Skip to main content

Posts

USHIRIKA ENEO LILILOPUNGUZA FOLENI YA AJIRA SERIKALINI WANAWAKE, VIJANA WAVAMIA SEKTA HIYO

  NA MARYAM SALUM, PEMBA::: WALIOSEMA ‘umoja ni nguvu utengano ni udhaifu’ wala hawakukosea.   Waliaamini kuwa, watu wanapofanyakazi kwa pamoja, maendeleo na ushindi kwa kweli hupatikana. Sheria namba 15 ya mwaka 2018 iliundwa kwa ajili ya kuipa nguvu   sekta ya ushirika, ili iweze kuimarika zaidi   kwa nia ya kuwafanya wananchi wapate ajira na kipato.      HISTORIA YA VYAMA VYA USHIRIKA Sekta ya ushirika iliasisiwa hapa Zanzibar tokea miaka ya 1923 hadi mwaka 1925, ingawaje haikupewa kipaumbele kikubwa kwa wakati huo, kutokana na ukosefu wa sera makini. Ambapo kwa wakati huo, jamii haikuwa ikiona manufaa kwa kuwepo kwa sekta hiyo, hali iliyotajwa kupana foleni ya ajira kubwa serikalini.                         HALI YA SASA Miaka ya hivi karibuni sekta hiyo, imepewa mkazo mkubwa na kujengewa mazingira na kuundiwa sera...

MAZIWA YA MAMA LULU YA KIPEKEE KWA MTOTO

      HABIBA ZARALI, PEMBA: KILA mwanzoni mwa wiki ya mwezi wa Agosti, ya kila mwaka, dunia huwa na wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama.   Lengo la wiki hii, huwa ni kusisitiza umuhimu wa maziwa ya mama kwa watoto wachanga na wadogo, kiafya.   Afya ni kitu muhimu katika maisha ya mwanadamu na kinyume chake, ni kuzalisha maradhi kadhaa yanayodhoofisha mwili na kiakili.   Katika kuhakikisha afya ya mwanadamu inaimarika, msingi wake huanzia tokea mtoto anapokuwa tumboni na mara anapozaliwa, kwa kuhakikisha anapewa mahitaji ya msingi ikiwemo maziwa ya mama.   Maziwa ya mama yana kinga kamili ikiwemo ya vitameni A vya kutosha ambavyo huwa ni kinga ya maradhi mbalimbali kwa mtoto mchanga.   Ingawa wapo baadhi ya akina mama hawapendi kunyonyesha na huamuwa kumuachisha ziwa mtoto mara tu, anapojifunguwa, kwa sababu tofauti ikiwemo kuhofia maziwa yake kuanguka, kupoteza haiba na muonekano wake.   Katika hatuwa ya kumli...

VIJANA WALIVYOPIGA HATUA KIMAENDELEO, SERIKALI YAWAPIGA MBELEKO

  NA HANIFA SALIM, PEMBA:: ‘ ’KIJANA ni mtu yeyote mwenye umri wa miaka 15 hadi miaka 35,’’ndivyo sera na sheria ya vijana Zanzibar inavyofafanua. Lakini kwa upande mwengine kijana ametafsiriwa kuwa ni mwanamke au mwanamme yeyote mwenye miaka katia ya 15 hadi 24, kama sera ya taifa ya Maendeleo na vijana ya mwaka 1996, na kama ilivyorekebishwa mwaka 2007.   K ijana ni mtu muhimu kwa taifa lolote ulimwenguni, kwani ndio nguvu kazi ya taifa, ndio taifa la kesho kama wasemavyo baadhi yao. Lakini kijana ndio tumaini la taifa na ndio mtu anayetazamiwa kwa mapana ya nchi, katika kuongoza, kukuza uchumi na kuzima majaribio ya kihalifu. Vijana wanakumbana na changamoto mbali mbali katika maisha yao, na mwisho wa siku taifa linamchukulia kama mtu aliyeshindwa na asiye na msaada wowote kwa taifa lake. Lakini katika umri huo wa ujana, inampasa kijana kujitambua ili aweze kuwa na muonekano halisi, sio kwa umri tu bali matendo zaidi. Ni lazima awe na ushawishi katika masual...