MAJIMBO YA UCHAGUZI CHINA KAMA TANZANIA, HAYASHIKIKI KWA WANAWAKE, RAIS WAO AENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI
NIPO,
jiji la Beijing linalopatikana takriban saa 12, kutoka uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Zanzibar, kwa usafiri wa anga.
Jiji hili ni
moja kati ya majiji manne yayounda taifa la China, likiwemo pia lile la
Shanghai, ingawa Beijing ndio mji mkuu.
Lenyewe
limezungurukwa na milima mikubwa kwa upande wa magaribi, ingawa kusini
mashariki na kaskazini mwa jiji hilo, linaujirani na bahari iitwayo Bohai.
Jiji hili,
lina ukubwa wa skweya kilomita 16,410, ambapo hadi mwishoni mwa mwaka 2023,
lilikuwa na wakaazi milioni 21.858.
Kati yao
hao, wanaoishi ndani ya mji husika wa kudumu ni watu milioni 19.198, sawa na
asilimia 87.8, huku ambao sio wa waakzi wa kudumu ni milioni 8.204 sawa na
asilimia 12.2.
Mpaka mwezi
April 2023, Beijing pekee inazo wilaya 16 ‘municipal districs’
ikiwemo ya Xichenga, Chaoyang, Fengatai, Shijingshan, Hiaidian, Miyun pamoja na
wilaya ya Yanging.
Ukingia
ndani ya jiji la Beijing, mara zote utakaribishwa na mazingira mazuri ya kijani
kibichi kinachotawala pembezoni mwa barabara kuu, inayotokea uwanja wa ndege wa
kimataifa wa China.
Uwingi wa
watu na gari, serikali ya China iliamua kuzijenga kama njugu barabara za juu ‘fly
over’, kusudi kupunguza kama sio kuondosha kabisa, foleni.
Ingawa kwa
taifa lenyewe la China, linaundwa na maeneo makubwa maalum mawili ‘special administration’
likwemo la mji wa Macao.
ELIMU KWA
MATOTO WA KIKE CHINA
Kwa mujibu
wa msomi nguli wa historia ya China Dk. Sun Jiwen, anasema serikali ya rais wa
sasa wa taifa hilo Xi Jinping, amefanikiwa kuweka mazingira ya kielimu
yanayowawezesha watoto kusoma.
Akasema, watoto
wa wakike wamekuwa mastari wa mbele kuliko wa kiume, kuanzia ngazi ya elimu ya
msingi hadi ile ya vyuo vikuu.
Akatoa mfano
kuwa, kila mwaka kila wanafunzi 100, wanaomaliza elimu ya vyuo vikuu, kwa
shahada ya kwanza watoto wa kike huwa na 52, na 48 huwa ni wanaume.
Vivyo hivyo
kwa elimu digree ya kwanza na kuendelea, kwa mwaka watoto wa kike huwa 48,
idadi ambayo wamepitwa kidogo mno na wale wa kiume.
HALI
IKOJE KWENYE BUNGE LA CHINA
Kwenye taifa
la china, linaloundwa na majimbo makubwa 23 yanayobeba wapiga kura zaidi ya
bilioni 1.5, ingawa bado wanawake wanaogombea, huangushwa.
Dk. Sun
Jiwen nilipomuuliza sababu ya idadi ya wanawake kuwahi kumaliza kwa wingi vyuo
vikuu, ingawa Bungeni kuwa wachache, anasema bado hawajaaminika.
‘’Bado
wapiga kura wanaume hawajawaamini wagombea wanawake, na ndio maana kila wabunge
100, wanawake ni sawa na 26 pekee,’’anasema.
JUHUDI ZA
SERIKALI YA CHINA
Profesa He
Wenping, anasema moja ni kwa rais aliyepo sasa kuandaa mazingira ya kuwainua
wanawake, ili waweze kugombea na kuchukua nafasi ndani ya Bunge la china.
