UKWELI WA DK. MWINYI BAADA YA KUINGIA IKULU, SASA WANAFUNZI 1,236 KONDE WATELEZA KWENTE '''TAIZ' WAKIWA GHOROFANI
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KWA sasa
wazanzibar wote, wamo katika shamra shamra za miaka sita ya uongozi war ais kipendwa
Dk. Hussein Ali Mwinyi, tokea alipowasili Ikulu ya Zanzibara mwaka 2020.
Lengo kuu la
yeye kuingia Ikulu, ilikuwa ni kumboa mzalendo wa Zanzibar, ili azidi kuwaletea
neemaa, baada ya kupokea kijiti za uongozi kutoka kwa mtangulizi wake Dk. Ali
Mohamed Shein.
Si unajua
ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM, iko demokrasia iliyokomaa, kwa kuhakikisha viongozi
wanapishana, ili kuomba ridhaa kwa wananchi, kila baada ya miaka mitano.
Mwenye Dk.
Mwinyi tokea awamu yake ya kwanza n ahata hii ya pili, ambapo sasa ameshatimiza
miaka sita ya uongozi, alipita kwa wananchiu kuwaomba ridhaa.
Nakumbuka vyema,
alipokuwa ndani ya Jimbo la Konde, aliwaomba wananchi kwanza kumpa ridhaa, ili
azidi kunogesha maendeleo ya kielimu, ikiwemo ujenzi wa skuli za kisasa.
‘’Nawaombeni
kura, nikifika Ikulu miongoni mwa ahadi zangu moja wapo ni kuwajengea skuli ya ghorofa
hapa Konde, ili kuweka mazingira rafiki ya elimu,’’alisisitiza.
Maneno hayo
Dk. Mwinyi aliwahi kuyarejea alipokuwa jimbo la Gando, kwamba anahamu kuona
Unguja na Pemba, imejaa maghorofa na vifaa kamili vya kujifunzia na kufundishia.
Ahada hizi
za Dk. Mwinyi kwa wakati ule, zilisisitizwa kwa mkazo na Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Makombeni.
‘’Dk. Mwinyi
amekuwa ni muungwa, na anapoahidi suala la kutekeleza huwa ni jambi rahisi,
naamini kule Konde, Kiwani, Mwambe, Kengeja na Michakani maghorofa yanakuja,’’alisema.
Hata aliyekuwa
mgombea uwakilishi Jimbo la Konde Zawadi Amour Nassor, nae aliwakumbusha
wananchi kuwa, wapo viongozi kadha waliopita walishafanya makubwa, ingawa na Dk. Mwinyi ataongeza.
‘’Wakati
ameshaahidi ujenzi wa skuli wa ghorofa ya Konde, naamini tumpeni kura, ataijenga,
maana huyu amekuwa na maneno kidogo na vitendo ndio vingi,’’alisisitiza.
BAADA YA
KUINGIA IKULU DK. MWINYI
Sasa ni
miaka sita, tokea mpendwa huyo arejee tena kuwaongoza wananchi wa Zanzibar, na
tayari wanafunzi wa skuli ya sekondari Konde wanajipatia haki yao ya elimu
wakiwa ndani ya skuli ya ghorofa tatu.
Kumbuka sasa,
wazanzibari hao, sasa wanasherehekea miaka sita ya Dk. Mwingi kuwaongoza, tokea
alipopewa ridhaa pale mwaka 2020.
Yeye anaendeleza
yale aliyoachiwa na watangulizi wake, ingawa kila mmoja ni shahidi miaka yake sita
ya uongozi, utadhania miaka 600, kutokana na utekelezaji wa Ilani uliotukuka.
Na ndio
maana, kwenye moja ya tunda la miaka yake sita hii, ni upatikanaji wa skuli ya
ghorofa tatu ya sekondari Konde wilaya ya Micheweni.
Kazi ya
kuifungua skuli hii, ilifanywa na mwenyewe Novemba 1, mwaka jana, ambae kisha
aliwahutubia wananchi wanaccm wa mikoa miwili ya Pemba.
