Skip to main content

MRADI MKAKATI UJENZI WA MATANGI YA KUHIFADHIA MAJI PEMBA, NI NJIA YA KUJIKWAMUA NA KIPATO

 



NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

MAJI ni rasilimali muhimu kwa maisha ya viumbe wote wanaoishi.

Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii lita trillion 11 hadi 12.5 za maji, hutumika kwa siku duniani kote.

Itambulike maendeleo yote duniani, hutegemea upatikanaji huduma muhimu za kijamii, ikiwemo maji safi na salama.

Mitandao ya kijamii imeripoti sekta ya kilimo pekee inachukua karibu lita trillion 8.0 za maji kwa siku, ikifuatwa na ya viwanda inayokisiwa kutumia lita trillion 2.3, huku matumizi ya nyumbani yakikisiwa kuchukua lita trillion 1.2 duniani kote.

Ndio maana, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huchukua juhudi za makusudi, kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama, kila siku.

Miongoni mwa juhudi hizo ni utekelezaji mradi wa kimkakati, wa ujenzi wa matangi makubwa ya kuhifadhia maji, katika maeneo ya mikoa miwili ya kisiwa cha Pemba.

Ofisa Mdhamini Ofisi ya Rais Pemba Shuweikha Abdallah Omar anasema, mbali na kusogeza huduma ya maji kwa wananchi, mradi huo unalenga kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

“Mradi huu ni miongoni mwa juhudi za kuifungua Pemba kiuchumi, pamoja na matumizi ya kawaida huduma ya maji ni kipengele muhimu, katika uwekezaji wa miradi ya maendeleo,” anaeleza.

Hivyo serikali ya awamu ya nane, chini ya Dk. Hussein Ali Mwinyi, imeweka nguvu kubwa katika ujenzi wa matangi makubwa ya maji, ilioamini yatasaidia kutatua changamoto ya upatikanji huduma hii.

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI

Hapa Ofisa Mdhamini wizara ya Maji, Nishati na Madini Pemba Mhandisi Suleiman Hamad Omar anasema,  mwaka wa fedha wa 2025/2026, wizara imejenga matangi manne makubwa ya maji (zinkAlminium) yenye uwezo wa kuhuifadhi maji mengi.

Anaeleza kila tangi lina uwezo wa kuhifadhi lita milioni 1, za maji kwa wakati mmoja, hatua inayofanya mradi huo kuwa miongoni mwa mradi mkubwa wa miundombinu ya maji kisiwani Pemba.

Mhandisi Suleiman anasema, serikali haikukurupuka bali ilifanya utafiti wa kina, kabla ya kuanza ujenzi wa mradi huo.

“Matangi haya yamejengwa kwa vigezo vya kimataifa, yakiwa na uwezo wa kuhimili mabadiliko yoyote ya hali ya hewa, kwa kipindi kisichopungua miaka 10, bila kufanyiwa matengenezo makubwa,” anafafanua.

Anasisitiza ubora huu ni kuhakikisha fedha za walipa kodi zimetumika kwa njia endelevu, na yenye tija ya muda mrefu, huku ujenzi huo ukizingatia maeneo yenye uhitaji mkubwa wa huduma.

Anafafanua kuwa, mkoa wa kaskazini Pemba, Matangi mawili yamejengwa katika shehia za Mtambwe Kaskazini na Mtambwe Kusini.

Ambapo tangi la Mtambwe Kaskazini, linatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 12,000, huku lile la Mtambwe Kusini, likitarajiwa kuwahudumia zaidi ya wananchi 10,000.

Na Matangi mawili yaliobakia  yamejengwa katika meneo ya Kengeja wilaya ya Mkoani na kwa upande wa wilaya ya Wete lipo kijiji cha Raha.

Ujenzi huu unalenga kusawazisha huduma pande zote za kisiwa, ili kusiwe na eneo linalobaki nyuma, na ujenzi wa matangi haya umepangiwa shilingi zaidi ya billion 15.77.

“Mradi huu unatekelezwa na serikali ya awamu ya nane, inayoongozwa na Dk. Mwinyi, unalenga kuhakikisha upatikanaji maji katika maeneo yote, hadi kukamilika kwake utagharimu shilling billion 15.77,’’anaeleza.