‘’Kwa mfano
wanawezeshwa kielimu, mikopo ya kukukuza pato lao, wafikirie kugombea na
kupambana na wanaume majimboni,’’anasema.
Jingine ipo
mikopo ya kujiendeleza elimu ya juu, maana imegundulika wengi wanaogombea wamekosa
kujiamini sababu, ikiwa ni kukosa elimu ya juu.
Akifungua
mafunzo ya siku 20 kwa waandishi wa habari wa Zambia, Gambia, Ethiopia,
Tanzania, Kenya na China, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la
Mawasiliano ‘CICG’ Han Likiang, anasema bado vyombo vya habari vinakazi ya
ziada.
‘’Wanawake
ni sehemu ya taifa, ni sehemu ya nguvu kazi, ni sehemu ya familia ni sehemu ya
viongozi, haya yanahitajika kufafanuliwa na waandishi wa habari,’’anasema.
WANAWAKE
WENYEWE WA CHINA
Young
Jujian, anasema wamekuwa wakifanyavyema kushiriki kampeni, chaguzi mbali mbali
na kuwaunga mkono wagombea wanaume, ingawa inapofika wakati wao kuomba nafasi,
huangushwa.
Hei Ujun
anasema, wamekuwa wachache ndani ya bunge la China, kwani wapo wanawake
wamekuwa wakiwafanyia uadui wa kidemokrasia wakati mwingine.
‘’Lakini hii
tabua ipo duniani kote, kuanzia nchi zilizoendelea na hata zilizoendelea, maana
wanawake hutiwa sumu na baadhi ya wanaume na kukosa kura,’’anasema.
WANAUME
WA CHINA
Hu Iyain
anasema, histori ya taifa lao tokea utawala wa rais wa kwanza Mwenyekiti Mao
Dzodung, iliwasahaulisha wanaume kuwapa nafasi wanawake.
‘’Kwa sasa
hali inaendelea kupanda juu, maa asilimia 26 ndani ya Bunge la China ni
wanawake, hali ambayo kabla haikuwa ikiridhisha,’’anasema.
Hey Idong,
anasema kidogo kidogo wapiga kura wameanza kuwazoea wagombea wanawake, jambo
ambalo awali lililonekana kama kituko.
Sun Lyu,
anakiri kuwa wapo baadhi ya wapiga kura wamekuwa na uwelewa taofauti wanapoona
mgombea mwanamke, na ndio maana, wapo wanaoangushwa hata kabla ya uchaguzi
mkuu.
UZOEFU
KATIKA MAENEO MINGINE
Zanzibar,
kwa mfano katika kisiwa cha Pemba yapo majimbo 18 ya uchaguzi, ingawa wanawake
wameng’ara katika majimbo manne.
Ni jimbo la
Chambani, Gando, Wete na pamoja na jimbo Konde wote kwa nafasi ya Uwakilishi
huku wanaume wakiendelea kushikilia majimbo 14, ingawa kwa nafasi ya ubunge ni
yote.
WANAHARAKATI
Dk. Mzuri
Issa Ali anayekiongoza Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania
TAMWA-Zanzibar anasema, wanategemea mno, kuona uchaguzi wa mwaka huu, wanawake
wanachukua hatamu ya uongozi.
‘’Tunaendelea
kuendesha mradi wa kuwahamasisha wanawake na uongozi, kupitia vyombo vya habari
na wapo zaidi ya 20 kwa Unguja na Pemba, waliokwisha onesha nia, sasa ni kazi
ya wapiga kura kuwaamini,’’anasema.
Sifuni Ali
Haji kutoka Mtandao wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’, analalamikia vyama
kutowaunga mkono wanawake, wanapoonesha azma ya kugombea.
VYAMA VYA
SIASA
Mwenyekiti
wa chama cha ACT-Wazalendo Othman Massoud, anasema wanawake ndio jeshi kubwa
ndani vyama, hivyo ni wakati na wao kugombea, badala ya kutegemea viti maalum.
