NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@
MALEZI
bora na makuzi ya mtoto, ni jambo muhimu
kwa maendeleo yake,kimwili na kiakili.
Hili linajumuisha huduma zote muhimu
anazostahili kupewa mtoto, kuanzia miaka 0 hadi 8, ili kumuwezesha kukuwa na
kufikia utimilifu wake.
Ikiwa ni kimwili, kiakili, kijamii,
kihisia na kimaadili, ilikushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na kuyamudu
mazingirayake.
Mara nyingi ni rahisi kupata haya yote,
kutoka kwa wazazi au walezi,lakini wengi wao husahau kwamba matumizi ya lugha
nzuri kwa watoto,inamchango mkubwa katika ustawi wao.
Na zipo sheria zinazopinga ukatili wa aina
zote dhidi ya watoto, kwamsingi kwamba malezi bora kwa mtoto, ndio msingi imara
kwa makuzi yake.
Mfano, Mkataba wa kimataifa wa haki za
watoto duniani (Conventionoftherightsofthechildren) wa mwaka 1989, ambao
umeanza kutumikarasmi mwaka 1990.
Ibara yake ya 19 inasisitiza, kuwa‘nchi
wanachama kuhakikishawanakuwa na sheria nzuri zitakazo mlinda mtoto juu ya aina
zote zaudhalilishaji’.
“Nchi wanachama zihakikishe zinakuwa na
sheria nzuri zitakazo mlindamtoto juu ya aina zote za udhalilishaji, uwe wa
kimwili au kiakili,kujeruhiwa, kudharauliwa, kutengwa au kudhulumiwa” inaeleza
sehemu yamkataba huo.
Mkataba
wa haki na Ustawi wa watoto wa Afrika
wa mwaka 1999,kifungu cha 19 kinasisitiza kila mtoto anayo haki ya
kufurahia nakunufaika na malezi bora ya wazazi, na ana haki ya kulindwa.
Na Sheria ya Watoto Zanzibar , namba 6 ya
2011, kifungu cha 15kinasisitiza kuwa, ‘mtu yeyote ambaeanamlea
mtoto, mwangalizi wa mtoto asimfanyie au kuruhusu mtu yeyotekumfanyia mtoto
matendo mabaya”.
Hii ni pamoja na kutomdharau, kumtelekeza
kwa namna ambayoitasababisha kumuathiri mtoto huyo kimwili au kiakili, na
atakaefanyahivyo, atakuwa amefanya kosa.
Bado wapo wazazi au walezi, hutumialugha
na maneno mabaya na yenye kuumiza wakati wa kufundisha aukukanya.
Muda mwingine hufanya hivyo bila kujua
kwamba ni tatizo katika ukuaji wa mtoto.
Eneo jingine, ni kuwa utafiti uliofanywa
na taasisi ya ‘Words Matter Charity ya UK’,mwaka 2023unaonyesha
kwamba, sentensi tano mbaya na zenye athari za muda mrefuzinazotumiwa mara kwa
mara na wazazi na walezi.
Ukaonesha maneno kama “hunamaana hutumiwa
na wazazi na walezi kwa watoto wao kwa asilimu 59, maneno mingine utafiti
ukaeleza kuwa, “wewe ni mjinga kwa asilimia 56”.
Ukaenda mabali zaidi utafiti huo na
kulitaja maneno “huwezi kufanya kituchochote vizuri kwa asilimia 52, ‘’hunathamani
yeyote kwa asilinmi 48 na ‘naona aibu kwaajili yako huwa kwa asilimia 48.
Huku utafiti ukisisitiza kwamba, maneno yanaweza kujenga au kubomoamaisha ya
mtoto, kwa kiasi kikubwa.
SIMULIZI
ZA WATOTO
Salum (13 sio jina lake rasmi) anahadithia,
wakati yupo darasa la tano, mwenyekiti wa kamati ya skuli yao, alimsimamisha
mbele ya darasa kwa ajili ya
kumfahamisha, ingawa maneno alioitumia hayakua mazuri.
Anasema japo miaka miwili imepita sasa, lakini
ni maneno yanayomuumiza kama alitamkiwa jana.
Fatma (15 si jana halisi) anaeleza aliwahi
kutamkiwa maneno mabaya, makali na yenye kuumiza na babayake mzazi, ambayo wamebaki akilini mwake
hadi leo,kwa kosa la kutokwenda skuli moja.
Watu watatu kati ya watano waliozungumza
na mwandishi wa habari hizi, walionyesha kuguswa moja kwa moja, na matukio
haya, na kuonyesha watu wao wa karibu ndio wanaohusika katika hili.
DINI ZINASEMAJE?
Sheikh Said
Ahmed anasema katika dini ya Kiislamu matumizi ya maneno ya busara, upole na
hekima ni msingi mkuu wa malezi na makuzi ya mtoto.
