KIVUMBI na vilio viliibuka katika Mahkama ya mkoa Wete,
kufuatia washitakiwa Suleiman Said Khamis (19) na Ali Iddi Ali (33) kwa
kutaka kujitupa dirishani, baada ya kupelekwa Chuo cha Mafunzo kwa muda wa
miaka saba, na kulipa fidia ya shilingi milioni 1, kwa kila mmoja kwa kosa la
kubaka kwa kikundi.
Kabla ya kusoma hukumu yao jana Juni 17, 2025, Hakimu wa Mahkama hiyo Zuwena
Mohamed Abdulkadir, alisema jumla ya mashahidi sita walisikilizwa mahkamani hapo,
na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuacha chembe ya shaka na
umewatia hatiani.
"Kutokana na ushahidi uliotolewa na mashidi wetu, mahkama
tumeridhika na kwani hauna chembe ya shaka,"alisema.
Alisema kwa mujibu wa vifungu cha 108(1) na 110 (1), (2) vya
vheria namba 6 ya mwaka 2018, kinaeleza kwamba kosa, la kubaka kwa kikundi
adhabu yake ni kifungo cha maisha.
Kabla ya kutolewa hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka wa serikali
Juma Mussa Omar, alimuomba hakimu huyo, kutoa adhabu kwa washtaka hao, kwa
mujibu wa vifungu na sheria zinavyoelekeza.
"Mheshimiwa Hakimu matendo haya ni hatari na
yanawathiri wananchi, hivyo ni vyema uegemee kwenye sheria zinavyoelekeza,
wakati unapotoa hukumu, kwani itakua ni darasa tosha kwao, na kwa
wengine," alieleza.
Aidha alieleza kuwa kutokana na heshima na utu wake
ulivyovunjwa binti aliebakwa, ni lazima angaliwe japo kwa chochote, licha ya
kua hakuna malipo yatakayolipa vitu hivyo utu na heshma yake.
Kwa upande wake Wakili wa utetezi wa washitakiwa Abeid Mussa,
aliiomba mahkama kutoa tahfifu wakati inapotoa hukumu, hakuna sababu za
kuwafunga kifungo cha maisha.
"Mheshimiwa hakimu hakuna sababu ya kuwafunga kifungo
cha maisha, wafanyie tahfifu, kwani vipo vifungu vya sheria, ambavyo vinawaelekeza
wakati mnapokutana na kesi kama hizo,"alieleza.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Zuwena alisema mahkama, imeona
washitakiwa ni kosa la mwanzo, hivyo imejiegemeza katika kifungu cha 314 cha sheria
namba 7 ya mwaka 2018, watatumikia chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka saba na
kulipa fidia ya milioni 1, kwa kila mmoja.
Washitakiwa Ali Iddi Ali miaka (33) na Suleiman Said
Khamis (19), Oktoba 11, mwaka jana majira ya saa 1:30 usiku, eneo la Kinyasini wilaya
ya Wete Pemba, wote kwa pamoja, mshitakiwa namba moja ni Ali Iddi Ali alimbaka
mtoto wa miaka 17.
Mshitakiwa nambari mbili Suleimana Said Khamis alimsaidia
mshitakiwa namba moja Ali Iddi Ali kutenda kosa hilo, ambapo ni kinyume na
kifungu cha 108 (1) na110(1) (2) cha sheria nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya
Zanzibar.
Mwisho.
Comments
Post a Comment