Skip to main content

‘ZLSC’ CHAPIGA HODI YA KISHERIA WINGWI MJANAZA

  


NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ sasa kimeelekeza nguvu yake kwa wananchi wa shehia ya Wingwi Mjananza wilaya ya Wete Pemba, kwa kambi ya siku tatu, ya kutoa elimu, ushauri na msaada wa sheria bila ya malipo.

Kambi hiyo, ipo ndani ya skuli ya Msingi ya Mjananza, ambayo ilianza jana April, 16, na ikitarajiwa kumalizika kesho majira ya saa 8:15 jioni.

Akizungumza na wananchi hao, juu ya utaratibu wa utoaji wa msaada huo, leo April 17, 2025 skulini hapo, Afisa Miradi wa ‘ZLSC’ Beny Louis Mlingi, alisema kwanza, mwananchi atapaswa asajiliwe, kwenye fomu maalum kambini hapo.

Alieleza kuwa, baada ya hapo atakutana na wanasheria nguli pamoja na mawakili na Vakili, wanaofanyakazi Kituo cha Huduma za Sheria, kwa ajili ya kusikilizwa lalamiko lake.



Alifahamisha kuwa, katika kambi hiyo, inawakaribisha wananchi wenye changamoto za kisheria, kama vile migogoro ya mipaka, ardhi, matunzo kwa watoto, waliokosa vyeti vya ndoa, vya kuzaliwa.

Eneo jingine wanaloshughulikia na kumpa muathirika ushauri na maelekezo ya kisheria na wale ambao wamekoseshwa mirathi, kutomaliziwa mahari pamoja na wale ambao, kesi zao zimekwama vituo vya Polisi.

‘’Lakini hata kama kuna mtu aliombwa rushwa wakati anafuatilia haki zake, au wakati mwingine alifanyiwa udhalilishaji na kiongozi, tunawahitaji kwa ajili ya kuwashauri kisheria,’’alifafanua.

Kwa upande wake Afisa Sheria wa ‘ZLSC’ Asha Maulid Khamis, aliwataka wananchi hao, kuondoa woga, wakati wanapofuatilia haki zao.




‘’Hatakama muume au baba amekutendea visivyo au wakati mwingine kuna mjomba au kaka, amekalia mirathi kwa muda sasa, ni vyema kwa wananchi wakatufika kutueleza na kuwashauri kisheria,’’alieleza.

‘’Kwa mfano tulipokuwa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake, zipo kesi za mirathi tumezipata na sasa wale warithi wanaweza kurithi, baada ya kuwapa ushauri na msaada wa kisheria,’’alifafanua.

Hata hivyo, aliwakumbusha wananchi kuwa, ‘ZLSC’ haishughulikii upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa pekee, bali hata migogoro kama ya ndoa, ardhi, madeni tunawakaribisha.









Sheha wa Mjananza, Hamad Said Ali, alisifu ubunifu wa ‘ZLSC’ wa kufunga safari na kuwafuata wananchi wake, jambo ambalo kama sio kuwepo wao, wengeendelea kuishi na changamoto zao.

Hata hivyo, amewakumbusha wananchi, ambo kwa jana na leo hawakupata nafasi ya kufika kwenye kambi hiyo, nafasi ya kesho ipo, na wafike ndani skuli ya Msingi Mjananza, ili kupata ushauri wa kisheria.

‘’Sio busara kama mtu anamgogoro wa ardhi, mirathi, matunzo ya watoto kukaa nyumbani, kwani wanaotoa ushauri na msaada wa kisheria, wapo ndani ya shahia yangu,’’alifafanua.

Wakizungumza nje ya kambi hiyo baada ya kuhudumiwa, wananchi wa shehia ya Mjananza, walielezea kufurahishwa kwao, na msaada wa kisheria walioupata.

Moza Haji Hamad na Salma Omar Pandu, walisema wanatamani kuona kila mwaka, wanapata kambi kama hizo, ili kufikisha malalamiko yao.

Kambi hiyo ya siku tatu, ilianza jana na inatarajiwa kumalizika kesho April 18, 2025, ambapo tayari ‘ZLSC’ kimeshawahudumia wananchi 112, wakiwemo wanawake 80 na wanaume 32 wa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake hapo juzi.

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’, kimeasisiwa mwaka 1992, kwa kutoa huduma za maktaba, kuwasomesha wasaidizi wa sheria na kutoa elimu, msaada na ushauri wa kisheria kwa wananchi bila ya malipo.

Mwisho  

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

HABARI ZA HIVI PUNDE

 TAARIFA za hivi punde, zilizofikia ofisi ya Pemba Today, zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, linamshikilia askari mwenzao, kwa tuhuma za ubakaji ndani ya moja ya kituo cha Polisi kisiwani Pemba Muume wa mwanamke aliyedai kubakwa na Mwanamke mwenyewe, wamedai kutokea kwa tendo hilo, na huku Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, akithibitisha kupokea kwa lalamiko hilo.... Kwa taarifa zaidi ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu, ambao kukuhabarisha ni fahari yetu...