Anafahamisha, hili
limo katika Qur-an tukufu sura ya 31:12-19, kupitia kisa cha Luqman
alipomshauri mwanawe, ambapo alitumia maneno ya upendo na yenye kuelimisha, yakionyesha
umuhimu wa mazungumzo ya busara ili mtoto aelewe kwanini jambo fulani ni baya.
Hata Mchungaji
Samuel Maganga anasema Bibilia inafundisha kua, maneno ya upole na busara hujenga
tabia njema na kuondoa chuki na maneno makali yanaweza kuumiza na kuleta uasi.
Akinukuu mstari
wa bibilia anasema “Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, isipokua
linalofaa”.
JE
SABABU NI ZIPI?
Salum Abdallah Suleiman mzazi miaka 70,
anasema, mila, tamaduni nadesturi zilizopo katika jamii ni miongoni mwa sababu,
zinazopelekeahali hiyo.
Anasema, jamii imejengeka kwamba mzazi,
mlezi au yeyote mwenye umrikumzidi mwingine, anahaki ya kuzungumza nae kwa
namna yeyote, aitakayo isiyo umiiza akili au mwili.
Jokha Ame Makame mzazi miaka 24 anasema,
mzazi kukosa elimu ya malezibora, inaweza kuwa ni miongoni mwa sababu ya hiyo.
Hata Mohamed Amour (67) anasema, historia
ya ukuaji wa mzazi ni moja yasababu, zinazopelekea hali hiyo.
Anaeleza kwamba, wengi wa wazazi wenye
tabia hiyo, walikulia mazingirahayo hayo, hivyo wamekuwa wakiamini kwamba,
maneno mabaya ndio malezi.
Nae Salama Abdallah Othman Mratibu
wanawake na watoto shehia yaMjimbini anaeleza, kutokujuwa athari za matumizi ya
maneno mabaya kwawatoto, ndio sababu ya hayo.
MITANDAO
YA KIJAMII IMERIPOTI NINI
Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii takriban
asilimia 33 hadi 40 ya watoto duniani kote hukabiliwa na ukatili wa maneno.
Aidha mitandao inaeleza kua watoto wa rika
zote kuanzia wachanga hadi vijana baleghe , wanaathiriwa na waneno machafu,
ingawa namna wanavyoyapokea hutofautiana kulingana na umri wao.
Aidha mitandao imeripoti uwepo wa athari
za kisaikolojia kwa watoto wanaokulia mazingira ya kutolewa maneno machafu,
ambapo kuna asilimia 64 ya uwezekano wa kupata afya duni ya akili ukubwani.
ATHARI ZAKE NI ZIPI?
Mtaalamu wa saikolojia Ahmada Salum Juma
anasema, zipo athari kazaa, ikiwa ni pamoja na kutokujiaminikwa mtoto.
Anasisitiza kua inaweza kupelekea
kujitenga pamoja na kupunguzaukaribu baina yake na mzazi au mlezi, kwani maneno
hayo, humfanya akatetamaa.
Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Wete Salma
Saleh Hamad anasema,hali hiyo inaweza kuathiri ustawi wa jamii wa mtoto hadu
utuuzima wake.
"Mtoto ambaye anajisikia kukataliwa
au kudharauliwa, anaweza kuanzakuonyesha hasira au kitendo chochote, kwa njia isiyofaa
ili ajilinde mwenyewe", anafafanua.
NINI
KIFANYIKE?
Mzazi Salim Abdallah Suleiman anawasihi
wazazi wenzake, kuhakikishawanatumia maneno chanya wakati wa kukanya au
kuelekeza watoto wao.
Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Wete, Salma
Saleh Hamad anasema, ni vizuri wazazi nawalezi kutumia elimu ya malezi bora,
hekima na busara hasa katikakauli zao.
Mwenyekiti wa watoto Bodi ya ushauri Taifa
Khamis Abdallah Mbaroukanasema, wazazi na walezi wanapaswa kuepuka matumizi ya
maneno na sentensi zisizofaa.
Naibu waziri wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na WatotoZawadi Amour Nassor anasema, malezi mazuri kwa mtoto,
ndio msingiimara kwa maisha yake ya baadae.
TAMWA-Zanzibar ni asasi ya kiraia
inayopambana na aina zote za ukatilidhidi ya wanawake na watoto, afisa programu
ya kupambana na matukiohayo Asia Hakim Makame, anawasisitiza waandishi wa
habari kuelimisha jamii athari za ainazote za udhalilishaji.
Anasema kuwa anaona hatua hiyo itawasaidia
kuongeza uwelewa wakupambana na matukio hayo.
MWISHO.





Comments
Post a Comment