‘’Viti vya
wanawake vinaweza kuondoka siku moja, hivyo lazima wanawake wajipange
kisaikolojia na kuingia majimboni, maana katiba haijawakataa,’’anasema.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa kusini Pemba, Yussuf Ali Juma, anasema chama hicho, kimekuwa na
utaratibu wa kuwajenga wanawake kiuongozi, kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.
‘’Ndio maana
hata wawakilishi hao wanne waliofuzu majimboni ni kutoka CCM, ni baada ya
kuwawezesha ngazi ya shina na sasa wako taifa,’’anasema.
Rais wa sasa
Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, anasema lazima vikwazo
viondolewe na wanaume na kuwaachia wanawake kupata uongozi.
Wakati
akiadhimisha miaka mwili ya uongozi wake ndani ya ukumbi wa zamani wa baraza la
Wawakilishi Wete Pemba, Rais wa Zanzibar Dk. Mwinyi, aliahidi kuendelea kuwapa
nafasi wanawake.
‘’Ijapokuwa
mawaziri na makatibu wakuu wote niliowateua wanafanya vuzri, lakini ukweli ni
kwamba wanawake wako juu zaidi ya
wanaume,’’alisema.
SERA/MIKATABA INASEMAJE
Mataifa kadhaa ulimwengini, Tanzania ikiwemo zimeridhia mikataba na matamko ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kwenye uongozi.
Hii ni kama ilielezwa katika tamko maarufu la la Haki za Binadamu la mwaka 1948.
Zanzibar imesaini mikataba ya kikanda na kimataifa, lakini safari ya utekelezaji ni ndefu kwa sababu hadhi sawa kwa wanawake na wanaunme katika uongoz.
Mara nyingi unapofanyika uteuzi nafasi wanazopewa wanawake huwa hazina hadhi sawa na zile wanazokabidhiwa wanaume.
Vyama vya siasa navyo vinawaacha nyuma wanawake katika kuwapa nafasi za kugombea kama, inavofanyika kwa wanaume na jina la mwanamke likipita huwa kama bahati mbaya.
Taarifa ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, inafafanua kuwa, kwa uchaguzi wa 2020, wanaume walioteuliwa na vyama kugombea kuingia katika Baraza la Wawakilishi walikua 190 na walioshinda ni 42 wakati wanawake walikuwa 61 na walioshinda ni wanane (8).
Taarifa za Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) na Umoja wa Mabunge (IPU) za 2017 zimeonesha kuwepo ongezeko dogo la viongozi wanawake katika serikali na mabunge.
Maana katika majimbo 50 ua uchaguzi ya Zanzibar, wanawake katika baraza la kutunga sheria, wanane hii ni saw ana asilimia16, wabunge ni wannne kwa asilimia 8, mawaziri ni sita sawa na asilimia 33 na Makatibu Wakuu ni saba sawa na asilimia 39.
Kati ya wakuu wa mikoa watano Zanzibar, wanawake ni wawili, huku wakuu wa wilaya 11, wanawake wakiwa wawili pekee, ambapo na masheha wanawake ni 81 kati ya 388.
Katiba ya Zanzibar ya 1984, kwenye kifungu cha 11 na cha 14, vimeweka wazi kuwa kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu.
Aidha Dira ya Zanzibar ya 2050 imeelezea jinsi gani masuala ya usawa wa jinsia juu ya kuondoa unyanyasaji na kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wanawake.
Sera ya jinsia inaeleza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya utoaji maamuzi, katika ngazi zote ni mdogo na kwa hivyo serikali, kwa kushirikiana na wadau wengine, itafanya juhudi kuona makundi yote na yaliyopembezoni.
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC) ambayo mkataba wake ulitiwa saini mwaka 2008 inaeleza, kutaka kuondoa utafauti na kuwatenga wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kusaidia kuwepo usawa wa kijinsia katika nchi wanachama na kufikia asilimia 50/50 kwenye maamuzi.
Mwisho





Comments
Post a Comment