Skip to main content

DK. MWINYI ASEMA JUKWAA LA UWEKEZAJI LA MWAKA 2025, KUWAVUTIA WAWEKEZAJI PEMBA

 


 NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema jukwaa la uwekezaji la mwaka 2025, litakuwa chanzo kikubwa cha kuwavuta uwekezaji, kutoka maeneo mbali mbali ulimwenguni, kuekeza Pemba.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana, kwenye jukwaa la uwekezaji, wakati akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari, lililofanyika maeneo huru ya uwekezaji wilaya ya Micheweni kisiwani humo.

Alisema, anaamini baada ya jukwaa hilo kumalizika, sasa wawekezaji watamiminika kisiwani, na hasa kwa vile katike maeneo hayo huru, yapo miundombinu rafiki kwa ajili yao.

Alieleza kuwa, jukwaa hilo sasa litachapuza maendeleo ya haraka ya kisiwa hicho, kama ilivyo kwa Unguja, hasa kwa vile ujenzi wa barabara kadhaa, unaendelea kwa kasi na zipo ambazo zimeshakamilika kwa kiwango cha lami.

Dk. Mwinyi alisema, hata ujenzi wa bandari za Mkoani Pemba, imeshatanuliwa na huku ujenzi wa bandari ya Shumba ukiendelea, kama ambavyo wakati wowote ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa utaanza.

‘’Naamini baada ya kukamilika kwa miundombinu yote hiyo, sasa kisiwa cha Pemba, hakitakuwa na sababu ya wawekezaji kutojitokeza,’’alifafanua.

Rais huyo wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, alisema sio miundombinu pekee, inayoendelea kurekebishwa na kuvutia wawekezaji, lakini hata uzinduzi wa mpango mkakati wa ZIPA ni sehemu nyingine.



Alieleza kuwa, kupitia jukwaa hilo, tayari ZIPA ilishazindua Mpango Mkakati wake wa mwaka 2025 hadi 2030, ambao ndani yake, yamo mambo kadhaa kama ni kipaumbele.

Alifafanua kuwa, Mpango Mkakati huo, umeanisha maeneo muhimu ya uwekezaji, ambapo kwa Pemba, vipo vivutizi maalum, kama vile vya uwekezaji wa mkakati.

‘’Ndani ya Mpango huo, unaonensha kwa sasa mwekezaji anaweza kuwekeza, uwekezaji wenye hadhi ya dola milioni 5, jambo ambalo ni tofauti na kule kisiwa cha Unguja,’’alifafanua Dk. Mwinyi.



Akiendelea kuuchambua Mpango huo Mkakati wa miaka mitano ijayo, alisema aidha unaweza kupata hadhi ya uwekezaji kwa dola milioni 2, ingawa kwa sharti lake ni kuajiri wafanyakazi zaidi ya 100.

‘’Lengo la serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufanya hivi, kwanza ni kuwavuta wawekezaji wengi zaidi, ili kisiwa cha Pemba, nacho kifunguke kiuchumi,’’alifafanua.

Hata hivyo Dk. Mwinyi alisema, Mpango Mkakati huo wa mwaka miaka mitano ijayo, ni kwa ajili ya Zanzibar nzima, ingawa kwa upande wa kisiwa cha Pemba, umewekewa mkakati maalum.

Akizungumzia sheria za uwekezaji, alisema kwa sasa Zanzibar inayosheria mpya, ambayo imeshafanyiwa marekebisho, hasa yale maeneo ambayo yalionekana kuwa na utata.

‘’Kwa sasa sheria yetu ni mpya imeondosha vikwazo, na leo (jana), tumeshazindua kanuni ambayo, inalengo la kuifanya sheria itumike vizuri zaidi,’’alisema.

Katika hatua nyingine, Rais huyo wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, alisema majukwaa kama hayo, ni muhimu kufanyika kila baada ya muda, kwani huwavuta wawekezaji kutoka maeneo kadhaa.

Alieleza kuwa, kupitia jukwaa kama hilo, wawekezaji hupata taaluma na mikakati ya serikali na fursa zilizopo katika eneo husika la uwekezaji.