Hafla hiyo,
ilifanyika uwanja wa mpira Konde, ambae aliwaeleza wananchi namna alivyofanikiwa
kuitekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa vitendo kwa wakati huo.
‘Leo ndani
ya uongozi wa serikali ya awamu ya nane, nimeshayatekeleza kwa vitendo, aliyowaaahidi
wananchi, ikiwemo ujenzi wa madarasa 2,773 katika skuli zote za Unguja na Pemba,’’alianza
hivyo.
Akasema,
Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 iliitaka serikali ya awamu ya nane, kujenga madarasa
1,500 ingawa wameshavuuka lengo hilo, kwa asilimia 184, na bado kazi inaendelea.
Kumbe hata
hivyo anasema, serikali imepanga hadi kufikia mwakani, iwe imeshajenga vyumba 2,000
vya madarasa katika skuli zote za Unguja na Pemba, ili kuondoa mikondo miwili.
‘’Ndani ya
miaka sita ya madarakani, ya serikali ya awamu ya nane, anawaeleza wale wengine
kuwa, kama wanapiga porojo na kusema, uongo waangalie takwimu kutoka wizara ya Elimu,
zitadhihirisha ahadi zangu ,’’anasema.
Kumbe Dk. Mwinyi
ndani ya miaka hii sita ya kuwaongoza kwa utulivu wazanzibar, mwenyewe anataja
mafanikio mingine kuwa, ni kuongezeka kwa bajeti ya mikopo ya elimu ya juu.
Hapa ukiwa
mtundu wa kufuatilia hutuba za Dk. Mwinyi utagundua kuwa, bajeti hiyo imeongezeka,
kutoka shilingi bilioni 11.5 hadi shilingi bilioni 33.4 mwaka 2024.
‘’Haya hayahitaji
porojo, maana nambari siku zote zinasema ukweli, na waje waangalie mafanikio
haya, sasa wanaopita pita wakisema hovyo, wapuuzeni,’’anaeleza.
Dk. Mwinyi akasema, kwa vile nia ya serikali ni pia kuondoa unyonge
wa ajira hasa za waalimu, anasema kwanza wapo waliokwisha ajira wafikao 3,384 na
mwaka jana na wingine 1,239 wataajiriwa baadae.
Hapa akitaja
skuli mpya za ghorofa, ikiwemo ya Konde kwamba nao watafika na jira hizo, ili
kuongeza idadi ya waalimu kutoka 24 wa sasa.
‘’Bado tuna
nia ya kuongeza idadi ya waalimu katika uajiri, ili kuhakikisha hakuna skuli
yenye upungufu wa waalimu, kwani kwenye samani na majengo, tuko vizuri,’’anafafanua.
Hapa akadakia
kuwa, kila skuli mpya inayojengwa kwa sasa, suala la miundombinu ya samani,
maktaba na maabara ya masomo ya sayansi ni lazima.
Tena akasema
hayo yanafikishwa, kutokana na kuimarika kwa bajeti ya mendeleo ya wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Amali Zanzibar, kwa kufikia shilingi blioni 518 sawa na ongezeko
la asilimia 552.
‘’Ndani ya
miaka sita ya serikali ya awamu ya nane, bajeti ya maendeleo ya wizara ya elimu
imekuwa, kwani kabla, ilikuwa ni shilingi bilioni 83,’’anasema.
WEMA
Katibu Mkuu,
wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdalla Said, anasema miaka
hii sita ya Dk. Mwinyi madarakani, ndani ya wizara wanayomingi ya kujivuania,
likiwemo ujenzi wa skuli ya ghofora ya Konde.
‘’Kwa mfano leo
ukienda shehia ya Konde, ipo skuli ya ghorofa tatu, na tayari kuanzia Janauri,
2025 wanafunzi 1,236 wameshaanza kuitumia, haya sio matunda madogo,’’anasema.
Tena akafafanua
kuwa, ujenzi huo unakwenda sambamba na azma ya kweli, ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein
Ali Mwinyi, ya kutaka kuoandoa mikondo miwili.
