Skip to main content

'ZRA' YAFANYA MABADILIKO SHERIA ZA KODI KUONGEZA UFANISI

 


NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

MAMLAKA ya Mapato Zanzibar 'ZRA' imesma, imezifanyia mabadiliko  sheria saba  za kodi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, yanalenga kuleta ufanisi katika makusanyo na kuwapa ahuweni wananchi.

Hayo yameelezwa leo August 28, 2026  na Mkuu wa Kitengo cha Habari Makame Khamis Mohamed  wakati akiwailisha mabadiliko ya sheria hizo kwa wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kisiwani Pemba, katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka hiyo Gombani Chake chake Pemba.

Alisema kua mabadiliko hayo, yanalenga kuleta ufanisi kwa mlipa kodi na serikali, kwani yamezingatia kupunguza kasoro mbalimbali, zinazojitokeza pande zote mbili wakati wa kulipa na kukusanya kodi hizo.

Alieleza kua mabadiliko ya sheria hizo pia yamezingatia mabadiliko na mwenendo wa sayansi na teknolojia,  pamoja na kuzingatia unafuu kwa walipakodi na kuongeza mapato kwa serikali kuu.

"Sababu ya madiliko ya sheria mbalimbali za kodi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ni kuongeza ufanisi zaidi katika ukusanyaji na ulipaji wa kodi, kwa kuondoa vikwazo vilivyokuwepo, kasi ya sayansi na teknolojia, kuleta unafuu kwa walipakodi na kuongeza mapato ya serikali" alieleza.


Akizungumzia sheria zilizofanyiwa mabadiliko, alisema ni pamoja na Sheria ya Kodi  ya  Ongezeko la Thamani, inaeleza kuondoshwa kwa kodi,  ambayo kwa sasa inatoa fursa kwa wawekezaji wa viwanda vidogo na vya kati, ambao hawajasajiliwa ZIPA, hawatolipa kodi ya 'VAT' katika uingizaji wa malighafi.

Alisema sheria nyengine iliofanyiwa mabadiliko ni sheria ya Fedha ya Kodi za  Miundombinu, ambapo marekebisho yake yanaruhusu uingizaji  wa vifaa saidizi vya watu  wenye mahitaji maalum, kutotozwa kodi ya miundombinu, jambo litakalosaidia ustawi wao.

Alieleza vifaa hivyo ni pamoja na viti mwendo, viungo bandia, visaidizi vya kuona na kusomea, fimbo nyeupe na mashine za kutolea hati nundu, na vyoo vinavyotumiwa na watu wenye ulemavu.

Alieleza sheria ya tatu iliofanyiwa mabadiliko, ni sheria ya Ushuru wa  Stempu, ambapo kwa sasa hati ya usajili kwa wafanyabiashara wanaolipa ushuru wa Stempu itamaliza muda wake ifikapo miezi 12 baada ya tarehe ya kutolewa. 


Aidha alieleza sheria hii, imekuja kupunguza kiwango cha ushuru wa stempu kwa asilimia 25,  kwa gari za biashara, jambo litakalorahisisha utoaji huduma bora kwa wananchi.

Alifafanua kuwa, sheria nyengine iliofanyiwa mabadiliko ni Sheria ya Ada za Bandari, ambayo inaeleza ada ya huduma za bandari, kwa wageni wanaosafiri ndani ya  Zanzibar (Pemba/ Unguja) na kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara imeongezwa  kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara dola 2 hadi  dola 3; na kutoka Unguja kwenda Pemba dola moja hadi mbili 2.

Mkuu huyo wa Kitengo cha Habari, kutoka ZRA alifahamisha sheria nyengine iliofanyiwa mabadiliko ni sheria ya  Ushuru wa  Bidhaa kinachoeleza, uingizaji wa bidhaa kutoka Tanzania Bara, hazitotozwa kiwango cha ushuru wa bidhaa, ikiwa zitahamishiwa kwa matumizi ya Zanzibar, ikiwa kiwango cha ushuru wake ni sawa au kikubwa kama kiwango cha Zanzibar.

Inaeleza , ikiwa ushuru wa bidhaa unaotumika Zanzibar ni mkubwa kuliko Tanzania Bara, tofauti ya ushuru huo itachukuliwa kuwa haijalipwa na itakusanywa Zanzibar wakati wa kuingizwa bidhaa hiyo Zanzibar.

Sheria hii inaeleza Ushuru wa bidhaa kwa kampuni zinazorusha matangazo ya Televisheni (Cable Television Company) umeongezwa na kuwa Asilimia saba (7%)  pamoja na kutoza Ushuru wa Bidhaa kwa kiwango cha asilimia kumi (10%) kwenye tiketi za kiingilio katika Viwanja vya Michezo, Kumbi za Starehe na Maeneo ya Burudani.

Sheria nyengine iliofanyiwa mabadiliko ni sheria ya Usimamizi wa Kodi, ambapo kwa sasa  cheti cha usajili wa mlipakodi, kitapaswa kuoneshwa hata kwa njia ya kidijitali, katika eneo la biashara.

''Sheria hii imeainisha kua adhabu ya faini kwa  mlipakodi atakeshindwa kutoa risiti ya kielektroniki imeanzia kiasi kisichopungua shilingi 200,000 na kisichozidi shilingi milioni 2.

Aidha imeainisha mlipakodi aliyekuwa nje ya Zanzibar anaweza kuomba kuongezewa muda wa kulipakodi kwa maandishi kwa Kamishna. Baada ya kiogozi huyo, kujiridhisha kwa sababu za kutokuwepo kwake Zanzibar, au maradhi au sababu nyingine za msingi.



Imeainisha kua ugomboaji wa deni kwa njia ya mtu wa tatu kupitia matumizi ya kadi za malipo za kielektroniki kutoka kwa watoa huduma za malipo ya kielektroniki.

Akizungumzia kuhusu makiso ya makusanyo yao, Makame alissema , kua 'ZRA' kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imekadiria kukusanya shillingi Tirrion 1.726 kupitia vyanzo mbalimbali vya makusanyo, hivyo amesisitiza wananchi kulipakodi kwa hiari ili kufanikisha hilo.


Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari walishiriki mafunzo hayo Mkurugenzi uratibu shirika la Magazeti ya serikali Pemba Haji Nassor Mohamed aliipongeza ZRA kwa kuwaogezea maarifa waandishi juu ya sheria mbali mbali za kodi huku akiwasihi kuendeleza utaratibu huo.


 

                                          MWISHO

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...