NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@
HATIMAE mtuhumiwa wa ubakaji wa mtoto wa
miaka saba, ambaye ni Askari wa Jeshi la Polisi mwenye namba H.5290 D/C Godfrey
Meckioru Mushi miaka (34) wa Limbani Wete, ameachiwa huru na mahkama ya mkoa
iliyopo, Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akitaja
sababu za kuachiwa huru mtuhumiwa huyo Hakimu wa Mahkama hiyo Zuwena Mohamed
Abdul-kadir alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, umekua dhaifu,
na pia umeshindwa kuleta mashahidi
muhimu.
Alisema
jumla ya mashahidi wanne walisikilizwa, ingawa ushahidi wao haukuweza
kuishawishi mahkama, na kuweza kumtia hatiani mtuhumiwa.
Alisema
upande wa mashataka hawakuleta shahidi ambae ni baba mzazi wa muathirika, ambae
yeye ndie aliemuhoji na kumuambia kama, mtuhumiwa ndie aliemfanyia kitendo
hicho.
‘’Mahkama
imepata wasiwasi na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe, kwamba ni wa
kupangwa,’’alieleza.
Alifahamisha
kwa kutokana na mazingita hayo, mahkama haikumtia hatiani, hivyo imemuachia huru,
Askari huyo, ili akaendelee na majukumu mingine.
Kwa
upande wake Mwendesha Mashtaka wa Serikali Juma Mussa Omar, hakukubaliana na
uwamuzi huo uliotolewa, na alitoa indhari ya kukata rufaa.
‘’Mheshimiwa
Hakimu mimi sijaridhika na hukumu hiyo, hivyo natoa indhari ya kukata rufaa
ndani ya wakati uliopangwa na sheria,’’alieleza.
Mtuhumiwa
huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 2024 eneo la Limbani wilaya ya Wete, mkoa
wa kaskazini Pemba, kwa alimuingilia kimwili mtoto wa miaka saba (7) jina
limehifadhiwa.
Ambapokufanya
hivyo, ni kosa kinyume na kifungu cha
108 (1) (2) (e) na 109 (1) vya sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
MWISHO.
Comments
Post a Comment