaika katika maisha yao ya kila siku",alieleza.
Hata hivyo, aliwaomba wanafunzi hao, kusoma
kwabidii na kuepuka vishawishi mbalimbali, ambavyo vitawaharibia yale malengo
yao, ambayo wamejiwekea.
Nao walimu wakuu wa Skuli hizo, wameushukuru
uongozi wa UVCCM mkoa wa kusini Pemba, kwa kuwajali na kuwathamini, hivyo
wameahid kuendeleza kuitunza miti hiyo, kwani kilikua nikilio chao cha muda
mrefu, ingawa kwa imepata ufumbuzi.
Hivyo walieleza kua, ndani ya skuli hizo
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama, na kuiomba
Serikali, kupatiwa huduma hiyo, ili wanafunzi wanufaike vizuri na nakuendelea
na masomo yao bila ya usumbufu.
Kwa upande wake Mjumbe wa UVCCM taifa kupitia vyuo vikuu Iddi William Ayubu, alisema kua, lengo la kupanda miti hiyo, ni kuweza kupatikana hewa nzuri na kuzuiya mmong’onyoko wa ardhi, ambao utasababisha kuwa na mazingira hatarishi.
Nae mwanafunzi wa skuli ya sekondari Mauwani
Yahaya Salim Omar alieleza kuwa, wamefurahishwa na Umoja huo wa vijana wa CCM, kwa
kuwajali na kuwathamani kushiriki katika zoei la upandaji miti.
Katika zoei hilo, miti 1,000 ambayo ili pandwa
ndani ya skuli za Mtangani na Mauwani, ni sehemu ay shamra shamra za maadhimisho
ya siku ya mazingira duniani, inayoadhimishwa kila ifikapo Juni 5, ya kila mwaka.
MWISHO.
Comments
Post a Comment