NA
HAJI NASSOR, PEMBA:::
SHAHIDI
nambari nne, Said Massoud ambae ni jirani wa mtuhumiwa wa ubakaji, Khamis Juma
Chumu ‘soda’ (76) mkaazi wa Mtoni,
amesema, mzee huyo hahusiki na tuhuma za ubakaji, kama zilivyowasilishwa
mahakamani hapo.
Alidai kuwa, mzee ‘soda’ ana mfahamu vyema, kwa ujirani na
ni mkarimu mno, hivyo amekuwa akizungumza na kila mmoja, na shauri lililopo
mahakamani, ni la kupangwa, ili kumachafua.
Shahidi huyo alidai kuwa,
amekuwa nae karibu mno mzee ‘soda’ na hata siku ya tukio alikuwa hayupo
kisiwani Pemba, na sio kweli kuwa, alikimbia baada ya kuwepo kwa tuhuma hizo.
Aliendelea kudai kuwa, mtoto
aliyedai kubakwa na mzee ‘soda’
hamfahamu jina lake wala apoishi, na anayemjua yeye ni mzee huyo pekee.
‘’Mheshimiwa Hakimu, mzee huyi
ni mtu wangu na karibu, kila mmoja mtaani anamuheshimu, sasa leo nikisikia
amebaka nishangaa sana’’,alidai shahidi huyo.
Kabla ya shahidi huyo kutoa
ushahidi wake, akiongozwa na wake wa utetezi Abeid Mussa Omar, Hakimu wa
mahakama hiyo Muumini Ali Juma, alimtaka shahidi huyo kusema ukweli.
Hakimu alimueleza shahidi
kuwa, mahakama inamtegemea yeye kuisaidia, maana hadi kufikishwa mahakamani
hapo, itakuwa anaelewa vyema tukio hilo.
‘’Sisi tunakusikiliza wewe,
ukisema uongo utaipotosha mahakama na ukisema ukweli utaisaidia, katika kufikia
haki, na vyenginevyo jukumu hili utalibeba wewe,’’alieleza.
Hata hivyo, Hakimu huyo alimtaka
shahidi huyo, kutoa ushahidi wake kwa njia ya kiapo, na huku akijua kuna
madhara ya kusema uongo, mahakamani hapo.
‘’Ukisema uongo shauri yako,
hapa duniani tunapita tu, sisi tunajivua na ukweli unao wewe na ndio maana
upande wa utetezi umekuleta kutoa ushahidi wako,’’alifafanua Hakimu.
Awali Wakili wa serikali Ali
Amour Makame, alidai kuwa shauri hilo lipo mahakamani hapo kwa hatua ya utetezi,
na wako tayari kuusikiliza.
Hivyo baada ya ushahidi huo,
wakili wa utetezi alimueleza Hakimu Muumini kuwa, ameshafunga ushahidi wao, na
kuiachia mahakama iendelee na taratibu zake.
Hivyo, hakimu huyo
aliliahirisha shauri hilo hadi Novemba
28, mwaka huu, kwa ajili ya kusomewa hukumu yake mtuhumiwa huyo, baada ya
kila pande Novemba 14, mwaka huu kufunga ushahidi.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa
huyo Khamis Juma Chumu ‘soda’ (76) mkaazi wa Mtoni wilaya ya
Chake chake, alidaiwa kumtorosha mtoto wa kike miaka 13, wakati akienda kuchota
maji mferejini, na kumpeleka nyumbani kwake.
Kufanya hivyo ni kosa,
kinyume na kifungu 113 (1) (a) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018,
sheria ya Zanzibar.
Kosa la pili ni la ubakaji, ambalo
anadaiwa kulifanya Mei 15, mwaka huu, ambapo anadaiwa kumbaka mtoto huyo majira
ya saa 4:15 asubuhi, eneo la Mtoni wilaya ya Chake chake.
Kufanya hivyo ni kinyume, na
kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6
ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment