NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@
MKAGUZI wa
jeshi la Polisi shehia ya Pandani wilaya ya Wete, Khalfan Ali Ussi, aliwakikishia
mafundi wanaojenga kiuto cha cha Pandani kuwa, kua jeshi la Polisi kwa
kushirikiana ulinzi shirikishi, kitakua bega kwa bega, ili kuhakikisha
wanakamilisha ujenzi huo bila ya uhalifu.
Alisema
kua kazi ya jeshi la Polisi ni kuhakikisha usalama kwa wananchi wake, hivyo ni
vyema kuendelea kufanya kazi zao wa weledi wa hali ya juu, na kujenga majengo
yenye kiwango cha hali ya juu.
Mkaguzi huyo
aliwataka wafanyakazi wa kampuni hiyo, kufanya kazi kwa uzalendo na uaminifu,
ili kujali na kulinda maslahi ya ya taifa.
"Mkifanya
hivyo mtaweza kujizuiya na matendo maovu, kama kujihusisha na vitendo vya
udhalilishaji ikiwemo ubakaji, wizi, ulevi kwani jeshi la Polisi, halitosita
kumchukulia hatua kali, kwa mfanyakazi yoyote atakaevunja sheria,"alisema.
Nae Mkandarasi
wa ujenzi huo pamoja na msimamizi wa mradi huo Laurent Johes na Juma Omar
Mohamed, walisema kuwa watashirikiana na jeshi la Polisi, kupitia mkaguzi huyo,
ili kufanyakazi zao kwa ufanisi.
Mapema
sheha wa shehia ya Pandani Khamis Rashid Ali alieleza kuwa, shehia kwa
sasa ipo salama na kupiga hatua katika kudhibiti na kupambana na matendo ya
udhalilishaji, kutokana na wananchi kutoa ushirikiano na jeshi la Polisi.
Hata hivyo,
alisema lazima jamii ya Pandani, iendelee kuheshimiana, ili kuhakikisha
wanawake na watoto wanabakia salama.
MWISHO. |
Comments
Post a Comment