Skip to main content

TAMU, CHUNGU USAFIRI WA UMMA KWA WATU WENYE ULEMAVU, HADI VIGARI VYAO WALIPISHWA KAMA MZIGO

 


NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@

UDHALILISHAJI katika vyombo vya usafiri ni pamoja na ukatili wa kijinsia, inayoashiria uvunjifu wa haki za binaadamu.

Kwa wenzetu wenye ulemavu, wao wamekuwa nambari moja kudhalilishwa, wakati wanapokwenda ama kurudi kwenye mipango yao ya maisha.

Hali hiyo hujumuisha kuguswa mwili bila ridhaa, matusi, kauli za kubaguliwa au kulazimishwa kukaa katika mazingira yanayoshusha heshima na utu wao.

Mkurugenzi wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu Juma Kombo Hija Pemba anasema, vyombo vya usafiri havipo rafiki kwao.

 Anasema ukiangalia Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa, inayolenga kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu, pamoja kusimamia haki zao.

Katika kuweka mazingira mazuri ni pamoja kusimamia haki zao na ujumuishwaji katika vyombo vya usafiri, hususana watu wenye ulemavu wa viungo.

Anasema yapo matukio matatu yaliyoripotiwa kwa mwezi Juni na Jualai mwaka huu, katika jumuiya hiyo amabapo mtu mmoja mwenye ulemavu wa viungo, alilipishwa nauli yeye pamoja na kiti mwendo chake.

Yupo abiria mmoja hajachukuliwa kisa dereva kuona kupotezewa muda na ipo kesi moja mtu mwenye ulemavu, amepakiwa ila kigari chake kimeachwa chini siku hiyo.

Mwinyi Hamad Othman ni mkaazi wa Majenzi wilaya ya Micheweni mwenye ulemavu, anasema, udhalilishaji wanaoupata kwa kuachwa na kutochukuliwa, hususan kwa daladala, ni sehemu ya udhalilishaji.



"Makonda na madereva wamekuwa wakitudhalilisha kwa kutudharau na kutuacha tunapokuwa njiani tunaposimamisha daladala, hawatupakii maana wanajua mpaka watubebe, watupandishe na wanaona tunawapotezea muda,’’anasema.

Faudhia Bakari Omar anasema, udhalilishaji wanaupata kwenye vyombo vya usafiri wa umma ni pamoja na kushikwa shikwa ovyo kwa kuwakamata baadhi ya maeneo na siyo rasmi.

Anasema wanataka wapande wenyewe kutokana na hali wanashindwa hupelekea mpaka kubebwa na mazingira hayapo rafiki, hasa kwa gari aina ya dyna.

Mtumwa Khamis Kombo anasema, wakati mwengine hukutana na madereva na makonda, huwalipisha wao wenyewao na vigari vyao.



‘’Kwa kiasi fulani, udhalilishaji tunaupata maana hutuambia tulipe nauli yetu na vigari nyetu, mbona wenye miguu yao hawalipishi, miguu,’’anahoji.

MIONGOZO INASEMAJE

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha  12 (1) kinasisitiza kuwa,  ‘watu wote ni sawa na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria’.

Sheria ya Watu wenye Ulemavu Nambari 8 ya mwaka 2022 kifungu cha 30 (1) kinakubali kuwa, ‘watu wenye ulemavu hawatobaguliwa na kudhalilishwa kwa namna yoyote na katika ngazi zote kutokana na ulemavu wake’.

Na katika kifungu cha 2, kimfafanua kuwa, ‘Baraza litaanzisha program mbalimbali kuzuwia watu wenye ulemavu kubaguliwa au kudhalilishwa ikijumuisha kuitwa majina yasiyofaa, kudharauliwa, kukejeliwa na kutumiwa vibaya’.



Azimio la Ulimwengu juu ya Haki za Binaadamu Toleo maalumu la kuadhimisha miaka 60 ya mwaka 1948 mpaka 2008 katika kifungu cha 5 mtu yoyote asiteswe, asidharauliwe kutendewa kinyama au kikatili.

Na katika kifungu cha 7 kikafahamisha mbele ya sheria watu wote ni sawa na wanastahili haki sawa za kulindwa kutokana na ubaguzi wowote unaoweza kuvunja.

Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu wa mwaka 2006, Ibara yake ya 15 kifungu cha 1 kinsisitiza kuwa, ‘hapana mtu atakayewekwa katika hali ya mateso au udhalimu, kutendewa au kuadhibiwa kinyume cha ubinadamu, kiudhalilishaji au kikatili kwa namna yoyote ile’.




Na katika kifungu cha 2, kikeleza kuwa, nchi wanachama zitachukua hatua za kisheria, kijamii, kielimu ili kuwalinda watu wenye ulemavu, katika misingi ya usawa na watu wengine, ili wasiteswe, wasifanyiwe udhalimu, kudhalilishwa.

BARAZA NA JUMUIYA ZA WATU WENYE ULEMAVU ZINASEMAJE

Mashavu Juma Mabrouk ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Pemba anasema, vyombo vya usafiri, havipo rafiki kwa watu wenye ulemavu.

Anasema malalamiko huwa anayapata kwa watu wa kundi hilo, ikiwemo kuachwa wanaposimamisha gari pamoja na kuvunjiwa viti vyao mwendo.

