NA HASINA KHAMIS,
OUT- PEMBA@@@@
AFISA Mdhamini wa
Wizara ya Fedha na Mipango Pemba Abdull-wahbi Said Abuu-bakar, amesema
usimamizi bora wa mali za umma itasadia kwa serikali, kufikia malengo
yaliyokusudia.
Aliyasema hayo leo Juni 6, 2024 katika kikao cha kupokea maoni ya wadau, kwa muongozo wa uondoaji wa mali za umma
na usimamizi, udhibiti wa matumizi ya vyombo vya moto vya serikali, ukumbi wa wizara
hiyo Gombani Chake chake Pemba.
Alisema changamoto
zilizopo katika wizara, taasisi za umma na mashirika, ni kushidwa kusimamia
kutunza na kutumia vyema mali za umma kama sheria inavyotaka.
"Hatufanyi
vyema katika kusimamia mali za umma, ambapo inasababisha kushidwa kufikia lengo
la mali hizo, jambo ambalo sio sahihi,’’alieleza Afisa Mdhamini huyo.
Aidha aliwataka
washiriki hao kutoka mashirika ya umma na taasisi za serikali, kutoa
ushirikiano na ofisi ya usajili wa hazina, pamoja na kutumia fursa hiyo kwa
kutoa elimu na maoni kwa jamii.
Nae Msajili wa Hazina
Zanzibar, Wahdi Mohamed Ibrahim, alisema sheria nambari 6 ya mwaka 2021 ya
usajili wa hazina, imewataka kutoa muongoza kama inavyoelekeza.
Alisema, upo
umuhimu kwa sasa mambo ya serikali kuwa wazi kwa yale yanayostahiki, ili umma ufahamu
utaratibu wa jinsi mali ya umma inavyoingia mpaka inapotoka.
"Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, inatumia fedha nyingi kwenye manunuzi kutumia muongozo
wa usimamizi na udhibiti wa matumizi ya vyombo vya moto, na uondoaji wa mali za
umma utaweza kupunguza gharama hizo na utitiri wa mali chakavu,"
alifafanua.
Kwa upande wa
washiriki, akiwemo Amina Ali Mohamed, Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili
na Mifugo, alisema rasimu hiyo ya muongozo wa uondoaji wa Mali za umma, ni
jambo muhimu ambapo serikali ameamua kulifanya kupitia ofisi ya usajili wa
hazina.
‘’Awali kila ofisi
ilikuwa na utaratibu wao, lakini kupitia muongozo huu utaweza kudhibiti katika
ngazi ya utumiaji, utunzaji mali na iwapo itakuwa chakavu, pia utaratibu
utakuwemo na ikibidi kuuzwa basi pato la serikali litapatikana,’’alieleza.
Nae Said Shaame
Bakari, kutoka Wizara ya Biashara, alisema mafunzo hayo yataweza kusaidia
kupata uelewa wa pamoja, kwa taasisi zote na kufuata mfumo mmoja.
Kikao hicho cha
siku moja, chenye moja ya lengo la kupunguza changamoto katika usimamizi wa
mali za umma, ambapo miongozo miwili imetolewa, na kuwasilishwa na
kusubiri kupokea maoni ya wadua.
MWISHO
Comments
Post a Comment