NA HAJI NASSOR, PEMBA
MAHAKAMA kuu Zanzibar kanda ya Pemba,
imempeleka chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 30, mshitakiwa Farid Abdalla Omar
mika (35) wa Chambani wilaya ya Mkoani, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa
mawili, likiwemo la kumlawiti mtoto wa miaka 6.
Jaji
Mahakama hiyo Ibrahim Mzee Ibrahim, alilipokea jalada la kesi hiyo, likitokea
mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, kwa ajili ya
kupangiwa hukumu.
Kesi hiyo
awali ilianzia kwenye mahakama hiyo na kuanza kusikilizwa mashahidi wa pande
zote mbili, na baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani, jalada la kesi yake, lilifikishwa
mahakama kuu kwa ajili ya kupangiwa hukumu.
Hayo
yalifanyikwa, kwa vile kosa la mshtakiwa huyo linaanzia miaka isiyopungua 30
ama kifungo cha maisha, ambapo mahakama ya Mkoa, haina uwezo huo kisheria.
Ndipo wiki
iliyopita, jalada hilo lilifikishwa mikononi mwa Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim wa
Mahakama kuu, na kuamza kulipitia kwa umakini, hadi ilipofika Novemba 21, mwaka
huu, akamua kumsomea hukumu.
‘’Mshitakiwa
kutokana na kutiwa hatiani kwa kosa la kwanza la kutorosha, mahakama hii kuu
inakupa miaka 10, na kosa la pili la kulawiti nalo utatumikia miaka 20 chuo cha
mafunzo, ‘’alisema Jaji Ibrahim.
Aidha Jaji
huyo akisoma hukumu hiyo, mbele ya waendesha mashtaka wa serikali Seif Mohamed
Khamis na Asiya Ibrahim, alisema kifungo hicho cha mshitakiwa huyo, cha miaka
30 kitakwenda sambamba.
‘‘Mshtakiwa,
ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashataka, ulitosha wewe kukutia
hatiani maana haukuacha chembe ya shaka, kuanzia wa mtoto mwenyewe hadi
mpelelezi,’’alisema Jaji huyo.
Kabla ya
kusoma kwa hukumu hiyo, mawakili hao wa serikali, waliiomba mahakama hiyo kuu,
kutoa dhabu kwali kwa mshitakiwa, ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia
kama hiyo.
Kosa la
kumtorosha mtoto huyo, ilithibiti kuwa alilitenda April 30, mwaka huu majira ya
saa 9:30 jioni, eneo la Tumbini Chambani wilaya ya Mkoani, kwa kumtorosha mtoto
huyo kutoka nyumbani kwao, na kumpeleka nyuma ya hospitali ya Tumbini.
Kosa la pili,
ni kumlawiti mtoto huyo siku hiyo hiyo majira ya saa 9:35 jioni, ambapo ni kosa
kinyume na kifungu cha 115 (1) sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment