Skip to main content

MHANDISI ZENA AONGOZA MATEMBEZI JUKWAA LA UWEKEZAJI LA MWAKA 2025 PEMBA, AWAAMSHA WANANCHI

 


 NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, amesema tayari serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeanza kwa vitendo kukifungua kisiwa cha Pemba kiuchumi.

Mhandisi Zena aliyasema hayo jana, eneo huru la Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, mara baada ya kuyapokea matembezi ya wanavikundi vya mazoezi na wananchi, kwenye kongamano la uwekezaji la mwaka 2025, yalioandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ‘ZIPA’.

Alisema, kufanyika kwa kongamano hilo ni sehemu ya kukifungua kisiwa hicho kiuchumi, ujenzi wa barabara kadhaa za kisasa pamoja na utanuzi na ujenzi wa bandari mbali mbali.

Alisema, serikali inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi, inaendelea kuonyesha kwa vitendo nia yake ya kukifungua kisiwa cha Pemba, kama alivyokuwa akiinadi wakati wakati wa kampeni.

Alieleza kuwa, kilichobakia kwa wananchi wa Pemba, ni kushirikiana kwa karibu na serikali yao, ambayo ina nia ya dhati kuona uchumi wa Pemba, unainuka.

‘’Kufanyika kongamano hili hapa Micheweni maeno huru ni sehemu moja wapo, ya kukifungua kisiwa cha Pemba, kiuchumi maana hata hapa wapo wananchi waliopata ajira za muda,’’alifafanua.

Akizungumza kuhusu kazi za ‘ZIPA’ Mhandisi Zena, alisema inafanyakazi kubwa ya kuhamasisha uwekezaji ndani ya nchi, kwa kuwaleta wawekezaji na taifa kupata manufaa.

Aliongeza kuwa, ujio wa wawekezaji hao, unatanua ongezeko la ajira kwa wananchi, na kuongeza pato la tu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

‘’Wenzetu wa ZIPA, kwanza niwapongeze kwa dhati kwa kazi mnayoifanya ya kuitangaaza Zanzibar na kusababisha kumiminika kwa wawekezaji,’’’alifafanua.

Hata hivyo Mhandisi Zena, alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa kazi kubwa ya kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji.

‘’Kwa mfano hapa eneo huru la Micheweni Pemba, sasa zipo barabara za kisasa zinazoingia ndani, miundombinu ya umeme, ambayo ni sehemu ya kuwavutia wawekezaji,’’alifafanua.

Alieleza kuwa, eneo jingine ni kuona ‘ZIPA’ imeshapanga kwenda kila mkoa wa Zanzibar kutoa elimu ya uwekezaji na kwa upande wa mkoa wa kaskazini Pemba, elimu hiyo itatolewa kwenye la hilo, kuanzia mwezi Septemba, mwaka huu.

Hata hivyo, amewakumbusha wananchi hao wa mkoa wa kaskazini Pemba, kuitumia fursa hiyo, ili wajifunze namna ya uwekezaji bora.



Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ‘ZIPA’ Saleh Saad Mohamed, alisema wanaendelea na jukumu la kuhakikisha, kuna na uwekezaji wenye manufaa kwa watu wote.

Alieleza kuwa, juhudi za Dk. Mwinyi katika kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji, inawapa ari ya kufanyakazi kwa bidii, jambo ambalo ni manufaa kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, alisema katika uwekezaji uliopo Pemba, umesababishwa na utendaji kazi kwa watendaji wa ZIPA.

‘’Nichukuwe nafasi hii, kuwapongeza sana wenzetu wa ZIPA kwa kazi kubwa wanayoifanya, ya kuvuta wawekezaji na sasa eneo huru la Micheweni, limekuwa la kuvutia,’’alifafanua.




Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaamed Khamis, alisema sasa Micheweni imekuwa mpya, baada ya kufunguliwa kwa eneo huru la Micheweni.

‘’Kwa hakika eneo hili, lilitangaazwa tokea mwaka 1992, kuwa ni eneo huru, ingawa kwa wakati huo, halikufanyiwa kazi, ingawa kwa sasa ndani ya mwaka 2025, limefunguliwa kwa kivitendo,’’alifafanua.

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Micheweni Pemba, walisema hatua ya Dk. Mwinyi ya kukifungua kisiwa cha Pemba, ni ishara ya ukweli wake na nia yake thabiti.

Hamad Issa Hamad, alisema Dk. Mwinyi ni kiongozii pekee, aliyeonesha ujasiri wa kuweka mazingira rafiki kwa vitendo eneo la uwekezaji.

Nae Bahati Mansour Kassim, alisema aliwaomba wawekezaji kuangalia kwa jicho la pekee, nafasi za wanawake katika ajira za muda na za kudumu.




Leo Juni 16, mwaka huu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwahutubia wananchi wa mikoa miwili ya na wawekezaji katika viwanja vya maeneo huru Micheweni, kwenye jukwaa la uwekezaji la mwaka 2025.

                    Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...