‘’Sisi
wizara ya Elimu, tunashukuru mno kwa jitihada zako maalum kwetu, ambazo
zinachangia kwa kiwango kikubwa, kuimarisha miundombinu ya elimu nchini,’’anaeleza.
MKOA
KASKAZINI PEMBA
Mkuu wa Mkoa
wa kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya, kubwa zaidi anakumbushia kuwa, awali
wanafunzi walikuwa wakiingia mikondo mitatu, ingawa kwa ufunguzi wa skuli hiyo,
hilo sasa limeondoka.
Anasema
miaka sita ya Dk. Mwinyi kwa wananchi wa Konde, na hasa baada ya kumalizika kwa
skuli ya ghorofa tatu, wanalo la kujivunia.
‘’Sasa wanafunzi
wa skuli ya sekondari ya Konde, naamini wanasoma kwa utulivu, na hakuna tena
mikondo miwili hapa, tunakushukuru,’’anafafanua.
Hata Mwakilishi
wa Jimbo la Konde Zawadi Amour Nassor, anasema sasa Konde, inag’ara kwa kuwepo
skuli tatu za ghorofa, ikiwemo Kifundi, Makangale na Konde.
‘’Leo ndani
ya miaka sita ya Dk. Mwinyi Konde inang’ara kama ilivyo majimbo mingine ya
Zanzibar, na mfano ni skuli hii ya Konde,’’anasema.
WANANCHI
Haji Ali Haji
anasema yapo mazuri yaliyofanywa na Dk. Hussein katika mkoa huo, ikiwemo ujenzi
wa skuli tatu za ghorofa, ndani ya Jimbo la Konde.
‘’Sisi
wananchi wa Konde na mkoa kwa ujumla, tunakushukuru sana, kwa jitihada zako, na
tunakuomba kuendelea kutuunga mkono,’’anafafanua.
Zuhura
Khatib Mwadini, anasema sasa watoto wao, wanasoma ndani ya skuli ya ghorofa,
ambayo miaka 62 iliyopita, haikujengwa.
‘’Kwa hakika
Dk. Mwinyi ni mtekelezaji kweli wa ahadi zake, maana wakati atuaomba kura na
kutoa ahadi ya ujenzi wa skuli ya ghorofa, kwa hakika sikuamini na leo nampa
tano,’’anasema.
Aisha Juma
Nassor, anasema yeye alisoma miaka 46 iliyopita, ingawa mazingira hayakuwa rafiki
kama leo, ikiwemo samani na vifaa vya kujifunzia.
MWALIMU/WANAFUNZI
Msaidizi Mwalimu
mkuu wakuli ya sekondari ya Konde Saleh Mbaroku Hemed, asema tunda kubwa la miaka
sita ya Dk. Mwiyi ni kupatiwa skuli ya kisasa.
‘’Kuanzia
mwezi na Januari mwaka jana, tumeshahamia rasmi, maana samani zote na vifaa vya
sayansi navyo viemshawekwa, kilichobakia ni kufanyakazi kwa bidii,’’anasema.
Maana idadi
ya vyumba walivyonavyo, sasa kila chumba kimoja ni wastani wa anafunzi 45, kama
inavyotaka sera za kimataifa.
Juma
Ramadhan Haji ni mwanafunzi wanaosoma skuli ya Konde, wanasema sasa wamefurahia
kuingia ndani skuli ya kisasa.
‘’Tunayafurahia
mno matunda ya Dk. Mwinyi kwetu, sasa kilichobakia ni kuongezea idadi ya
waalimu wa sayansi tu,’’anasema.
UJENZI WA
SKULI HIYO
Skuli hiyo yenye
ghorofa tatu, ina madarasa 42, yenye uwezo wa kusomewa na wanafunzi 1,890
wastani wa wanafunzi 45 kwa kila darasa moja.
Inazo ofisi
nne za waalimu, ofisi ya Mwalimu Mkuu, ukumbi wa mkutano, vyoo 52, maabara
mbili za sayansi, chumba cha TEHAMA, ushauri nasaha pamoja na maktaba moja na
kugharimu shilingi bilioni 6.2.
Mwisho
Comments
Post a Comment