Kubwa, akawataka wananchi, kuyatumia maji hayo, kwanza kwa kukuza pato lao, kwani ndio miongoni mwa azma ya Dk. Mwinyi.

Hakuacha kuwakumbusha wananchi, kwamba ulinzi wa miundombinu yake, wa kwanza ni wananchi wa maeneo husika, wakiongozwa na weingine.

UIMARISHAJI VYANZO VYA ASILI NA MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI

Ujenzi wa matangi makubwa hauna maana, ikiwa hakuna vyanzo vya uhakika vya kujaza maji hayo.

Mhandisi Suleiman anabainisha kuwa, sambamba na ujenzi wa matangi, serikali imeweka nguvu kubwa katika kuboresha na kuongeza vyanzo vya asili vya maji, ikiwa ni pamoja na kuchimba na kukarabati visima.

Maana anasema, lengo ni kuhakikisha matangi yanapokea maji ya kutosha na kwa muendelezo bila kukatika katika, kama ilivyo hapo zamani.

Jitihada hazikuishia hapo, kwani wizara pia, inafanya ukaguzi wa kina wa mfumo mzima wa usambazaji wa nuduma ya maji uliopo.

"Tumeimarisha vyanzo vya maji na tunapitia upya miundombinu iliopo, ili kujiridhisha kwamba itafaa au kuna uhitaji wa kubadilisha,” anaeleza.

Haya yote yanalenga kuhakikisha udhibiti wa maji hayo ili yawafikie wananchi yakiwa safi, salama na mengi pale yatakapoanza rasmi matangi, kutumika.

Kazi hii ya kutathmini upya mabomba na miundombinu ya zamani, itahakikisha maji yanayotoka kwenye matangi hayo mapya, yanawafikia wananchi bila ya vikwazo.

JINSI WANANCHI WATAKAVYO FAIDIKA

Mradi huo upo katika hatua za kutumika, huku matunda yake yakitarajiwa kuwafaidisha wananchi wengi.

Mwanaid Juma Khamis wa Mtabwe kusini wilaya ya Wete anasema, ile tabu ya kutembea umbali mrefu na kutumia saa nyingi kutafuta maji, inaenda kumalizika.

Bakar Said Bakkar wa Mtambwe Kaskazini, anamatarajio  kua. mradi huo utafungua milango mipya ya fursa za kiuchumi, hususan katika sekta ya kilimo.

“Mbali na matumizi ya kawaida, mradi huu utakuza sekta ya kilimo cha umwagiliaji, ambayo kwa takriban miaka miaka minne iliyopita, ilikwama kutokana na tabu ya maji,” anaeleza.

Akikagua mradi wa ulazaji mabomba ya Maji Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah, alisisitiza kuwa serikali haitaishia hapo.

“Mpango uliopo ni kuendelea kujenga matangi mengine ya aina hio, katika maeneo kadhaa, yenye shida ya huduma ya maji safi na salama,” anasisitiza.

Dira hii inaungana kikamilifu na Mipango ya Maendeleo ya Zanzibar, pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, hasa lengo namba sita, linalotaka kila mtu apate maji safi na salama, ifikapo mwaka 2030.

Kwani hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji, Nnishati na Madini ya mwaka 2026/2027, inaeleza kiwango cha uzalishaji maji, kimeongezeka kutoka wastani wa lita million 211 na kufikia lita milioni 218 kwa siku.

Kiasi hicho ni  sawa na asilimia 86.5 ya mahitaji kwa mwaka 2025/2026, huku mahitaji halisi yakiwa ni lita million 252 kwa siku, hali inayopelekea kuwepo kwa upungufu wa wastani wa lita million 34 kwa Zanzibar.

Katika kuungamkono juhudi hizi wananchi wanalojukumu la kulinda miundombinu hii dhidi ya uharibifu wa makusudi au wizi.

Kwani Matangi na mabomba haya ni mali ya umma iliyowekezwa kwa manufaa ya umma.

Hivyo ni lazima jamii ishirikiane na serikali kulinda mazingira yanayozunguka vyanzo vya maji na visima ili kuzuia kukauka kwa maji ya ardhini kutokana na ukataji miti au shughuli zisizo endelevu za kibinadamu.

Mradi wa ujenzi wa matangi manne ya maji yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja kila moja kisiwani Pemba,  ni ushahidi wa vitendo wa dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli.

MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...