‘’Unaona kwa mfano kupitia jukwaa hili, kumesainiwa kanuni, kuzinduliwa kwa Mpango Mkakati wa miaka mitano pamoja na jarida maalum, linaloelezea mpango na fursa za uwekezaji Zanzibar,’’alieleza.

Hata hivyo, aliwahakikishia wananchi wa ukanda wa Micheweni, kwamba wataifaidika na ajira pamnoja na ujenzi wa miradi ya kijamii kutoka kwa wawekezaji.

‘’Tunawashauri kuwa, kila mwekezaji anaeekeza katika eneo hilo na jingine, aone umuhimu wa kuwasaidia wananchi, katika kufanikisha miradi yao mbali mbali, kupitia faida wanazozipata,’’alifafanua.



Mapema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchimu na Uwekezaji Zanzibar Sharif Ali Sharif, alisaini kanuni ya Uwekezaji, ambayo imekuja kuimarisha na kuweka hadhi maalum ya uwekezaji Zanzibar na hasa kisiwa cha Pemba.

Alisema, inafahamika wazi, kuwa mwaka 2023, Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, alishasaini sheria ya Uwekezaji, ambayo ina mambo mingi mazuri, ikiwemo kukitaja kisiwa cha Pemba, kama eneo la mkakati.

Alieleza kuwa, sasa ni aimani yake kuona wawekezaji, wanaingia kwa wingi kisiwani Pemba, katika maeneo na visiwa vidogo vidogo.

Katika hatua nyingine waziri Sharif, alisema kanuni imebainisha mambo ya kuzingatia katika visiwa, ambavyo ni muhimu katika uwekezaji.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ‘ZIPA’ Saleh Saad Mohamed, mara baada ya kuzindua mfumo, uzinduzi wa jarida na kusaini mkataba wa ushirikiano baina ya taasisi kadhaa, alipongeza hatua hiyo.

Alisema mkataba huo umesainiwa baina ya ZIPA, Kamisheni ya Utalii na Shirika la Bandari, kwamba sasa minara iliyokuwa ikiongoza meli pekee, iwe ni sehemu ya kivituo cha utalii.

‘’Hivyo sasa, minara iliyopo visiwani, uwekezaji utawekwa, kama wanavyofanya wenzetu baadhi ya mataifa, ambayo huwa ni kivutio kwa wageni,’’alieleza.

Akigusia mfumo uliozinduliwa, alisema ni sehemu ya pili, na sehemu ya kwanza, ulizinduliwa mwaka 2023, ambapo unamsaidia mwekezaji kujisajili ZIPA, kielektroniki.



‘’Kwa uzinduzi wa mfumo kwa awamu ya pili, utamsaidia mwekezaji kuwasilisha ripoti na changamoto zake kwa wakati, pamoja na taasisi nyingine za serikali kama TRA, ZSSF, ZRA na kamisheni ya kazi kufutilia taarifa wanazozihitaji,’’alisema.

Mkurugenzi huyo Mtendaji alieleza kuwa, mfumo huo utasababidha serikali na taasisi zake, kuona kwa uwazi uchangiaji, ulipaji kodi pamoja kufuatilia kodi stahiki kwa mwekezaji.



Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 2023, imemtaka Waziri husika wa uwekezaji, kutengeneza kanuni ‘regulation’ ili utekelezaji wa sheria hiyo, iwe rahisi.

Katika jukwaa hilo la uwekezaji, wawekezaji mbali mbali wa ndani ya nje, walihudhuria, ambapo pia ZIPA ilizindua jarida lake, ambalo sasa litakuwa linachapishwa kila miezi sita.

                       Mwisho

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

HABARI ZA HIVI PUNDE

 TAARIFA za hivi punde, zilizofikia ofisi ya Pemba Today, zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, linamshikilia askari mwenzao, kwa tuhuma za ubakaji ndani ya moja ya kituo cha Polisi kisiwani Pemba Muume wa mwanamke aliyedai kubakwa na Mwanamke mwenyewe, wamedai kutokea kwa tendo hilo, na huku Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, akithibitisha kupokea kwa lalamiko hilo.... Kwa taarifa zaidi ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu, ambao kukuhabarisha ni fahari yetu...