Skip to main content

KAIMU MKURUGENZI "ZSSF" ATOA NENO KWA WAAJIRI

 


NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

KAIMU Mkurugenzi Mwendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Pemba Msabah Masoud Msabah, aliwataka waajiri kufuata sheria zilizowekwa na Mfuko huo ili kuhakikisha upatikanaji wa haki za msingi za wanachama wao.

Aliyasema hayo April 16 2025, wakati akizungumza na wadau wanaohusika na uandaaji wa malipo ya michango katika mfuko huo kutoka taasisi binafsi, huko Tibinzi Chake Chake Pemba.

Alisema iwapo waajiri watafuata sheria zilizowekwa na mfuko huo, itasaidia kupata haki zao zote za msingi ndani ya mda husika, jambo ambalo ni kipaombele cha mfuko huo.

Alisema kwa sasa mfuko umeanzisha mfumo maalumu, utakaomuwezesha mwanachama kuweka pamoja na kupata taarifa zake zote za mwenendo wa uchangiaji wake, hivyo ni vyema kwa waajiri kutumia mfumo huo ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa.

"Mfuko wa hifadhi ya Jamii (ZSSF) umeandaa mfumo  maalumu utakaomuwezesha mwanachama kupata taarifa zake kwa urahisi ( employers potlal), basi ni vyema kwa waajiri kutumia mfumo huo ili kuboresha huduma ", alieleza.

Hata hivyo alitoa wito kwa washiriki hao kuendelea kutoa mashirikiano ili kuimarisha huduma za mfuko huo.



Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii  Afisa hifadhi ya jamii Pemba Said  Omar Juma alisema kua, mfuko huo unaumuhimu mkubwa kwa jamii kwani inamuhakikishia kipato mwanachama baada ya kustaafu pamoja na kutoa ulinzi wa kifedha kwa wanufaika.

Hata hivyo alisema Mfuko wa hifadhi ya jamii unahuduma ya uchangiaji wa hiari ambao walengwa wake ni wajasiriamali, mamalishe,  boda boda na watoto wenye umri kuanzia siku moja hadi miaka 18, hivyo aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo ipasavyo.

Alisema iwapofursa hiyo itatumika ipasavyo itasaidia kuongeza usawa kwa jamii, pamoja na kuchangia katika miradi ya maendeleo kutokana na uwekezaji unaofanywa na mfuko huo.

Hata hivyo akiwasilisha mada kuhusu fao la ajali kazini afisa huyo alisema ni vyema mwanachama aliefikwa na kadhia hiyo kufuata taratibu zilizowekwa ikiwemo kuwasilisha taarifa za ajali kazini mapema iwezekanavyo.

Nae Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa mfuko huo Pemba Madi Jaf, akiwasilisha mada kuhususu upatikanaji wa huduma za wanachama kwa njia ya mitandao alisema kwa sasa mfuko unaprogramu tatu zitakazomuwezesha mwanachama kupata taarifa zake.

Hivyo aliwataka wadau hao kuitumia pamoja na  kutoa elimu kwa wanachama  wengine kujiunga na programu hizo ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi ili kuondosha usumbufu na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wameshauri mfuko huo kuboresha zaidi mifumo hio, ili itoe taarifa kwa wakati na usahihi pamoja na kuipongeza "ZSSF" kwa kuwapatia mafunzo hayo yatakayowasaidia katika utendaji wao.

Awali katika ufunguzi wa mkutano huo Mratibu  wa tume ya maadili ya viongozi wa Umma Abdullah Muhammed Mbarouk alisema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watendaji hao ili kuimarisha utendaji kazi wa taasisi zao.

Hata hivyo aliwaomba watendaji hao kutumia lugha nzuri wakati wa kutoa huduma kutokana na umuhimu wao katika taasisi zao.

Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ulianzishwa   chini ya sheria ya mfuko wa Usalama wa Zanzibar Na 2 ya 1998, ikiwa miongoni mwa  kazi zake ni kuhifadhi michango ya wanachama na kutoa mafao kwa wanachama wake, huku fao lake kuu likiwa ni fao la ustaafu  na inafanya kazi  katika visiwa vya Unguja na Pemba.

MWISHO

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...