NA MARYAM SALIM, PEMBA@@@@
KUTOKUFIKA kwa mtuhumiwa Zaid Mussa
Zaid miaka (46) mkaazi wa Machomanne pamoja na wakili wake katika mahakama ya
Mkoa ‘C’ Chake Chake Pemba, kumepelekea shauri hilo kuahirishwa mahakamani
hapo na kupangwa tarehe nyengine kwa ajili ya utetezi.
Mapema Mwendesha mashitaka
akiwakilisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka wa serikali, Kheir Hassan Omar,
aliieleza mahkama hiyo mbele ya Hakimu Hamisuu Saadun Makanjira kwamba, shauri hilo
lilifikishwa katika mahakama hiyo, kwa ajili ya utetezi ingawa mtuhumiwa na wakili
wake, hawakuhudhuria.
"Mheshimiwa Hakimu, shauri
lilimefikishwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa utetezi, ambalo linamkabili
mtuhumiwa Zaid Mussa Zaid, anaedaiwa kupatikana na dawa za kulevya.
"Ingawa mtuhumiwa na wakili wake,
hawakuja mahakamani na hatuna taarifa zao, hivyo tunaomba mahkama kutokana
na shauri hili, liahirishwe na lipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa
utetezi," alidai.
Baada ya ombi hilo la kuahirishwa
kutoka kwa Mwendesha Mashitaka, Hakimu huyo hakuwa na pingamizi, hivyo aliliahirisha
shauri hilo na kutaka lirudi tena mahakamani hapo Juni 25 mwaka huu, kwa
utetezi.
Aidha Hakimu huyo, pamoja na
mtuhumiwa huyo alitoa onyo kwa wakili wa matuhumiwa nae aitwe na wafike siku
hiyo, ili taratibu nyingine ziendelee, za shauri hilo.
Kabla ya kuahirishwa kwa shauri Hati
ya mashitaka ya mtuhumiwa inadai kwamba, mtuhumiwa anakabiliwa na kosa la
kupatikana na dawa za kulevya.
Ilidaiwa kwamba mnamo Agosti 31 mwaka
2024, majira ya saa 6:0 mchana shehia ya Wawi, bila halali, alipatikana na kete
89 zinazosadikiwa kua ni za dawa za kulevya aina ya Heroin, zikiwa na uzito wa gramu
1.0947, jambo ambalo ni kosa kisheria.
MWISHO.
Comments
Post a Comment