‘’Mila, dini na taratibu haiwezekani mwanammke kubebwa na mwanamme, ila hapana jinsi na watu wenye ulemavu hukutana na viashiria pamoja na udhalilishaji,’’anasema.

Hidaya Mjaka Ali Msimamizi wa huduma za marekebisho kwa watoto wenye ulemavu Pemba anasema, udhalilishaji wa kufanyiwa kitendo kwenye vyombo vya usafiri, vimepungua isipokuwa vyombo havipo rafiki kwao.



Kumbe zipo badhi ya nchi kuna vyombo vya usafiri vipo rafiki kwa watu wenye ulemavu wa viungo, huenda safari zao bila kupata changamoto na viashiria vya udhalilishaji.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar TAMWA kupitia Afisa Programu wa kupambana na udhalilishaji Asia Hakim, ametahadharisha juu ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa wenye ulemavu.

Katika kupunguza athari hizo, TAMW imewajengea uwezo waandishi wa habari, kuripoti matukio ya udhalilishaji hasa maeneo yasiopewa kipaumbele, ikiwemo kwenye vyombo vya usafiri.

‘’Tunao mradi wa ‘Tunaweza Pamoja’ unaotekelezwa na UN-Women kwa kushirikiana na TAMWA Zanzibar, hasa kwa wialaya za Wete na Micheweni,’’anafafanua.

SERIKALI KUU INAFANYAJE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akifungua Ijitimai ya Kimataifa Kidoti, anasema vitendo hivyo vinatia aibu jamii na inaenda kinyume na maamrisho ya dini.

Anasema lazima jamii ishirikiane kutokomeza vitendo hivyo, kwa kuchukua na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria.

Anasema kupitia njia hiyo itaweza kuandaa jamii ambayo itapiga vita mambo yote yanayosababishwa na mmongonyoko wa maadili katika jamii ikiwemo vitendo vya udhalilishaji

Akiwasilisha bajeti ya wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka 2026/2027, Waziri wa wizara hiyo,  Athanas Paul anasema, wizara itahakikisha kuimarisha uratibu wa ufikiwaji wa usawa wa kijinsia na kupambana na vitendo vya udhalilishaji.

Akasema katika kupunguza wimbi hilo, wizara kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, inaendelea kutumia mbinu tofauti kukabiliana na vitendo hivyo.

‘’Wizara inaendelea kuweka mikakati mbalimbali inayolenga kutatua na kuratibu, kusimamia na kutekeleza Mpango Kazi wa Pili wa Kitaifa wa Kupambana na Vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa wanawake na atoto,’’ anaelezea.

Hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha mwaka 2025/2026 ya makamo wa kwanza wa rais iliyosomwa Harusi Said Suleimanam inasema imendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kubadili tabia kwa kuachana na tabia hatarishi.  

Kuwajengea uelewa watu wenye ulemavu na jamii kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu na kuendeleza mapambano dhidi ya udhalilishaji.

 

MKUU WA VYOMBO VYA MOTO ANALIPI

Mkuu wa waendesha bodaboda wilaya ya Micheweni Juma Khamis Nassuha anasema, zipo sheria ndogo ndogo na kubwa na ipo katiba ya Jumuiya yao, ambapo hayo yote yanapigwa vita.

 Nae dereva wa gari ya Wete- Chake chake Abdalla Ali Akida, anakiri kuwa baadhi yao, huwaacha watu wenye ulemavu, ingawa ni kutothamini tu utu wao.

‘’Mimi huwasikubali kuwaacha, labda iwe gari imeshajaa, hapo huwawashia taa na kuwapita,’’anasema.

Haida Juma Jabu, kondakta wa gari ya Micheweni- Chakechake, anasema hajawahi kuwaacha watu wenye ulemavu wala kuwalipishia viti vyao mwendo.

‘’Ni kweli tabia zetu sisi makondakta na madereva tunatofautiana na sikatai, kwamba wapo wenzetu wanawaacha, lakini mimi huwabeba,’’anasema.

NINI KIFANYIKE

Fatma Mkaha Sharifu anasema ni serikali kuwasaidia, ili kuepukana na changamoto hiyo, ikiwemo kuwepo kwa adhabu kali kwa wanaowaripoti.

Mashavu Juma Mabrouk, anasema elimu iendelee kutolewa kwa maderava, makondakta na watu wenye ulemavu, ili mwafaka upatikane.

TAKWIMU

Kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2023 mpaka 2025 Zanzibar iliripoti matukio 609 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake ikihusishwa matukio ya kubakwa, kuingiliwa kinyume na maumbile, kutoroshwa, shambulio la aibu kukashifiwa na shambulio.

Ikiwa mwaka 2023 matukio  yalikuwa 236 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia  kwa waathirika wanawake  sawa na asilimia 12.0 na kwa mwaka 2025 yalikuwa  211 sawa na asilimia  11.7 na mwaka 2025 yalikuwa162 sawa na asilimia  13.2.

Na katika mwaka 2023 hadi 2025 matukio ya kubaka yaliyoripotiwa yalikuwa 234 kwa  wanawake,  matukio ya kuingilia kinyume na maumbile  yalikuwa 31, matukio ya kutorosha  22 , matukio ya shambulio la aibu, kukashifu yalikuwa 148, na matukio ya shambulio yalikuwa  174.

               MWISHO.

 

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...