Skip to main content

RC SALAMA: AKABIDHIWA RIPOTI YA AWALI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA

 

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

IDARA ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, imemkabidhi ripoti ya awali, ya kampeni ya msaada wakisheria ya Mama Samia, mara baada ya kumalizika kwa kambi ya siku 10 ndani ya mkoa huo.

Kabla ya kukabidhi kwa ripoti hiyo, Mkuu wa Idara hiyo Pemba Bakari Omar Ali, alipongeza ushirikiano alioupata kutoka kwa maafisa wa taasisi mbali mbali za serikali, wakati wote wa kampeni hiyo.

Alisema, katika kampeni hiyo, waliwatumia maafisa wa kamisheni ya wakfu, ardhi, mawakili wa serikali, makadhi, maafisa ustawi, matukio ya kijamii pamoja na waandishi wa habari.

Alieleza kuwa, maafisa hao walisaidia kwa kiasi kikubwa, kupokea malalamiko na kuyapatia ufumbuzi papo hapo na mingine kuziandikia barua taasisi husika.

Alifahamisha kuwa, kampeni hiyo ambayo ilikuwa katika mifumo miwili, moja ni kuwafuata wanafunzi wa skuli, vyuo vya elimu ya juu pamoja na mikutano ya jamii.

‘’Tulijigawa timu mbili, moja wilaya ya Micheweni na nyingine Wete, ambapo maafisa kadhaa walikuwa wanakutana na makundi mbali mbali ndani ya jamii, na kuyapa elimu na ushauri wa kisheria bure,’’alifafanua.



Aidha Mkuu huyo wa Divisheni ya Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Pemba, Bakar Omar Ali alisema, wakati hayo yakifanyika, timu nyingine iliweka kambi katika eneo la Jamhuri Wete, kwa ajili kutoa huduma papo hapo.

Alisema, wapo wananchi ambao walikuwa hawajapata nyaraka kama vile vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho vya ukaazi, usaliji wa vyeti vya ndoa na utatuzi wa migogoro mingine.

‘’Mheshimiwa Mkuu wa mkoa, kambi yetu iliwasaidia mno wananchi, maana hata mawakili, wanasheria, makadhi, watendaji wa mwanasheria mkuu, walitoa huduma bila ya malipo kwa wananchi,’’alifafanua.





Mapema Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib, alisema ataisoma ripoti hiyo, na kama kuna jambo hajalifahamu, atawasiliana na Idara hiyo.

Alisema, wazo la Mama Samia kuwa na kampeni hiyo, imeasaidia kwa kiasi kikubwa, na kuongeza upatikanaji haki zao mbali mbali.

Alieleza kuwa, kampeni hiyo ni sehemu ya maono ya Mama Samia, katika kuhakikisha wanawake, watoto, watu wenye ulemavu na watu wingine wasiojiweza wanapata haki zao mbali mbali.

‘’Lakini hata suala la kuwafikia wanafunzi na wanajamii kwa mikutano ya elimu, ushauri na msaasa wa kisheri iliwaamsha wanajamii, kujua haki na wajibu wao kisheria,’’alisema.

Mapema Mratibu wa kampeni hiyo wilaya ya Micheweni Khamis Bakar Aman, wakati akimkabidhi ripoti hiyo Mkuu wa wilaya ya Micheweni Khatiba Juma Mjaja, alisema changamoto kubwa, walioibua ni utelekezaji wa wanawake na watoto.



Alisema, walipokea kesi kadhaa ambazo wanawake wanawalalamikia waume zao, walioko dago nje ya Pemba, wakishindwa, kupeleka huduma kwa familia zao.

‘’Ijapokuwa tulibaini changamoto nyingine, lakini hili la wanawake kulilia huduma kwa waume zao, ndio linaongoza, hivyo ni sehemu kwa wilaya kulifanyia kazi,’’alifafanua.

Mkuu wa wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja, alisema kazi iliyofanywa na Idara hiyo kusimamia kampeni ya Mama Samia, ni nzuri.

Alisema, anaamini sasa wapo wananchi waliopata uwelewa wa wajibu na haki zao mbalimbali, kama vile umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa, usajili wa vyeti vya ndoa, kifo na haki za wanawake na watoto.

Wakati huo huo Mratibu wa Kampeni hiyo wilaya kwa wilaya ya Wete Moza Rajab Baraka, alimkabidhi ripoti kama hiyo Mkuu wa wilaya ya Wete na Mkurugenzi baraza la mji wa Wete, na kuwampa shukran kwa misaada yao.



Alisema, ushauri, maelekezo na mbinu walizotoa zilisaidia mno kuhakikisha kampeni hiyo ya siku 10, inakwenda vizuri na kumalizika kwa wakati.

Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, kwa mkoa wa kaskazini Pemba, iliendelea tena kuanzia Mei 31, na kumalizika Juni 9, mwaka huu.

                         Mwisho   

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...