NA HAJI NASSOR, PEMBA MAHAKAMA kuu Zanzibar kanda ya Pemba, imempeleka chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 30, mshitakiwa Farid Abdalla Omar mika (35) wa Chambani wilaya ya Mkoani, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili, likiwemo la kumlawiti mtoto wa miaka 6. Jaji Mahakama hiyo Ibrahim Mzee Ibrahim, alilipokea jalada la kesi hiyo, likitokea mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, kwa ajili ya kupangiwa hukumu. Kesi hiyo awali ilianzia kwenye mahakama hiyo na kuanza kusikilizwa mashahidi wa pande zote mbili, na baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani, jalada la kesi yake, lilifikishwa mahakama kuu kwa ajili ya kupangiwa hukumu. Hayo yalifanyikwa, kwa vile kosa la mshtakiwa huyo linaanzia miaka isiyopungua 30 ama kifungo cha maisha, ambapo mahakama ya Mkoa, haina uwezo huo kisheria. Ndipo wiki iliyopita, jalada hilo lilifikishwa mikononi mwa Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim wa Mahakama kuu, na kuamza kulipitia kwa umakini, hadi ilipofika Novemba 21, mwa...