Skip to main content

WADAU UANDAAJI MALIPO 'ZSSF' PEMBA TUMIENI MIFUMO KURAHISISHA TAARIFA

 


NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Pemba, Abdulwahab Said Abuu-bakar aliwataka wadau wanaohusika na uandaaji wa malipo ya michango katika mifumo ya Mfuko wa hifadhi ya jamii (ZSSF) kutumia mifumo hiyo kwa usahihi ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wanachama wake.

Aliyasema hayo April 15, 2025 katika mkutano wa kuwajengea uwezo wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa (ZSSF) Tibirinzi Chake Chake Pemba.

Alisema kumekua na malalamiko ya ucheleweshwaji wa upatikanaji wa mafao ya ustaafu kutoka kwa wanachama, yanayosababishwa na taasisi kushindwa kuweka kumbukumbu vizuri, katika mifumo hiyo.

Hivyo alisema ni vyema kwakila taasisi kuhakikisha inatimiza majukumu yake vizuri ili kupunguza malalamiko hayo kwa wastaafu wa serikali na taasisi binafsi.

"Ni vyema  taasisi zihakikishe  zinatimiza majukumu yake vizuri ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wastaafu wa serikali na taasisi binafsi" alisema.

Alieleza kua  serikali imeandaa utaratibu wa kuwalipa wastaafu mafao yao ndani ya wiki mbili baada ya kustaafu, hivyo amewataka wadau hao kutumia vizuri  mifumo ya habari na mawasiliano ili kulifanikisha hilo.

Alisema mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) inatumia mitandao ya kijamii ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa, hivyo amewaomba wadau hao kutumia mitandao hiyo pamoja na kushajihisha wengine kuitumia ili kuondoa changamoto ya ucheleweshwaji wa mafao kwa wanufaika.

Aidha aliipongeza (ZSSF) kwa kua na utaratibu wa kukutana na wadau hao mara kwa mara, ambayo ni hatua muhimu katika kuchochea maendeleo, huku akiwasihi kuendeleza utaratibu huo.



Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii Afisa hifadhi ya jamii Pemba Said Omar Juma alisema,  Mfuko wa hifadhi ya jamii ni kwaajili ya watu wote wenye ajira rasmi na zisizo rasmi.

Alieleza kua hifadhi ya jamii inaumuhimu mkubwa kwa jamii kwani inamuhakikishia kipato mwanachama baada ya kustaafu pamoja na kutoa ulinzi wa kifedha kwa wanufaika.

Alisema ingawa kunachangamoto ya uelewa mdogo kwa wananchi, pamoja na uhaba wa mashirikiano kutoka kwa wananchi, lakini wamekua wakifanyajitihada mbali mbali ikiwemo kutoa elimu kwao.

Alisisitiza kua hifadhi ya jamii ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa, hivyo ni wajibu wa serikali, taasisi binafsi na wananchi kuungamkono ili kuzidi kuimarika.

"Hifadhi ya jamii ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa, hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuanzia  serikali, taasisi binafsi na wananchi kuungamkono ili uzidi kuimarika" alieleza.

Nae Afisa tehama wa ZSSF Pemba Madi Jafar Khamis alisema matumizi ya mifumo katika ukusanyaji wa taarifa itasaidia kuweka sawa kumbukumbu za fedha pamoja na kuhifadhi taarifa kwa usahihi na kwa wakati.

Akiwasilisha mada kuhusu fidia ya ajalikazini inayotolewa na( ZSSF) Ali Mtemani Hussen Afisa hifadhi ya jamii Pemba alisema, fidia hio ni haki ya msingi ya kila mwanachama atakaepata kadhia hii,  huku akisisitiza kua (ZSSF) ipo kwa ajili ya kustawisha jamii.

Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi ZSSF Pemba Msabah Massoud Msabah aliwataka wadau walioshiriki mafunzo hayo kuendelea kutumia mitandao ya mfuko huo kwa kutoa maoni na ushauri ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi.




Hatahivyo alitoa shukrani kwa wadau walioshiriki mafunzo hayo huku akiwaomba kuripoti changamoto zao ili kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Nae mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Ali Talib Bakkar kutoka wizara ya Fedha na mipango, alitoa pongezi kwa  mfuko wa hifadhi ya jamii kwa kuwapatia mafunzo hayo, huku akiwataka wadau wengine kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu ili wanachama wapate mafao yao kwa haraka.

   MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...